Kila Kitu Kinamsujudia Allaah سبحانه وتعالى, Je,Wewe Mwanaadam?
Anasema Allaah سبحانه وتعالى
((أَوَ لَمْ يَرَوْاْ إِلَى مَا خَلَقَ اللّهُ مِن شَيْءٍ يَتَفَيَّأُ ظِلاَلُهُ عَنِ الْيَمِينِ وَالْشَّمَآئِلِ سُجَّدًا لِلّهِ وَهُمْ دَاخِرُونَ)) (( وَلِلّهِ يَسْجُدُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الأَرْضِ مِن دَآبَّةٍ وَالْمَلآئِكَةُ وَهُمْ لاَ يَسْتَكْبِرُونَ)) ((يَخَافُونَ رَبَّهُم مِّن فَوْقِهِمْ وَيَفْعَلُونَ مَا يُؤْمَرُونَ))
((Je! Hawavioni vitu Alivyoviumba Allaah, - vivuli vyao vinaelekea kushotoni na kuliani, kumsujudia Allaah na vikinyenyekea?
Allaah سبحانه وتعالى Anatuambia kuwa Yeye Pekee, Asiyekuwa na mshirika wala msaidizi Ndiye Apasaye kuabudiwa. Vitu vyote vinamsujudia wakati wote vikitaka visitake:
((وَلِلّهِ يَسْجُدُ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالأَرْضِ طَوْعًا وَكَرْهًا وَظِلالُهُم بِالْغُدُوِّ وَالآصَالِ))
((Na viliomo mbinguni na katika ardhi vinamsujudia Allaah tu vikitaka visitake. Na pia vivuli vyao asubuhi na jioni)) [Ar-Ra'd: 15]
Na katika Hadiyth ifuatayo,
عن أبي ذر، رضي الله عنه، قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: ((أتدري أين تذهب هذه الشمس؟)). قلت: الله ورسوله أعلم. قال: ((فإنها تذهب فتسجد تحت العرش، ثم تستأمر فيوشك أن يقال لها: ارجعي من حيث جئت)) مسلم
Imetoka kwa Abu Dharr رضي الله عنه kwamba Mtume صلى الله عليه وآله وسلم amesema: ((Unajua jua hili linakwenda wapi?)) Nikasema: "Allaah na Mjumbe Wake Wanajua". Akasem: ((Linakwenda na kusujudu chini ya 'Arsh, kisha linasubiri amri. Na karibuni litaambiwa: Rudi ulikotoka)) [Muslim]
Na Ibn 'Abbas رضي الله عنهما amesema: "Mtu moja alikuja na kusema: "Ewe Mjumbe wa Allaah, nilijiona katika ndoto jana usiku nikiswali nyuma ya mti. Niliposujudu na mti ukawa unasujudu. Kisha nikausikia unasema: ((Ee ِAllaah, Niandikie kwako kwa sijda hii malipo, na Nifutie kwayo madhambi, na Ijaalie kwangu mbele yako ni akiba, na Nikubalie kama ulivyomkubalia mja wako Daawuud)) Ibn 'Abbaas akasema: "Mjumbe wa Allaah صلى الله عليه وآله وسلم akasoma Aayah inayotaja kusujudu kisha akasujudu na nikamsikia akisema maneno hayo hayo aliyosimulia mtu yaliyotajwa na mti" [At-Tirmidhiy, Ibn Maajah, Ibn Hibbaan katika sahiyh yake]
Na ndio maana Allaah سبحانه وتعالى Anasema:
((أَلَمْ تَرَ أَنَّ اللَّهَ يَسْجُدُ لَهُ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَمَن فِي الْأَرْضِ وَالشَّمْسُ وَالْقَمَرُ وَالنُّجُومُ وَالْجِبَالُ وَالشَّجَرُ وَالدَّوَابُّ وَكَثِيرٌ مِّنَ النَّاسِ وَكَثِيرٌ حَقَّ عَلَيْهِ الْعَذَاب))
((Je! Huoni kwamba vinamsujudia Allaah viliomo mbinguni na viliomo katika ardhi, na jua, na mwezi, na nyota, na milima, na miti, na wanyama, na wengi miongoni mwa watu. Na wengi imewastahiki adhabu)) [Al-Hajj: 18]
Aayah hiyo mwisho inasema kuwa ((Na wengi imewastahiki adhabu)) kwa maana kwamba wale ambao hawataki kusujudu [Ibnu Kathiyr 6:540].
Basi ndugu Muislamu tunatumai kuwa hutokuwa miongoni mwa wanaostahiki adhabu. Hivyo timiza Swalah zako tano za fardhi zipasavyo kuswaliwa kwa kuzidumisha na kuziswali kwa wakati wake. Kisha utakapokuwa umezidumisha Swalah zako tano basi jiongozee kuswali Swalah za Sunnah uzidi kumnyenyekea Mola wako na kupata fadhila nyingi za kusujudu na za kuswali Swalah za Sunnah. Na pia kila unaposoma Aayah iliyo na Sajdah, pinduka umsujudie Mola wako Mtukufu.
************
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha



Assalam aleykum, ndugu zangu
Assalam aleykum, ndugu zangu natoa hongera nyingi mno kwa kazi hii iliyojaa vitu muhimu sana kwa dini yetu. Naomba mtuwekee link ya INVITE FELLOW MUSLIMS ili tuweze kuwafahamisha ndugu zetu waislamu wasioujua huu mtandao, Wallahi hii website ni ya manufaa makubwa.
Allah awazidishie na pia site hii iwe chachu ya mabadiliko yetu inshallah.
Wa 'alaykumus-salaam wa
Wa 'alaykumus-salaam wa RahmatuLLaahi wa Barakaatuh
Tunashukuru kujua kuwa mnafaidika na mafunzo haya.
Kuhusu ombi lako Inshaa-Allaah tutalitimiza hivi karibuni kwa tawfiyq ya Allaah Subhaanahu wa Ta'ala. Du'aa zenu muhimu kwetu Allaah Atufanyie wepesi kutekeleza hizi kazi na Atutakabalie.
Ndugu Zako
AL HIDAAYA