Ubikira wa Msichana wa Miaka Saba Akilala na Mwanamme

SWALI:

 

Assalam alaikum ww! mimi nilitumba na rafiki yanyu kumuuliziya swali hili: kama mtoto wakike angaliki na mwyaka mi saba kuteremka aka lala na mwanaume uyo ni bikra ao si bikra?


 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu ubikira wa msichana wa miaka saba akilala na mwanamme.

Hakika ni kuwa suala la kulala na mtu lina utata lakini tutaziangazia maana mbili ambazo zinaweza kujitokeza:

 

1.     Ikiwa mwanamme huyo atalala tu na msichana huyo wa miaka saba bila kufanya kitendo cha ndoa ubikira wake utabakia. Hivyo, msichana huyo atakuwa ni bikra. Hata hivyo ni makosa makubwa mno wa mwanamme kulala na msichana kitanda kimoja kishari’ah hata kama hawatofanya lolote.

 

2.     Ikiwa mwanamme huyo atajimai na msichana huyo, ubikira wa msichana huyo utakuwa umeondoka. Mara nyingi ikiwa ni hivyo inakuwa mwanamme ndiye aliyelazimisha kitendo hicho kwa hivyo yeye atapata madhambi ya zinaa na atakuwa amemdhulumu sana mtoto huyo kumuingilia kwani matokeo yake ni mabaya mno.

 

Bonyeza kiungo kifautacho upate maelezo zaidi

 

Mwanaume Kamuingilia Kwa Nguvu Hadi Ametokwa Damu, Je, Amevunja Bikra?

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share