05-Kwa Ajili Ya Allaah Kisha Historia: Khumus

 

Hakika  ya khumusu ni kitu kingine kilichotumika vibaya na  wanazuoni na mujtahidina(wakishia),ikawa ni njia ya kuwaingizia mabwana wakubwa ikawa inawaingizia mali nyingi sana.

Ingawa maelezo ya kisheria yanaonyesha kwa mashia wa kawaida hawalazimishwi khumusu. Bali ni nkhiari yao kufanya hivyo , ispokuwa wao wanaruhusiwa kuitumia khumsi kama wanavyo tumia mali zao,  Bali anazingatiwa yule  anayetoa khumus kuwapa mabwana wakubwa kuwa anapata madhambi kwa anapingana na maelezo ya Amiril muuminin na viongozi wa Ahlul Bayt (Alayhim Salaam).

Na ili aufahamu vizuri msomaji  uhakika wa khumus na jinsi ya kutumika kwake tutaielezea  maudhui ya khumus na kushamiri kwake katika historia, na tutayatia nguvu maneno yetu hayo kwa maelezo ya kisheria na maneni ya maimamu na fat’wa za wanazuoni wanaotegemewa na kukubalika maneno yao.

 1. Inasimuliwa na Dharis Al Kinaniy kua aliuliza Abuu Abdillah (Alayhis Salaam): zina imengizwa kwa watu kutoka wapi? Nikasema sijui najitoa muhanga kwa ajili yako, akasema, nikutoka katika khumus zetu Ahlul Bayt isipokua mashia wetu watakasifu hiyo imehalalishwa kwao tangu kuzaliwa kwao (Usuulu Al Kaafiy 2/205) sherehe ya Al Shaykh Mustafa.

 

 1. Inasimuliwa na hakimu Muudhin bin Issa amesema: nilimuuliza baba Abdillah (Alayhis Salaam) kuhusu  kauli yake Mwenyezi Mungu(Subhaanahu wa Ta’ala)

[8:41](واعلموا أنما غنمتم من شيئ فإن لله خمسه وللرسول ولذي القربى) الأنفال  41

{Na jueni ya kwamba chochote mnachokiteka( mnacho kipata ngawira) , basi sehemu yake ya tano ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume  na jamaa zake Mtume} (Al Anfal 41). Akasema Abuu Abdillah(Alayhis Salaam) kwa kueka mikono yake juu ya magoti yake,kisha akaashiria kwa mikono yake akasema {hivyo na apaa kwa Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) nifaida inayopatikana siku hadi siku, isipokua baba yangu amejaalia shia wake kuwahalalishia ili  wajitakase}(Al Kaafi 2/499)

 1. Inasimuliwa na Umar bin Yazid amesema: nilimuona masmaa kwenye mji wa madina amechukua mali kumpelekea Abii Abdillah mwaka huo,Abuu Abdilah akairudisha…ikafikia kusema:ewe Abaa Sayyara tumekuchagulia wewe na  tukakuhalalishia kwa hiyo chukua mali      yako na kila kilichopo mikononi mwa mashia wetu  hapa duniani wao wamehalalishiwa hilo mpaka atakapo kuja mahdi Al-muntadhar (Usulul Kaafi  2/268).

 2. Imepokewa kwa Muhamad bin Muslim kutoka kwa mmoja wao(Alayhis Salaam) hakika hali mbaya watakayo kuwa nayo watu siku ya Qiyama ni pale atakapo simama mwenye khumsi nakusema: ewe mola khumus yangu,na sisi tumeitowa kwa ajili yako kuwapa  mashia wetu ili wawaweke vizuri watoto wao na kwa ajili ya kuwatakasa watoto wao (Usulul Kaafi 2/501. 

 3. Imepokewa kutoka kwa Abii Abdillah (Alayhis Salaam) amesema: hakika watu wote wanaishi chini ya vivuli vyetu isipokuwa sisi tumewahalalishia mashia wetu hilo.[Manla Yahdhuruhu Al Faqiyhu  2/243].

