Wanandoa Walionyimana Haki ya Unyumba Kwa Miaka Minne Je Wafunge Ndoa Upya?

SWALI:

 

MIMI NINA RAFIKI YANGU ANAISHI HAPA MAREKANI ANATATIZO NA MKE WAKE tatizo lenyewe ni hili hawana muafaka wowote kwa sababu mkewe alijenga nyumba na akanunua plot moja ya kujenga nyumba bila kumshirikisha mumewe ndio imefikia hatua mume kuto kuelewana na mkewe hadi imefikia hatua wananyimana unyumba yaani tendo la ndoa wala hawalali kitanda kimoja, lakini wanalala chumba kimoja kwa muda wa miaka minne. Sasa hivi tumewasuruhisha wamerudisha upendo. Je, watu hawa watafunga ndoa upya ao wanaruhusiwa kukutana kimwili bila kufunga ndoa upya. lakini kwa muda wote huo wa miaka minne wametengana tu bila kupeana taraka. na watuhawa wanahitaji kufuata maamuzi ya quran tukufu ili waweze kuishi. tunahitaji msaada wenu. asalam alaykum

 


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu wanandoa kunyimana unyumba kwa muda wa miaka minne. Hakika ikiwa ulivyosema ni hivyo kuwa mume hakutoa talaka japokuwa kulikuwa hakuna haki ya unyumba hao wawili ni mume na mke na hakuna ndoa mpya baina yao.

 

Jambo ambalo tunakushauri ni kuwa hawa wanandoa ni muhimu kwenda katika Msikiti au centre ya Kiislamu iliyo karibu wakapata ushauri nasaha wa karibu ili kila mmoja kati yao ajue haki na wajibu wake katika ndoa. Ikiwa hawatafanya hivyo basi huenda tatizo hilo likaibuka tena na wakati huo litakuwa baya zaidi.

 

Na Allaah Anajua zaidi.

 

 

Share