Mut'a Na Yanayo Husiana Nayo
Nilikuwa nataka kuweka anuani ya sehemu hii kua ni{MWANAMKE KATIKA USHIA}lakini nikaibadilisha anuani hiyo kwa sababu nimeona mapokezi yote yanayopatikana katika vitabu vyetu yananasibishwa(yanaegemezwa) kwa mtume(Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na kwa Amiril muiminina na kwa Abii abdillah(‘Alayhi sallam) na wengineo miungoni mwawanazuoni.
Na mimi sikutaka wana zuoni hao wapatwe na lawama za aina yeyote ile kwani katika riwaya hizo kuna maneno machafu ambayo mtu yeyote hawezi kuyaridhia katika nafsi yake, vipi mtu atayaridhia maneno hayo kwa mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) au atawezaje kuyaridhia kwa Ali wa mtume au kwa maimamu watukufu (amani ya mungu iwashukie)
Hakika mut’a imetumika vibaya sana na mwanamke amedhalilishwa (kwa sababu ya dhana ya uhalali wa mut’a) udhalilishaji mbaya sana,watu wengi wakawa wanakidhi matamanio yao ya kimwili chini ya pazia ya mut’a,na kutumia jina la dini,wakilitumia neno lake Mwenyezi mungu lisemalo: {....فما استمتعتم به منهن فآتوهن أجورهن فريضة....}{mtakapostarehe nao baada ya kufunga nao ndowa basi wapeni mahari yao kwani ni lazima kuwapa.{Annisaai 24.
zimepokewa riwaya nyingi kutoka kwa mashia zinahimiza mut’a mpaka wakafikia kuweka thawabu kwa mwenye kufanya mut’a na madhambi kwa mwenye kuacha mut’a,na inazingatiwa kila asiefanya si muislamu(kwa mtazamo wamashia)
Soma pamoja namimi ushahidi huu:
1-Amesema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):{Atakae starehe(kufanya mut’a) na mwanamke muumin atakua sawa na aliyezuru Al-kaaba mara sabini} inawezekanaje mtu alie strehe na mwnamke awe ni
2-Amepokea Asuduq kutoka kwa Asadiq amesema{Hakika mut’a ni dini yangu na dini ya baba zangu atakaeifanya (mut’a)atakuwa amefanya hivyo kwa kufuata dini yetu na atakae pinga(mut’a)atakuwa ameipinga dini yetu na atakuwa na imani tofauti na imani yetu,}MANLA YAHDHURUHU AL-FAQIYH 3/366 , na huku ni kumkufurisha yule asiye kubali mut’a.
3-Aliulizwa Abu Abdillah(‘Alayhi sallam) je mwenye kufanya mut’a anapata thawabu?akasema:{ikiwa anafanya hivyo kwa kutaka kupata radhi za Mwenyezi Mungu basi kila neno atakalomsemesha (huyo mwanamke aliyefanya nae mut’a) Mwenyezi Mungu atamuandikia jema moja, atamkaribia, mwenyezi mungu atamsamehe dhambi moja, na atakapooga husamehewa madhambi kiasi cha maji yaliyopita katika nywele zake}MANLA YAHDHURUHUL AL-FAQIYH 3/366.
4-Na amesema Mtume(Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):{atakaejistarehesha(kufanya mut’a) mara moja atsalimika na hasira za Mwenyezi Mungu, na atakae fanya(mut’a) mara mbili atafufuliwa pamoja na watu wema, na atakae fanya(mut’a) mara tatu atakua pamoja nami peponi}MANLA YAHDHURUHUL AL-FAQIYH 3/366.
