Kuwa na Mume Hataki Kufanya Kazi Anapoambiwa Huwa Mkali, Nachukiwa Hadi Huwa Sitaki Kulala Naye

SWALI:

 

Asalam aleikum ndungu yangu muislamu

Mtalaka wa amii yangu ndie aliemleta mume wangu kunitaka kwa wazazi wangu.  Tuli waulizia na tukaambiwa ni familia nzuri na ana dini yake. Nika sali istikhara na nika kubali kuolewa. Wazazi wangu na familia waka furahi na tuka fanya harusi. Ndugu yake mume wangu ndie alikuja kumuolea. Baada ya harusi nikakaa mie mitatu mpaka nilipo kutana na mume wangu. Tuka fanya harusi yetu na alhamdulillah mambo yakawa mazuri. Baada ya kukaa nae aka hataki kufanya kazi kwa sababu ata kwenda kusoma na shule watampa pesa nayi ni baad ya mie kadha kuapata hayo mapeni nikawa na mwambai afanye kazi tuwe na akiba nyumbani tukitokewa na jambo lolote tuwe na akiba yeye ni mtu mmoja mkali sana huwa ana ni rukia kama mtoto hata mamake na ndugu zake pia ana wafnya hivyo familia yake wana sema ana tabia mzito sana na mimi na jaribu kumfurahisha kwa kila njia lakini pia haoni mpaka nikawa nakataa mara ingine kulala nae jee nitakuwa na fanya makosa hata kama sina hamu nae.

 


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kuwa na mume asiyetaka kufanya kazi. Jambo la mume au mke wakati mwengine kuwa mkali kwa mwenziwe ni suala lisilo epukika wakati mwingine kwani kila mmoja ameumbwa na maumbile yake. Hata hivyo, maumbile ya ukali huweza kubadilishwa na badala yake kukawa na upole na kushauriana.

 

Hata hivyo, tayari una mume ambaye ni mkali jaribu sana kuwa na tabia ya upole, ulaini, utulivu na subira kwani hizi ni tabia ambazo huangusha ukali na usimba wa mtu. Allaah Aliyetukuka Anatueleza: “Na tafuteni msaada kwa kusubiri na kwa kuswali; na kwa hakika jambo hilo ni gumu isipokuwa kwa wanyenyekevu” (al-Baqarah [2]: 45).

 

Usifanye makosa ya kumyima mumeo haki yake yake ya kitanda kwani ukifanya hivyo mumeo atakuwa ana madhambi kwa anayoyafanya nawe utakuwa mkosa nambari mbili. Mpe haki yake ili usipate madhambi mbele ya Allaah Aliyetukuka kwani kwa kufanya hivyo huenda ukauteka moyo wake na hivyo kubadilika kwa njia iliyo nzuri.

 

Mbali na ukali wake jaribu kutafuta wakati mzuri wa kuzungumza naye, na katika kuzungumza tumia hekima na mawaidha mazuri. Na kufanya hivyo huenda ukambadilisha na tabia yake hiyo mbaya akawa na tabia na maadili mema na mazuri. Usichoke dada yetu kwani kwa kufanya kazi hiyo utakuwa na ujira ulio mkubwa mbele ya Allaah Aliyetukuka.

 

Ikiwa unaona baada ya kufanya yote hayo bado mumeo yuko vilevile itakuwa ni vyema uitishe kikao baina yako, yake, familia yake na yako au wawakilishi wa familia hizo zenu mbili ili mzungumzie kuhusu tatizo hilo mlilo nalo. Twatarajia mema kwa idhini ya Allaah Aliyetukuka. Pia kithirisha du’aa kwa Allaah Aliyetukuka haswa katika nyakati ambazo du’aa hukubaliwa huku ukimlilia Mwenye kubadilisha nyoyo Ambadilishe mumeo. Nasi tukio pamoja nawe katika du’aa hizo.

 

Na Allaah Anajua zaidi.

 

 

Share