Ikiwa Hana Ushahidi Kuwa Ni Bidhaa Za Mayahudi, Anaweza Kununua?

SWALI:

 

Assalaam Aleykum Warahmatullah Wabarakatu, kuna bidhaa kama coca cola, mafuta ya baby care, jonson baby, na vyakula mbalimbali ambavyo inasemekana hutengenezwa na waisreali. Je kutumia vitu hivi haifai? Na je kama bidhaa hizihizi zinatengeneza nchi nyingine (si israeli) pia haifai? Tukumbuke kuwa haifai kuhukumu kitu kama hatuna uhakika: je nitahukumuwa vipi ikiwa nitatumia bidhaa hizo kwa kuwa sina ushahidi kama zinatengenezwa na Waisraeli. Natumai nitapata jibu lililofasaha kwani swala hili linatutatiza sana jamii ya Kiislaam. Natanguliza Shukrani. Wahadha Assalaam Aleykum.


 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kususa bidhaa za Mayahudi na wanaowasaidia.

 

Hakika ni kuwa suala hili halina utata kabisa, utata unakuja tu kwa kuwa sisi tumezoea bidhaa hizo kwa kiasi ambacho kuacha imekuwa ni mtihani kwetu. Kwa ajili hiyo tunajipatia udhuru mmoja na mwingine ili kuendelea kutumia bidhaa hizo.

 

Kanuni ya Uislamu iko wazi, kuwa tunatakiwa kushirikiana katika wema na ucha Mungu na kutoshirikiana katika uadui.

Allaah Aliyetukuka Anasema:

Na saidianeni katika wema na ucha Mungu. Wala msisaidiane katika dhambi na uadui. Na mcheni Allaah. Hakika Allaah ni Mkali wa kuadhibu” (al-Maa’idah [5]: 2).

Na ‘Aliy bin Abi Twaalib (Radhiya Allaahu ‘anhu) naye akasema: “Mwanaadamu ana maadui wa tatu: Adui yake, adui wa rafiki yake na rafiki wa adui yake”. Hawa ni maadui watatu ambao tunafaa tujihadhari nao sana kwani wao humkoroga na kumvunja adui yao pamoja na rafiki wa adui yao.

Kwa yaliyo juu ni dhahiri kuwa Waislamu wana wajibu mkubwa wa kuwasaidia ndugu zao Waislamu sehemu zote za ulimwenguni kwani wao kwa wao ni ndugu. Na kwa minajili hii, kushirikiana na kumfaidisha adui ili kumuua Muislamu ni jambo ambalo halifai kabisa. Ni madhambi makubwa zaidi kusaidia kumuua Muislamu kwa njia yoyote ile. Ndio Mtume (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) akasema:

 

Mnusuru nduguyo akiwa amedhulumu au amedhulumiwa”. Akaulizwa: “Yule aliyedhulumiwa tunafahamu lakini huyu aliyedhulumu tusamsaidiaje?” Akasema: “Muepusheni na dhuluma kwani kufanya hivyo ni kumnusuru” (al-Bukhaariy).

 

Kuwanusuru na kuwasaidia ndugu zetu ni kutumia njia nyingi kama:

1.     Kuwasaidia katika Jihaad yenyewe.

2.     Kuwasidia kifedha ili waweze kujinasua na kujihifadhi kwa kuwa na silaha za kuweza kupambana na adui.

3.     Kususia bidhaa za wenye kumsaidia adui na hii inakuwa ni wajibu wa kila Muislamu.

4.     Kuwaombea du’aa kila wakati ili Allaah Aliyetukuka Awasaidie, kwani du’aa ni ‘Ibaadah.

 