ninasema: kwa ajili ya kupata thawabu hizi (za mut’a) walimu wote wa hapa chuoni na viongozi pamoja na wanawake wazuri waliopo hapa chuoni wote wanafaya mut’a kwa wingi sana,na nakusudia kutaja miongoni mwao bwana ALSADRU-NA AL-BAROO JARDY-NA ASHIRAZY-NA ALQAZ’WAYN, NA ALTABTABAI,NA ASSAYID AL MADANIY, bila kumsahau kijana anae nyanyukia , ABDUL HARITH AL-YASIRIYI,na wengineo, hakika hao (waliotajwa) wanafanya mut’a kwa wingi na kila siku kwa hamu yakupata thawabu hizo(zilizo tajwa) na kutaka kua pamoja na mtume peponi .
na amepokea bwana FAT-HULLAHI ALKASHAANIY,katika kitabu : TAFSIR MINHAJI ALSADIQIYNA kutoka kwa Mtume(Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “atakae fanya mut’a mara moja atapata daraja ya Husain(‘Alayhi sallam),na atakae fanya mara mbili atapata daraja ya Hassan(‘Alayhi sallam),na takae fanya mara tatu atapata daraja ya Alli Bin Abii Talib(‘Alayhi sallam),na atakae fanya mara nne atapata daraja yangu”
Tuchukulie mtu mmoja mchafu ataamua kufanya mut’a mara mmoja hivi kweli ataweza kupata kama ya Husain?au akafanya mara mara mbili au tatu au nne ataweza kuwa na daraja (cheo) kama Hassan au Ally au Mtume(Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)?je cheo cha Mtume(Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)na vyeo vya maimamu wetu ni duni kiasi hiki?
Hata kama mtu anaefanya mut’a atakuwa amefikia ngazi ya ya juu katika imani hivi kweli ana weza kufikia cheo cha Hussein au Hassan au Ally au Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)?!
Hakika daraja ya Husein ni ya juu sana hawezi kuifikia mtu hata akiwa imani kiasi gani,pia mtu hawezi kufikia daraja ya Hassan auAlly auMtume hata
Wameiruhusu mut’a mpaka kwa wanawake wa familia ya mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)
Basi ninasema kuwa jamaa zake mtume ni watukufu hawafanani kufanyiwa kitendo kama hicho (mut’a) kwa sababu wao ni kizazi cha mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)na watu wa nyumbani kwake wanawezaje kufanyiwa kitendo kama hivho, na nitawatajia sababu ya hilo inshaa Allah.
amebainisha kulainiyi kuwa mut’a inafaa japo kwa tendo moja la ndoa , kati ya mwanaume na mwanamke,na suala hili limeelezewa katika kitabu FURUL-AL-KAFI 10/460.
Na si lazima mtu utakae fanya nae mut’a awe mkubwa bali inawezekana kufanya mut’a na mtoto wa miaka kumi , na kwa kuthibitisha hili ,amepokea Al-kulainiy katika kitabu AL-FURUI juzuu ya 5
Na hoja zote hizi zitapatiwa majibu Mwenyezi Mungu akipenda,lakini ninasema: yote yaliyo nasibishwa kwa Abii Abdillah yanaonyesha kuruhusu mut’a kwa msichana mwenye miaka kumi,lakini baadhi
Alipokuwa imamu AL KHOMEINIYU akiishi Iraq tulikua tunaenda kwake kupata Elimu mpaka ukawa uhusiano wetu na yeye ni mkubwa sana ,na ilitokea siku moja kukubali mwito wa kuutembelea mji TAL-AFAR,(tal-afar ni mji ulio magharibi mwa mji wa AL-MUUSWAL)kiasi cha mwendo wa saa moja na nusu kwa gari, akaniomba nisafiri nae,nikasafiri nae,wakatupokea na wakatukirimu takrima iliyo kubwa kwa muda tuliokuwa kwenye familiya moja ya kishia yenye kukaa huko na walikubaliana kueneza ushia sehemu hiyo,wanaendelea kuzihifadhi picha za ukumbusho tulizo piga nao nyumbani kwao.
Na ulipo malizika muda wa safari tulirudi,na tulipokua tuna rudi tukipitia Baghdadi alitaka imamu tupumzike kutoka na na uchovu wa safari, akaamrisha tuelekee katika mji wa Al-atafiya anapokaa mtu mmoja mwenye asili ya kiirani aitwae Sayid Swahib ambae alikuwa akifahamiana sana na imamu Khomeiny.
