Alipokosa Kuzini Na Kijakazi Alikuwa Anatumia Mikono Kujitoa Matamanio- Sasa Nguvu Zimemwisha Atumie Dawa Au Vyakula Gani?

SWALI LA KWANZA:

 

Mimi ni kijana ambaye nilizoea sana kufanya tendo la ndoa na kijakazi wetu. Ilifikia wakati nikimkosa nikijifurahisha mwenyewe kutumia mkono. Tabia hii mbaya nimekua nayo kwa miaka mingi sasa hadi imefikia wakati huwa na maumivi sana ya mgongo na mishipa. Vile vile nahisi sina mguvu tena za kiume. Mimi bado sijaoa. Je, ni dawa gani au vyakula vipi naweza kutumia kurudisha hali yangu ya kawaida.

 

 

SWALI LA PILI:

 

Aslm alkm. Nauliza hivi ni vyakula gani au vitu vipi alivyopendekeza mtume wetu Muhammad (s.a.w) ambayo vinaongeza nguvu za kiume. Na je kama mume ana upungufu wa kuzalisha mwanamke ni vitu vipi apasavyo kutumia ili kumsaidia?

 

 

 

 

 


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Mwenye Swali la pili tunapenda kukukumbusha wewe na wote wenye kuzoea kufupisha Salaam au kufupisha kumswalia Mtume wetu (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kuwaombea radhi Maswahaba au kufupisha kumtukuza Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala), ni bora waache kufanya hivyo na waandike kwa urefu kwani zote hizo ni 'Ibaadah na ni bora kuzifanya kwa ukamilifu ikiwemo katika kuandika, kutamka n.k. Pia kuongeza neno 'Ta'ala' kwenye Salaam kwa kusema 'Assalaamu 'Alaykum wa RahmatuLlaahi Ta'ala wa Barakaatuh', si jambo tulilofundishwa katika Salaam na hivyo ni bora mtu kuliepuka katika Salaam.

 

 

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu vyakula vinavyo ongeza nguvu za kiume.

 

Ama ukosefu wa nguvu za kiume ni ugonjwa ambao unawakabili wanaume kwa sababu moja au nyingine. Ikiwa huo ni ugonjwa inabidi tutafute dawa kama alivyotuagiza Mtume wetu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Hakuna ugonjwa isipokuwa una dawa yake. Hivyo, tafuteni dawa enyi waja wa Allaah”. Hivyo, ushauri wetu ni kila mwenye tatizo hilo aende kwa twabibu au daktari aliyebobea katika masuala hayo.

 

Ama ndugu yetu ambaye alikuwa anazini na kijakazi ni madhambi makubwa katika Uislamu.

 

Jambo hili Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Amelikanya na kutuonya hata tusilikaribie kabisa: 

((وَلاَ تَقْرَبُواْ الزِّنَى إِنَّهُ كَانَ فَاحِشَةً وَسَاء سَبِيلاً))

 

((Wala msikaribie uzinzi. Hakika huo ni uchafu na njia mbaya)) [Al-Israa:32]

 

Soma maelezo yafuatayo kuhusu ubaya na madhara yake:

 

 

Anaishi Na Kuzini Na Mtu Asiyemuoa Lakini Anaswali, Je, Swalah Zake Zinakubaliwa?

 

 

Kufanya Zinaa Na Kumuoa Mwanamke Aliyeshika Mimba

 

Isitoshe baada ya kukosa kuzini akawa anazini na mkono, ambayo pia ni madhambi katika Dini. Ushauri wetu mwanzo ni kuwa ndugu yetu huyo atubie kwa kutekeleza masharti yaliyowekwa na sheria. Masharti yenyewe ni:

 

1.     Kuacha maasiya.

2.     Kujuta katika kufanya hayo maasiya.

3.     Kuazimia kutorudia makosa hayo.

 

Baada ya hapo atafute dawa kwa tatizo hilo lakini dawa yenyewe haitoweza kufanya kazi ikiwa utaendelea kujichua sehemu za siri kwa mkono.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share