Ndugu Amefariki Ameacha Mama, Watoto 3 wa Kike Na 1 Wa Kiume Na Kuna Hisa Ya Mali Yake

 

SWALI:

 

Asalam aleikum

 

Niko na swali ambalo laleta vita katika familia na ni habari ya urathi nina ndugu ambaye amefariki na amwecha watoto wane - watatu wa kike na moja wa kiume, na mimi katika hio mali nina share pia  na amwecha  mama, ndugu wa kiume  tatu na dada  moja  sasa hii mali itagawanywa vipi. Naomba msaada katika haya maswala.

 

 


 

 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu urithi wa ndugu aliyeaga dunia.

 

Awali ya yote ni kuwa kabla ya mgao kufanywa inatakiwa ijulikane hisa ya aliyefariki. Wewe kama ndugu ambaye mlikuwa mnashirikiana naye katika mali inataka mwanzo utoe mali yako ijulikane yake ni ngapi bila ya kudhulumu hata chembe.

 

Baada ya kujulikana hisa yake, sasa ndio mnaweza kuigawa. Maadamu aliyefariki ana watoto, ndugu zake wa kiume na wa kike hawatorithi chochote. Kulingana na swali pia inaonyesha aliyefariki kaka yako hakuacha mke wala baba kabisa. Ima alikuwa na mke akamuacha au ameaga dunia kabla yake ilhali baba yake mzazi inaonyesha naye ameaga. Ikiwa wapo hai itabidi mtueleze mnapopata jibu kwa swali lako hili. Ikiwa ni hivyo mgao wao utakuwa kama ifuatavyo:

 

1.     Mama atapata sudusi ya mali ya mtoto wake (1/6 au 16.7%).

2.     Mtoto wa kiume atapata thuluthi (1/3 au 33.3%).

3.     Ilhali watoto watatu wa kike watagawa nusu ya hiyo mali. Hivyo, kila mmoja atapata sudusi (1/6 au 16.7).

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share