Akafurahi sana Sayid Swahib kwa kuja kwetu,na tulifika kwake wakati wa Adhuhuri,akatuandalia chakula cha fakhari,akawasiliana na jama zake wakahudhuria, na wakajaa katika nyumba ile kwa kutukirimu sisi,na akatutaka Sayid Swahib usiku ule tulale kwake,na akakubali imamu khomeniy hilo,na ilipofika wakati wa isha tuliletewa chakula cha usiku,wakawa walio hudhuria wanaubusu mkono wa imamu,na kumuuliza mas-ala na akiwajibu mas-ala yao, na ulipokaribia wakati wa kulala na waliohudhuria wameshaondoka,isipokua wenye nyumba , imamu KHOMENEI alimuona binti wa umri wa miaka minne au mitano,mzuri sana imamu akamuomba baba yake mtoto (sayd swahib) amlete ili afanye nae mut’a baba yake mtoto akakubali kwa furaha kubwa, basi akalala imamu khomeni na yule msichana akiwa mapajani kwake, huku tukisikia kilio chake na kelele zake!!
Usiku ule ulipita,ilipofika wakati waasubuhi,tulikaa na kunywa chai, akaniangalia imamu khomeniy na akakuta alama ya kulipinga lile jambo waziwazi katika uso wangu,kwasababu vipi atafanya mut’a na mtoto mdogo huyu wakati katika nyumba ile kuna wasichana wakubwa wazuri anaoweza kufanya nao mut’a , kwa nini asifanye nao badala yake afanye na mtoto mdogo ?
Akaniambia : Sayid Husein umesema nini kuhusu kufanya mut’a na mtoto mdogo?nikamwabia : bwana wangu kusema ni kwako, na kitendo chako ndio sahihi , kwa sababu wewe ni imamu mwenye kujitahidi,haiwezekani kwa mtu mfano wangu mimi kuona au kusema isipokua ulivyoona wewe au ulivyosema,(nilisema hivyo kwa sababu wakati huo nisingeweza kupinga chochote)
Akasema : “ sikia Sayid Husein,hakika kufanya mut’a na mtoto mdogo inafaa lakini kwa kucheza nae na kum’busu na kumpitishia dhakari katika mapaja yake, kwa sababu tendo la ndoa haliwezi.
Na alikua Imamu Khomeiny akiona inafaa kufanya mut’a mtoto hata ane nyonya, akisema:{ si vibaya kustarehe na mtoto anae nyonya kwa kumkumbatia na kuichezesha dhakari kati ya mapaja yake na kum’busu} tazama kitabu chake ATAHRIRU_ALWASILA 2/24/MLANGO, NAMBA 12.