 4. Imepokewa kutoka kwa Yunus bin Ya’qub amesema: nilikuwa kwa Abii Abdillah(Alayhis Salaam) mara akaingia mtu mmoja kutoka katika mji unaoitwa Qanatin akasema: (nimejitolea muhanga kwako, zinaingia mikononi mwetu faida nyingi na  mali nyingi  na biashara na tunajua kuwa kuna haki yenu ndani yake nasi hatukulitekeleza hilo ipasavyo, akasema (Alayhis Salaam) hatujawatendea haki pale tulipowalazimisha jambo hilo,)[Manla Yahdhuruhu Al Faqiyhu  2/23].

 5. Imepokewa  kutoka kwa Ally bin Mahziyar,kuwa amesema nimesoma katika kitabu cha Abii Jaafar (Alayhis Salaam) nikakuta kuwa alikuwa na mtu mmoja na kumuomba, amruhusu apate chakula chake na kinywaji chake katika khumus,basi akaandika(Alayhis Salaam) kwa mkono wake ( ninaye mpatia kitu katika haki yangu basi yupo katika uhalali)[Manla Yahdhuruhu Al Faqiyhu  2/23].

 6. Alikuja mtu kwa Amiril muumini (Alayhis Salaam),akasema: nimepata mali  nikaitumia,Je ninatoba? Akasema (niletee khumus yangu, akampa khumus yake,akasema (Alayhis Salaam) hiyo ni  yako, hakika ya mtu  anapotubia hukubaliwa toba pamoja na mali yake) [Manla Yaahdhuruh Al Faqiyhu 2/22].

 

Basi riwaya hizi na nyinginezo nyingi ziko wazi katika  kuwasamehe mashia  khumus kwani wao wameruhusiwa wasitowe  basi anayetaka kuitumia yeye mwenyewe,au kuila wala asiwape Ahlul Bayt chochote basi hiyo ni halali yake  kufanya atakavyo na wala  hakuna dhambi juu yake, bali pia haiwapaswi wao kutoa mpaka atakapo kuja mahdi anaesuniriwa, kama ilivyopokewa katika riwaya ya tatu.

Na hatakama angekuwepo Imamu (kiongozi wa kishia) asingepewa mpaka asimame kiongozi wa Ahlu Bayt, basi itawezekana vipi  kupewa wanazuoni na mafaqihi?

Fatwa za mafaqih na wanazuoni wanao tegemewa katika kuwazuia mashia kutowa khumusi.

Kufuatana na hoja zilizo tangulia na nyinginezo nyingi zilizoweka wazi  kusamehewa mashia kutowa kuhums zilitolewa fatwa nyingi kutoka kwa wanazuoni wakubwa na mujtahidin miongoni mwa wale wenye upeo mkubwa wa elimu na ambao wana nafasi kubwa kati ya wanazuoni wetu, zinazo halalisha khumsi kwa mashia na kutompa mtu yoyote mpaka atakapo kuja  kiongozi wa Ahlul Bayt:

 1. Almuhaqaqu Al –Hiliyunajmu-ddiyn Jafar bin Al Hassan aliefariki [676 H] alisisitiza kuwepo uhalali wa manufaa  na majengo na sehemu za biashara kwa siri na kusema: haipasi kuitoa hisa inayo patikana katika kuwapa watu wa khumus, Tazama kitabu Sharaiu Al-Islam  182-183   Kitabul Khumus.

 2. Yahya bin Said Al- hiliyu aliyefariki[690H] alipendelea  mtazamo wa kuruhusu khumus na nyinginezo kwa mashia ikiwa ni takrima na fadhila kutoka kwa  maimamu wa Ahlul-Bayti kama ilivyo katika kitabu chake (Al Jamiu Lisharaiu Na:151).

 3. Al Hassan bin Almut-har A Hiliyu ambae aliishi katika karne ya nane,alitoa fatwa ya kuruhusu khumus kwa mashia na kuwazuia kutowa kama ilivyo katika kitabu (Tahrur Al Ahkam Na:75).

