Achari Ya Ndimu

Achari Ya Ndimu

Vipimo

Ndimu / Limau - 23

Chumvi - 3 Vijiko vya supu

Bizari ya manjano - ½ Kijiko cha chai

Pilipili nyekundu nzima - ½ Kikombe

Pilipili ya sambal- 2 Vijiko vya supu

Masala ya unga - 1 Kijiko cha supu

Karoti - 4

Maji ya ndimu - 1 ½ Vikombe

Siki - ½ Kikombe

 

Namna Ya Kutayarisha

  1. Osha ndimu na ikiwa ni rangi ya kijani unaweza kuchambua maganda, kisha zikate vipande vipande.
  2. Katika chupa la kiasi, changanya vipimo vyote isipokuwa karoti, maji ya ndimu, siki na sambal (pilipili ya chupa).
  3. Weka chupa pahali pa joto au juani kwa muda wa wiki 2 – 3.
  4. Halafu ikishaiva ongezea karoti zilizo katwa katwa, maji ya ndimu, siki na sambal na hakikisha mchanganyiko wa  maji ya ndimu imefunika ndimu vizuri.
  5. Na itakuwa tayari kwa kuliwa na wali na venginevyo.

 

 

 

Share