Nilikaa katika ofisi ya imamu ALKHUUIY,wakaingia vijana wawili yaonekana kuwa wametufautiana katika mas-ala Fulani waka afikiana kumuuliza imamu AL KHUNIY,ili awafahamishe jawabu, akauliza mmoja wao,unasemaje imamu kuhusu mut’a? je nihalali au ni haramu? Akamuangalia imamu AL KHAUNIY yule kijana huku akiwa amehisi jambo katika swali lake,kisha akamwambia wapi unaishi?akasema yule kijana naishi Al mauswil,lakini sasa hivi niko hapa Annajaaf inapata miezi miwili,imamu akamuuliza yule kijana : je wewe ni Ahlu sunna?akasema kijana ndiyo, imamu akasema: mut’a kwetu sisi(mashia) ni halali lakini kwenu(Ahl-ssunna) ni haramu,yule kijana akasema mimi nipo hapa yapata miezi miwili nikiwa mgeni katika mji huu,basi utaniozesha binti yako ili ni starehe nae mpaka nitapo rudi kwetu? imamu akanyamaza kidogo kisha akamwambia: mimi ni mtukufu na hili jambo ni haramu kwa watukufu,na ni halali kwa mashia wa kawaida
Kijana akamwaangalia Asayid AL KHUUIY huku akitabasamu na mtazamo wake unaonyesha kuwa kijana kafahamu kwamba imamu AL khuuiy ametumia taqiya kisha wakasimama na kuondoka, nikamtaka rukhsa imamu AL khuuiy ya kutoka, nikakutana na wale vijana wawili,nikaelewa kuwa mwenye kuuliza ni Ahlu sunna na mwenzake ni shia wametofautiana juu ya mut’a je ni halali au haramu? Wakaafikiana juu ya kuuliza marejeo ya dini ya AL imamu AL khuuiy,nilipo wazungumzisha vijana wawili hao, yule wa kishia alipandisha hasira na kusema :Enyi watu waovu,mnaruhusu kustarehe na wasichana wetu ,na mnatueleza kua ni halali na inawakurubisha,kwa Mwenyezi Mungu na mnatuharamisha kustarehe na mabinti zenu? yule kijana akaondoka na huku akitukana na kushutumu na akiapa kuingia katika madhehebu ya Ahlu sunna,nikawa namtuliza yule kijana na kumuapia kwa mungu kuwa mut’a ni haramu na nikampa ushahidi wa hilo.
Hakika mut’a ilikua inafaa zama za ujinga, uislamu ulipo kuja uliibakisha mut’a kwa muda,kisha ikaharamishwa katika vita vya Khaibara,lakini lililozoeleka kwa mashia na wasomi wao ni kwamba Omar bin Khatab ndie aliye iharamisha, na haya ndiyo yaliyoelezwa na baadhi ya wanazuoni wetu.
Na ukweli ni kwamba mut’a iliharimishwa katika vita vya khaibar.
Amesema Amirul Muuminin (‘Alayhi sallam) {aliharamisha mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) siku ya khaibar kula nyama ya punda wakufugwa na ndoa ya mut’a} tazama (ATTAHDHB 2/186)(AL-ISTIBAR 3/142),(WASAILU
Na akaulizwa Abuu Abdillah (‘Alayhi sallam):{Je walikuwa waislamu katika zama za mtume(Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wakiona bila ya kutangaza? Akasema:hapana}(tazama ATTAHDYB 2/189).
Amesema tausi akifafanua maneno hayo; hakika Abu abdillahi hakukusudia kwa maneno yake hayo ndoa ya kudumu isipokuwa alikusudia mut’a ndio maana ameyaleta maelezo haya katika mlango unaohusu mut’a .
Hakuna shaka kwamba hoja mbili hizi ni zenye kuifuta mut’a na kuibatilisha .
Amiril-muuminin (‘Alayhi sallam) ameelezea kuharamishwa mut’a kutoka kwa mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na hii ina maana kuwa Amirul muuminin (‘Alayhi sallam) amesema kwamba mut’a iliharamishwa tokea siku ya khaibara na bila shaka viongozi wengine baada yake walijua hukumu ya mut’a baada ya kuja kwao kuwa imeharamishwa . Na hapa tuko mbele ya habari aina mbili : zilizo pokewa zinazoeleza waziwazi kuhusu uharamu wa mut’a ,Na zile zinazo nasibishwa kwa maimamu zinazo himiza kufanya mut’a, Na hili ni tatizo muislamu anachanganyikiwa afanye mut’a au asifanye?
Usawa ni kuacha mut’a kwasababu ni haramu kama zilivyothibiti habari zake kutoka kwa Amirul muuminin(‘Alayhi sallam) ama maelezo yaliyo nasibishwa kwa maimamu bila shaka si sahihi, bali ni habari za uzushi wamesingiziwa maimamu,(‘Alayhi sallam)kwani hawawezi kwenda kinyume na jambo alilo liharamisha mtume(Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam),na Amiril-muminina akawa na msimamo huohuo baada ya mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ukizingatia wao ndio walio chukua elemu kutoka kwa mababu na mababu kwa sababu wao ni familia moja,
Alipo ulizwa Abuu Abdillah(‘Alayhi sallam):(Je walikuwa waislamu katika zama za mtume(Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wakioa bila ya kutangaza? Akasema:hapana, haikua hivyo)kama asingekua anajua kuwa mut’a ni haramu asingejibu kwa kusema hapana, hasa ukizingatia swali liliulizwa kuhusu mut’a na kwamba Abu jaafar alieipokea habari hii ameika katika mlango wa mut’a kama tulivuo sema.
