Nini Maana Ya Jina La Thaurat, Rumaytha, Rumaysa, 'Aaswif, 'Aaswim, Nurfan na Nasfar

SWALI:

 

Assalam alaykum,

Nimependa jina la Thaurat lakini silielewi maana yake. Kwaiyo naomba kujua maana ya jina hili. Aidha ningependa kujua kwamba Thaurat na Thauhat ni sawa au yana maana tofauti.

Pia naomba maana ya majina-Rumaitha na Rumaysah, Asif na Asim, Nurfan na Nasfar.

 

Wasaalam alaykum

 


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu maana ya baadhi ya majina. Majina yenyewe ni kama yafuatayo:

 

 

 

Namba

Jina

Jinsiya

Maana

 

1

Thaurah

 

 

Mapinduzi

 

Tharwah

Mvulana/ Msichana

Huenda jina la kwanza likawa ni Tharwat badala ya Thaurat. Hili lina maana ya utajiri.

2

Thauhat

 

Jina hili halipo katika majina ya Kiarabu, huenda akawa amekosea kimaandishi.

3

Rumaythah

Msichana

Jina la zamani la Kiarabu – halina maana yoyote ile.

4

Rumayswaa’

Msichana

Huyu alikuwa Swahabiyah mtukufu aliyebashiriwa pepo na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Alikuwa mama yake Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ‘anhu). Na maana yake ni shada la maua.

5a

Asif

Mvulana

Msamaha

5b

‘Aasif

Mvulana

 

Waziri muweza

6

‘Aaswim

Mvulana

 

Anaye jiepusha na maasi na ‘Asim ni mlinzi.

7

Nurfan

 

Jina hili halipo katika majina ya Kiarabu, huenda akawa amekosea kimaandishi.

8

Nasfar

 

Jina hili halipo katika majina ya Kiarabu, huenda akawa amekosea kimaandishi.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share