Mume Mkali Sana, Hana Raha Na Mimi, Hapendi Niwe Na Furaha, Ananifanyia Vitimbi - Anasema Hakunipenda Ila Amenioa Tu!

SWALI:

 

asalam aleikum. ndugu zangu wa alhidaaya nina swali langu nataka uniffahamishe, mimi niko na mume wangu twaishi pamoja lakini hatuelewani kabisaa. na tangu niishi nae sasa nina miaka 7 nimezaa nae watoto. na tabiya yake nimkali sana nakila akiniona hana raha na mimi na mimi sijamfanya jambo lolote kubwa na mungu ndio shahidi yangu ndio anayaona. na pia hapendi mimi nione raha ama nifurahike mpaka kwenye roho yangu hua yaniuma nakumuogopa na pia hua yuwaniambia mambo mabaya nakunionesha viimbi ndani ya nyumba yake bila kosa lolote. Ikiwa nimefanya kosa dogo hua hata hajali kuni azirisha kwa watu kuambia mke wangu hivi vile mpaka hii roho yangu yaniuma. na mimi ni mtu siwezi vita na yeye ni mtu wa vita hataki hata kitu chochote niseme hata kama nichaukweli na yuwapenda kuniambia wewe mwanamke gani? Mimi sikukupenda nakuowa tu. Na kama kitu pengine sijapendelea hua ataka nipiga. na mimi niko nchi za ulaya sina mama wala baba niko peke yangu, sasa sijui ndugu zangu naomba wenu ushauri tafadhali.


 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu mumeo aliye mkali asiyependa uwe na furaha.

 

Hakika hili ni tatizo sugu katika jamii yetu popote ilipo, tukiwa tupo Afrika Mashariki au Ulaya. Ni masikitiko makubwa kuwa wenye kuathirika na kutatizwa wengi ni dada zetu katika Imani na Uislamu.

 

Hata hivyo, kama tulivyokariri mara nyingi ni kuwa matatizo haya na mitihani hii inatufika kwa yaliyochuma mikono yetu. Allaah Aliyetukuka Anatuambia:

 

Na misiba inayokupateni ni kwa sababu ya vitendo vya mikono yenu, na Allaah Anasamehe mengi” (42: 30).

 

Haya yaliyochuma mikono yetu ni kukosa kufuata maagizo ya Allaah Aliyetukuka na Mtume Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Lau tungekuwa tukifuata maagizo hayo basi tungekuwa mbali na hayo. Mara nyingi huchukulia mwanamme anayetoka Ulaya anakuwa ni mzuri na ana pesa kwa hiyo hukubali mara moja kuhusu ndoa hiyo bila kujua Dini ya mtu huyo, maadili yake na tabia zake. Haya kwa ufupi tuliyoyasema ni muhimu sana, nayo ni:

 

1.     Dini ya mwanamme mwenyewe pamoja na msimamo wa Uislamu.

2.     Maadili yake.

3.     Tabia yake.

 

Bila kutazama hayo basi matatizo yanapotokea huwa ni mtu mwenyewe wa kujilaumu. Kwa kuwa tatizo hilo tayari limekukabili hatuna budi nasi kukupatia nasaha njema ili uweze kuepukana na hayo. Inatakiwa ufuate mfumo ufuatao:

 

1.     Mbali na kuwa ni mkali ni muhimu upate muda ambao amemakinika na kutulia ili uzungumze naye kuhusu maisha yenu ya wakati huu.

 

2.     Ikiwa atakuwa amebaki na ukali inabidi mwanzo uwajulushe wazazi wako mbali na kuwa wapo mbali sana nawe kuhusu yanayokusibu katika unyumba. Na ikiwa wazazi wake wako Ulaya karibu na mji au nyumba yenu itabidi uwaeleze yanayoendelea ili upate ufumbuzi mzuri.

 

 

3.     Na ikiwa wote wazazi wako na wake wapo mbali itabidi uende katika Markaz (centre) ya Kiislamu au Msikiti ili uende ukaonane na Imaam, Shaykh mwadilifu, mwenye elimu na mcha Mungu ili umueleze matatizo unayokumbana nayo katika maisha ya unyumba. Imaam au Shaykh atamuita mumeo ili awasikilize nyote wawili na atoe uamuzi wa kuweza kurekebisha uovu huo wa mumeo au kuachanishwa naye kwani mumeo hana sifa kabisa za mume Muislamu.

 

Tunamuomba Allaah Aliyetukuka Akupatie ufumbuzi kwa tatizo hilo ulilonalo na Akupatie badali iliyo njema.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

 

Share