Na haikuwa inawezekana kwa Abii Abdillah(‘Alayhi sallam) wala maimamu walikuwa kabla yake na baada yake kwenda kinyume na amri ya mtume(Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) au kuuhalalisha jambo aliloharamisha au kuzua jambo lisilo julikana katika zama zake (‘Alayhi sallam).
Kwahayo inakua wazi kuwa habari zilizokuja kuhimiza mut’a si maneno ya maimamu , isipokuwa nimaneno yaliyosemwa na watu kisha wakawasingizia maimamu kwa kutaka kuwatusi AHLIL-BAITI,na kuwakosea adabu , na kama si hivyo itatafsiriwaje kuhalalisha kwao kufanya mut’a na familia ya mtume na kuwaita makafiri wasiofanya mut’a?
Pamoja na kuwa maimamu wote (‘Alayhi sallam) haikupatikana habari sahihi kuwa mmoja wao,aliwahi kufanya mut’a wala kuihalalisha mut’a, je watakua wameishi katika dini isiyo kuwa ya kiislamu?
Likiwa wazi kwetu
Kulainy amepokea kutoka kwa Abii Abdillahi(‘Alayhi sallam) kwamba mwanamke mmoja alikuja kwa Omar ibn Khatab akasema :hakika mimi nimezini akaamrisha kupingwa mawe,akaelezewa Amirul-muumini(‘Alayhi sallam) akamuuliza: vipi umezini? Akasema: nilipita kijijini ikanipata kiu kali sana nikamuomba maji bedui mmoja akakataa isipokua nitakapojitolea nafsi yangu kwake(kukubali kuzini nae), ilipo nizidi kiu, nikahofia kufa akaninywesha maji nami nikamwachia nafsi yangu, akasema Amirul muumini(‘Alayhi sallam) hiyo ni ndoa na apa kwa bwana wa Al kaaba,(AL FURU’U 2/193).
Hakika ya mut’a kama inavyojulikana inakuwa kwa kuridhiana pande mbili na kuwa na hamu baina yao, ama katika upokezi huu mwanamke aliyetajwa alikuwa na shida, mwenye kulazimishwa,akajitolea nafsi yake ili apate kunywa maji, hii haichukuliwi ni zinaa kwa hiyo kulikuwa hakuna haja ya kutaka kutwaharishwa na Omar , zaidi ya hayo -ni muhimu kuzingatia - kuwa Amirul muuminin ndie ambae amepokea uharamu wa mut’a kwa kunakili toka kwa mtume(Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika vita vya Khaibar,vipi atatoa fatwa hapa kuwa hii ni ndoa ya mut’a?! na fatwa yake inaonyesha kuhalalisha kukubali na kuridhika kwa kitendo cha mme na mke?!
Hakika fatwa hii lau angalisema mmoja wa wanafunzi ingehesabiwa kwake ni kosa ambalo anstahiki lawama juu yake basi iweje kosa hili linasibishwe na Amiril-muminin(‘Alayhi sallam)ambae anafahamika ni nani katika elimu na fatwa?
Hakika yule aliyeinasibisha fatwa hii kwa Amirul muuminina ama ni mwenye chuki anayetaka kumtukana , au ni mwenye lengo jengine kwa hiyo akazusha kisa hiki na kukinasbisha kwa Amirul-muminin ili aifanye mut’a iruhusike kisheria ili yeye na wenzake kama yeye waweze kujihalalisha zinaa kwa jina la dini, hata kwa gharama ya kuwasingizia maimamu bali hata kumsingizia mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).
