Marehemu Ameacha Kaka, Dada Na Mjukuu
SWALI:
Marehemu amewachja kaka mmoja wa mama mmoja, kaka mmoja wa baba mmoja, madada wawili wa mama mmoja na mjukuu kwa mtoto wake wa kiume {aliyefariki kabla}. Ahsante.
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ahli zake, Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka siku ya mwisho.
Hakika swali hili haliko moja kwa moja kwani kuna mengi ambayo hayakuelezwa lakini ikiwa muulizaji ana hakika hao ndio warithi au jamaa wa karibu kabisa kwa marehemu basi watarithi
1) Mjukuu akiwa ni wa kiume atapata wirathi wote na hao wengine, kaka wa kwa mama, madada wa kwa mama na kaka wa kwa baba hawatapa chochote.
2) Ikiwa mjukuu ni msichana basi atapata nusu (1/2) ya wirathi, kaka wa kwa mama na madada wa kwa mama hawatapata chochote na kilichobaki yaani nusu (1/2) atapewa kaka wa kwa baba.
Lau huyu marehemu alikuwa na mzazi au wazazi walio hai na pia alikuwa na mke au mume mgawo wa wirathi utabadilika.
Tanbihi kwa wenye kuuliza Maswali ya Mirathi:
1. Kijana mwanamume.
2. Kijana mwanaume wa kijana mwanaume (mjukuu).
3. Baba.
4. Babu wa kwa baba.
5. Ndugu mume wa kwa baba na mama (khalisa).
6. Ndugu wa kwa baba.
7. Ndugu mume wa kwa mama.
8. Kijana mwanaume wa ndugu mume khalisa.
9. Kijana mwanaume wa ndugu mume wa kwa baba.
10. Ami wa kwa baba na mama.
11. Ami wa kwa baba.
12. Kijana mwanaume wa ami wa kwa baba na mama.
13. Kijana mwanaume wa ami wa kwa baba.
14. Mume.
15. Binti.
16. Binti wa kijana mwanaume.
17. Mama.
18. Dada khalisa.
19. Dada wa kwa baba.
20. Dada wa kwa mama.
21. Bibi mzaa baba.
22. Bibi mzaa mama.
23. Mke.
Hii itatusaidia sana katika kujibu maswali yenu ya mirathi. Shukran.
Na Allaah Anajua zaidi.
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha



baba amewaacha watoto wake
baba amewaacha watoto wake wanane wanawake wanne na wanume wanne kwa wake wawili.na mali,pesa alizoziwacha zinatumiwa na ndugu zake jee tufanyee nini wafahamu haya?