Sambusa Za Nyama 2

Sambusa Za Nyama 2

Vipimo

kiasi ya sambusa 45

Manda za sambusa za tayari (spring rolls) - 1 pakiti

Nyama ya kusaga - 2lb

Kitunguu saumu (thomu/galic) - 6/7 habba

Tangawizi - kipande cha kiasi 

Nyanya - 1

Pilipili mbichi - Unavyopenda

Chumvi - kiasi

*Bizari ya sambusa - 2 vijiko vya chai

Vidonge vya supu ( magi cubes) - 2

Ndimu - 1

Vitungu maji vilivyokatwa - 3

Kotmiri ilyokatwa katwa - ½ Kikombe        

Mafuta ya kukaangia - kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Saga nyanya, thomu, tangawizi na pilipili mbichi  pamoja kwenye blender.
  2. Tia nyama kwenye sufuria pamoja na mchanganyiko wa nyanya uliyosaga, bizari, chumvi na vidonge vya supu, kisha uipike kwa moto wa kiasi mpaka ikauke. Halafu kamulia ndimu na uache motoni tena kidogo, kisha utaepua uiwache ipowe.
  3. Ikisha powa kabisa utatia vitungu na kotmiri utachanganya vizuri na tayari kufungwa.
  4. Halafu utazikaanga na mafuta yakiwa moto kiasi mpaka zibadilike rangi na kuiva, kisha weka kwenye chujio au sahani yenye karatasi za jikoni iliuchuje mafuta yakuzidi na itakuwa tayari kwa kuliwa.

Vipimo Vya Masala Ya Sambusa

Pilipili manga - 3 vijiko chai

Bizari ya pilau (cumin) - 2 vijiko chai

Mdalasini nzima - 4 Vijiti

Karafuu - 2 vijiko chai

Iliki - kiasi

Namna Ya Kutayarisha

Utasaga vipimo vyote, (ukipenda unaongezea pilipili nyekundu kavu) katika mashine ya kusagia na itakuwa tayari kutumia kwenye vipimo vya sambusa.

Kidokezo:

Unaweza kusaga zaidi ukaweka kwenye chupa na kutumia wakati mwengine.

 

 

 

Share