 4. Ashahidu Athaniy aliofariki [966 H] amesema katika (Majmai Al Faaida wal Burhan 4/355-358): alionelea kuruhusu khumus bila sharti na akasema: hakika huo ndio usahihi kama ilivyo katika kitabu (Masaliki Al Afhamu,68).

 5. Al Muqadas Al Ardabiyliyu aliyefariki[993H] nae ni faqih katika  mafaqih wakubwa wa zama zake  mpaka wakambandika jina  la (Al Muqadas) amesema kwa kuruhusu moja kwa moja kutumia mali za wasiokuwepo kwa ajili ya mashia khasa wakati wa shida,na akasema:habari zote hizi zinajulisha kuondoka wajibu wa khumusi moja kwa moja  zama ghiba ya imamu na kuridi kwake , kwa maana ya kukosekana  ulazima na  kukosekana ushahidi wa nguvu wa faida na machumo na kutokuwepo ngawira.

Ninasema: neno lakehili limetolewa katika neno lakeAllah (Subhaanahu wa Ta’ala)

(واعلموا أنما غنمتم من شيئ)

{Na jueni ya kwamba chochote mlicho kipata kitika   ngawira}Al anfal:41. kisha akabainisha kuwa kuna riwaya nyingine kutoka kwa  Al-Mahdiy akisema mashia tumewahalalishia khumus.

 1. Al-Allama Salar amesema: hakika viongozi wameruhusu khumus katika zama za ughaiba kwa kuwatukuza na kuwakirimu mashia tu. Tazama kitabu (Al-Marasiym 633).

  Al-Allama Salar amesema: hakika viongozi wameruhusu khumus katika zama za ughaiba  kwa kuwatukuza na kuwakirimu mashia tu. Tazama kitabu(Al-Marasiym 633).

 2. Asayid Mohammad Ali Tabatabay aliyefariki mwanzoni mwa karne ya kumi na moja amesema: kauli sahihi  ni kuruhusu (Madariku Al Afham  344).

 3. Mohammad Baqir Asabzawariyu aliyefariki mwishoni mwa karne ya kumi na moja amesema: faida inayopatika katika habari nyingi,katika uchunguzi wa kuruhusu khumusi kama vile sahihi al harith bin Mughira,na sahihi Al Fudhalaa na riwaya ya Muhammad bin Muslim,na riwaya ya Daudi bin Kathiyr na riwaya ya Sinan na sahihi ya Zurara na sahihi ya Ali bin mahziyaar na ya Kurayb: ni kuhalalisha khumus kwa mashia.

  Na akaingia katika kuzijibu baadhi ya hojjah zinazo pingana na rai hii akasema: hakika hojjah zinazo ruhusu ni sahihi zaidi  kuliko nyengine kwa hiyo hana nafasi mtu kuziacha kwa ajili ya hojjah nyingi , kwa ujumla ni kwamba kauli ya kuhalalisha khumusi wakati wa ghaiba ina nguvu sana (Tazama kitabu Dhukaira Al Maadi  292).

 4. Mohammad Hassan al Faydhu Al-Kashaaniy katika kitabu chake (  Mafatihu Al-sharia(229) (Miftahu 260) amechagua msimamo unaoonelea kuanguka yote yanayo mstahiki Al-mahdi, akasema: kwa kulihalalisha hilo viongozi wetu  kwa ajili ya mashia.

 5.  Jaafar Kashifi Al Ghatai aliyefariki(1227 H) katika  kitabu Kashif Al  Ghatai(364): ametaja uhalali wa khumusi kwa maimamu na kutokuwa wajibu kuitowa kuwapa.

 6.  Mohammad Hassan Al Najafiy aliefariki (1226 H) katika kitabu  Jawahiru Al Kalaami ,6/141 ameamua kuruhusu kuchukua khumus mashia katika zama za ghaiba bali na zama za kurudi , na kubainisha kuwa  maelezo haya yana karibia kuwa mutawaatir (habari iliyo pokewa na watu wengi ambayo haina wasiwasi ukweli wake)

  .

