Mama Mkubwa Kaacha Watoto Na Wajukuu

 

SWALI:

 

Asalaam alaykum, kwanza ninamshukuru ALLAH SUBHANNA WATAALLA na ninamtakia neem kipenzi chetu Mtume MUHAMMAD SWALAALLAH ALAYHI WASSALAAM. Suala langu ninatatizo kuhusu mirathi hii nina Mama yangu mkubwa alijaaliwa kuzaa mtoto mmoja wa kike, na huyo dada yangu akajaaliwa kupata watoto 3, bahati nzuri Allah Subhanna Wataala akamfisha huyo dada yangu baada kama ya wiki pia mama mkubwa akafariki, kwa mama mkubwa aliaacha nyumba moja je hawa wajukuu wana haki ya kurithi hiyo nyumba, Mama mkubwa ameacha Mume, ndugu wa kwa baba na mama, na hao wajukuu je mirathi yao itakuwaje mgawanyo wao, Wabillah Taafiq


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu mgao wa mirathi wa aliyefariki mama mkubwa. Ama kuhusu mgao ambao kila mmoja atapata kishari’ah ni kama ifuatavyo:

 

1.     Mume wa aliyefariki atapata nusu (1/2) ya mali.

2.     Ndugu wa aliyefariki kwa mama na baba watapata mali iliyobaki (yaani ½). Mgao wao utakuwa mwanamme atapata sehemu mbili kwa sehemu moja ya mwanamke.

3.     Ama wajukuu wa binti za aliyefariki hawatopata chochote.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share