Jina La Swahabiyyah Aliyemhifadhi Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Katika Vita Vya Uhud

 

SWALI:

Naomba unambie  jina la mwanamke aliyemkingina Bw. Mtume na kunfunika wakati kashabigwa na kutulewa meno yake ya mbele baadae wakataka kumpiga mishale na huyo mwanamke akamlalia Bw. Mtume na mishale hiyo ikampiga yeye mgogoni na kufa. Naomba jina la mwanamke huyo. Shukrani,

 


 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani ndugu yetu kwa swali lako hili kuhusu tukio miongoni mwa matukio mengi ya bwana Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).

Tukio hili ni lile la Vita vya Uhud vilivyopiganwa mwaka wa 3H/ Januari 625M. Hakika ni kuwa Swahabiyah huyu hakufariki kama ulivyotaja bali aliishi na kuaga dunia baada ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kufariki. Huyu Swahabiyah alikuwa anaitwa Umm ‘Ammaarah Nuswaybah bint Ka‘ab al-Maazaniyah (Radhiya Allaahu ‘anha). Yeye alibashiriwa Pepo na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na ni miongoni mwa wanawake wawili wa ki-Answaari waliohudhuriya Bay‘ah ya ‘Aqabah ya pili.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share