Na hakika uharibifu unaopatikana katika ndoa ya mut’a ni makubwa kwa pande tofauti:
1-Inapingana nasi (maelezo) ya kisheria kwa sababu ni kuhalalisha alicho kiharamisha Allah.
2-Hakika limesababisha jambo hili (la kuhalalisha mut’a) kutengeneza riwaya za uongo na kuzinasibisha kwa maimamu (‘Alayhi sallam) pamoja na matusi machafu yaliyomo ndani yake ambayo hawezi kuyaridhia yoyote yule mwenye imani japo chembe ndogo tu.
3- Na miongoni mwa uharibifu wa mut’a ni kuruhusu kufanya mut’a na mwanamke aliye jihifadhi,aliyeolewa hata kama yupo kwa mwanamme bila ya mmewe kujua, na katika hali hii wanaume hawatakua na imani kwa wake zao,kwasababu inawezekana mwanamke kuolewa kwa mut’a bila mumewe wa kisheria kufahamu na bila ridhaa yake;na huu ni uharibifu hakuna uharibifu zaidi ya huu. Tazama(FURU’IAL KAFIY 5/463),(TAHDIYBUL-AL AHKAMI 7/554)-(AL- ISTIBSAAR 3/145).
Yatakuaje mawazo yake tu na hisia zake siku atakapogundua kuwa mkewe ambae yupo katika himaya yake ameshaolewa na mwanamume mwingine ndoa ya mut’a?!
4- Na wazazi vilevile hawatakuwa na imani na mabinti zao wadogo kwa sababu wanaweza kuolewa ndoa ya mut’a bila wao kujua, ni anaweza baba kustukizwa na uja uzito wa mwanae mdogo , …kwa nini …..imekuaje…? hajui…..ni ya nani ?hajui pia ,aliolewa na mtu?ni nani? Hakuna anae juwa, kwa sababu alimuacha akaondoka zake.
5-Watu wengi wanaofanya mut’a wanajiruhusu wao kufanya mut’a na mabinti za watu,lakini wao watakapoendewa na mtu kwa ajili ya kuposa binti zao, au jamaa zao akitaka kuoa mut’a hawakubali na hawaridhiki ,kwa sababu wao wanaona ndoa ya aina hii inafanana sana na zinaa, na kwa hiyo ni aibu kwao nao wanalihisi hilo pale wanapo fanya mut’a na na bint za watu, basi hakuna shaka yakuwa wao wanajizuia kuwaozesha mabinti zao kwa wengine ndoa ya mut’a maana yake ni kuwa wana jihalalishia kufanya mut’a na mabinti za watu wakati wao wanawaharmishia watu kufanya mut’a na mabinti zao.
Ikiwa mut’a imeruhusiwa ki sheria au ni jambo la mubaha basi kwa nini kuna uzito wa kuwaruhusu wageni kufanya mut’a na mabinti zao au jamaa zao?!
6-Hakika ndoa ya mut’a haina kushuhudiza wala kutangaza , wala kuridhia walii wa mke wala hakuna kuridhiana , isipokuwa mut’a ni mkodisho tu,kama inavyo semekana kua Abuu abdillahi kasema hivyo, basi iweje jambo lenye picha kama hii litangazwe na kuenezwa kwa watu?
7-Hakika ndoa ya mut’a imewafungulia mlango wanaume na wanawake wasiokuwa na maadili hasa vijana katika kuuengemeza uchafu wao kwa jina la dini , na limepelekea hilo kuiharibu sura ya dini na watu wake , kwa hiyo yanabainika madhara ya mut’a kidini kijamii na kitabia , na kwa sababu hiyo iliharamishwa mut’a, na kama mut’a ingekuwa na faida isinge haramishwa ,lakini ilipokuwa madhara yake ni makubwa mtume aliiharamisha na Amiril-muminin pia akawa na msimamo huo.
- Login or register to post comments
- Email this page


