Chops Za Viazi Kwa Nyama Ngombe (Beef Potato Chops)

Chops Za Viazi Kwa Nyama Ngombe (Beef Potato Chops)

Vipimo

Viazi - 1 kilo na nusu takriban

Chenga za mkate (breadcrumbs) - 2 vikombe

Mayai - 3

Mafuta ya kukaangia - kiasi ya karai kujaa nusu

Vipimo Vya Mjazo wa Nyama

Nyama ya kusaga ya ngombe - ½ kilo

Vitunguu vilokatwakatwa - 2  

Tangawizi mbichi ilosagwa - 1 kijiko cha supu

Thomu (saumu/garlic) ilosagwa - 1 kijiko cha supu

Bizari ya mchanganyiko - 2 vijiko vya chai

Pilipili mbichi ilosagwa - 2

Ndimu -  2 kamua

Chumvi - kisia

Kotmiri ilokatwakatwa - nyingi kiasi

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Chemsha viazi kisha, menya maganda, uweke katika bakuli kubwa kisha upondeponde.
  2. Weka nyama katika sufuria na viungo vyote isipokuwa kotmiri na vitunguu.
  3. Tia ndimu, ikaushe kwenye moto ichanganyike vizuri na viungo.
  4. Ukipenda kolezea zaidi kwa pilipili.
  5. Zima moto, changanya vitunguu na kotimiri.
  6. Fanya duara la viazi kisha weka kijiko kimoja cha chai mjazo wa nyama.

 

 

     7. Teka tena viazi kidogo ufunikie, kisha banabana ufunike nyama ndani ya kiazi huku unafanya round na kulibatabata chop. Ikiwa limechukua viazi vingi pembeni, punguza viazi kidogo kidogo bila ya kutokeza mjazo.

      8. Piga mayai katika kibakuli, chova chops kisha garagaza katika chenga za tosti (breadcrumbs) kisha choma katika mafuta ya moto (deep fry).

      9. Epua zinapogeuka rangi ya hudhurungi au brown. Weka katika chujio zichuje mafuta kisha panga katika sahani zikiwa tayari.

Kidokezo:

Ukipenda tolea kwa chatine ya nazi. Au tolea kwa sosi ya ukwaju na chatine mtindi inapatikana hapa

Sosi Ya Ukwaju

Chatine Ya Mtindi Na Nanaa

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

 

 

 

Share