Mwanaume Kutoboa Sikio Swalah Zake Zinakubaliwa?

SWALI:

 

 Kijana wakiume ametoboa sikio na anasali vipi ibada yake?


 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kutoboa sikio kwa mwanamme.

Kujieguza maumbile kwa kujifananisha na jinsia nyingine ni hila za Shaytwaan ambazo ameahidi kuwapoteza waja na Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Ametuonya naye:

(( لَّعَنَهُ اللّهُ وَقَالَ لَأَتَّخِذَنَّ مِنْ عِبَادِكَ نَصِيبًا مَّفْرُوضًا)) ((وَلأُضِلَّنَّهُمْ وَلأُمَنِّيَنَّهُمْ وَلآمُرَنَّهُمْ فَلَيُبَتِّكُنَّ آذَانَ الأَنْعَامِ وَلآمُرَنَّهُمْ فَلَيُغَيِّرُنَّ خَلْقَ اللّهِ وَمَن يَتَّخِذِ الشَّيْطَانَ وَلِيًّا مِّن دُونِ اللّهِ فَقَدْ خَسِرَ خُسْرَانًا مُّبِينًا ))(( يَعِدُهُمْ وَيُمَنِّيهِمْ وَمَا يَعِدُهُمُ الشَّيْطَانُ إِلاَّ غُرُورًا)) (( أُوْلَئِكَ مَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ وَلاَ يَجِدُونَ عَنْهَا مَحِيصًا))

((Allaah Amemlaani. Naye Shatwaan alisema: Kwa yakini nitawachukua sehemu maalumu katika waja wako)) ((Na hakika nitawapoteza na nitawatia matamanio, na nitawaamrisha, basi watakata masikio ya wanyama, na nitawaamrisha, basi watabadili Aliyoumba Allaah. Na mwenye kumfanya Shaytwaan kuwa ni mlinzi wake badala ya Allaah, basi huyo amekhasiri khasara ya dhaahiri)) ((Anawaahidi na anawatia tamaa. Na Shaytwaan hawaahidi ila udanganyifu)) ((Hao makao yao ni Jahannamu, na wala hawapati makimbilio kutoka humo)) [An-Nisaa: 117 - 121  

Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ametupasha habari kuwa Allaah Amemlaani mwanamme mwenye kujifananisha na mwanamke na kinyume chake.

 

Hata hivyo, Ibadah yake ya Swalah ni sahihi na makosa yake ya kutoboa sikio atapata. Na ni madhambi kama haya ambayo yatamfanya Muislamu siku ya Qiyaama awe ni mwenye kuhasirika na kuwa aliyefilisika kama alivyotuarifu Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Kwa hiyo, ni vyema sana kwako uweze kuzungumza na kijana huyo na kumuelimisha kuhusu hilo kosa ili aweze kufanya toba na kurudi kwa Allaah Aliyetukuka.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share