Maana Ya Twahaarah

 

 

Maana ya Twaaharah

 

Alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Twahara ni nini? Na inakuaje?

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Twahaarah kwa neno la usahali lenye kufahamika ina maana ya usafi. Hata hivyo, kishariy’ah ina maana zaidi ya usafi kwani katika Uislamu kitu au mtu anaweza kuwasafi lakini si twaaharah.

 

 

Kwa hiyo kishariy’ah kuwa na twahaarah ni ile hali ya kwamba mtu hana najisi na yuko safi kutekeleza ‘ibaadah kama ya Swalaah na nyinginezo zinazohitajia mtu kuwa twahaarah.

 

Kwa faidi ziyada bonyeza kiungo kifuatacho: 

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Mlango Wa Twaharaah

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share