Maana Ya Jina La Asmaa

SWALI:

 

ASSALAM ALEYQUM WARAHMATULLAH,


KWANZA NAWAOMBEA KILA LA KHERI KUTOKA KWA ALLAH KWA DAAWA TUNAYO PATA KUTOKA KWENU. PILI NAOMBA MNISAIDIE KUJUA MAANA YA NENO/JINA ASMAH!!! NATUMAI MAJIBU MAZURI NA YA KURIDHISHA YATAKAYO NIFARIJI KUTOKA KWENU.


WASSALAM.

 


 

 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu maana ya jina Asmaa’.

Asmaa’ awali ya yote alikuwa ni Swahaabiyah (Swahaba wa kike) aliyesilimu pamoja na baba yake ambaye ni Abu Bakr Asw-Swiddiyq (Radhiya Allaahu ‘anhuma). Na wote binti na baba walibashiriwa kuingia Peponi na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Pia kuna Swahaabiyah mwengine aliyekuwa ni mwakilishi wa wanawake wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) mwenye jina Asmaa’ bint Yaziyd (Radhiya Allaahu ‘anha).

 

Ama maana ya jina hilo ni; tukufu, adhimu, maarufu, aali au bora sana, thamani, pia maana yake nyingine ni wingi wa jina ‘ismu’ (na ‘asmaa’ ni majina) na kadhalika.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share