Kwa kuwa kutumia vitu hivyo itakuwa ni kumsaidia adui ili kuwaua Waislamu, hivyo matumizi ya bidhaa hizo itakuwa haifai. Bidhaa za Israili huwa kawaida zinatengenezwa katika nchi na idhini yao wenyewe, kwani wao wana haki hiyo kimataifa. Kwa ajili hiyo faida yote inarudi kwao, mfano ni Coca cola ambayo ina matawi katika kila nchi lakini unga wa kutengeneza kinywaji hicho unatoka Atlanta, Marekani na faida ndio inarudi huko. Kwa hiyo, utumiaji wa bidhaa hiyo itakuwa haifai kwani madhara ni yale yale. Ikiwa kweli huna uhakika, basi itakuwa hakuna tatizo kutumia bidhaa hiyo ikiwa ni halali kutumiwa na Muislamu lakini ikiwa una hakika inabidi kwa Uislamu wako uepukane na manunuzi yake na matumizi yake.

 

Yale yanayosemwa ni mambo ya hakika si mambo ya eti eti. Ushahidi ni ule unaotoka kwa mwenzio ambaye ni Muislamu na wala hana sababu ya kukudanganya. Na wao wenyewe lau ingekuwa si kweli wangejitetea kwa kuandika makala na kuyasambaza kama walivyoandika katika tovuti yao kuwa si kweli kuwa hati za Coca cola zinawakilisha maneno haya: La Muhammad, La Makkah. Na hili nalo kuwa kama hawasaidii Israili wangelikuwa wameliweka wazi kabisa. Kunyamaza kwao ni kuyakinisha ukweli wao. Na haiwezekani kuwa Waislamu wote wanaosema ni waongo mkweli ni mimi mwenye shaka ya hilo. Na zipo dalili kuwa wamekuwa wakiisaidia dola haramu ya Israili kwa miaka thelathini sasa.

 

Kisha Coca cola ina tatizo kuwa si kinywaji cha siha bali kina madhara makubwa katika mwili wa mwanaadamu jambo lililofanya bunge la India kuipiga marufuku uuzaji wake katika hoteli ya bunge lao. Hata hivyo, kwa vikwazo walivyowekewa na Marekani ilibidi wairuhusu kuuzwa tena katika eneo hilo.

Kadhalika vinywaji vyote vinavyotengenezwa na kampuni hiyo kama vile fanta, sprite n.k. vinaingia katika kususiwa huko.

Pia Pepsi na wenzake kama Mirinda, Seven Up na zinginezo, zote hizo ni katika makampuni yanayohusiana na dola haramu la Israel.

Na pia kununua bidhaa katika maduka yao makubwa ya vyakula kama Sainsbury na yale maduka ya nguo kama Marks and Spencer, Debenham n.k. ni kuwasaidia Mayahudi wka njia moja au nyingine. Maduka hayo kila mwaka yanatangaza kutoa faida zake asilimia si chini ya 20 kuisaidia dola hilo dhalimu la kizayuni.

 

Pia fatwa ya 1984 ya Majlis Ulamaa ya Afrika Kusini imeyakinisha kuwa vodka inatumika katika utengenezaji wa kinywaji hicho pamoja na dalili zao.

 

Tunakuwekea chini list ya bidhaa tulizojaaliwa kukusanya ambazo ima ni za Mayahudi moja kwa moja, au wana ushirikiano, hisa n.k.

 

 

MAKAMPUNI NA BIDHAA ZA MAYAHUDI ZA KUSUSIWA

 

 

 

 

AOL Time Warner

 

Apax Partners & Co Ltd

Coca-Cola

 

Danone

Delta Galil

 

Disney

Estée Lauder

 

IBM

Johnson & Johnson

 

Kimberly-Clark

Lewis Trust Group Ltd

 

L'Oreal

Marks & Spencer

 

Nestle

News Corporation

 

Nokia

Revlon

 

Sara Lee

Selfridges

 

The Limited Inc

Home Depot

 

Intel

Starbucks

 

Timberland

McDonald's

 

Arsenal FC

 

Tunamuomba Allaah Aliyetukuka Atufanikishie mambo yetu ya kuweza kuwasaidia ndugu zetu kwa njia zote ikiwemo kususia bidhaa za Israili na washirika wake.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share