 7.  Ninamalizia kwa sheikh Ridha Al Hamdaniy aliefariki (1310 H) katika kitabu chake Misbahu Al faqiyh (155): basi ameruhusu khumus katika hali ya ghaiba, na Sheikh Al Hamdaniy huyu ni mtu wa karibuni sana (si mtu wa zamani) kabla ya karne moja  au zaidi.

 

Kama hivyo tunaona ya kwamba kauli ya kuhalalisha khumus kwa mashia,na  kuwasamehe wao kutowa kauli hiyo ndio inayojulikana kwa wanazuoni wote wazamani na wa sasa  na ndio kauli iliyofanyiwa kazi mpaka mwanzo wa karne ya kumi na nne, achilia mbali kuwa ndiyo yenye ushahidi wa uhalali wake, ,basi itawezekana vipi na ili hali ni hii kutowa khumsi na kuwapa wanazuoni? Pamoja na kuwa maimamu (Alayhis Salaam) waliikataa khumus na wakairudisha kwa wenyewe na wakawasamehe kutowa  hiyo khumusi, je inawezekana kuwa wanazuoni ni bora kuliko maimamu (Alayhis Salaam)?

Hakika fat’wa za kuhalalisha  khumus kuwapa mashia haiishii kwa hawa tulio wataja peke yao  miongoni mwa wanazuoni  bali pia kuna zaidi ya idadi hii  tulio itaja na kwa kupita karne hizi, lakini tumechagua katika kila karne moja katika  mafaqihi na wanaosema kwamba si halali kuwalazimisha watu kutowa khumsi, na kauli hii ndiyo waliyo isema wanazuoni wengi kwa nyakati tofauti kwani ndio kauli inayo tegemewa katika mas’ala haya,na kwa sababu ya kukubaliana kwake na maelezo ya kisheria na vitendo vya maimamu (Alayhis Salaam).

 

Na tutachukua fatwa mbili za wanazuoni wawili miongoni mwa wanazuoni wa  kishia nao ni:  sheikh Al mufidu na  sheikh Al Tuusiy,amesema  sheikh Al mufid: wamekhitalifiana watu miongoni mwetu kwa hilo yaani  khumus wakati  wa ghaibah kila kundi  na msimamo wake ( kisha anataja idadi ya kauli hizo) miongoni mwa wanazuoni kuna wano iondosha kauli ya kutowa khumsi wakati wa ghaiba na kwa sababu ya hojjah zilizo tangulia , na wengine kuna wanaolazimisha izikwe na wanaitafsiri iliyo pokewa isemayo: ( hakika ardhi itatoa hazina zake wakati atapo dhihiri  Al imamu  na kua yeye (Alayhis Salaam) atapo simama, Mwenyezi Mungu atamjulisha hazina zake na atazichukua kutoka  kila sehemu)

Kisha akachagua kauli moja katika hizo.

Kuindosha  khumus kwa mwenye mamlaka  yaani Al Mahdiy, ikiwa ana wasiwasi wa kufikwa na umauti kabla ya kuja kwake atamuusia anae muamini katika akili yake na dini yake,kwa sharti hili mpaka aje amkabidhi imamu, akikuwahi kuja kwake asipowahi atamuusia mtu atakaye isimamia mwenye sifa kama zake kwa uaminifu na dini kisha  wataendelea kuusiana kwa kufuata sharti hili mpaka atakapo kuja imamu, na kauli hii kwangu iko wazi zaidi kuliko zote zilizotazngulia, kwa sababu khumusi ni haki ya imamu aliyejificha na hayakutuka maelekezo yoyote kabla ya kujificha kwake ambayo yanaweza kufuatwa.

Kisha akasema na khumsi inakwenda kama vile zakka ambayo hutolewa pale anapopatikana anaye stahiki kwa hiyo haipasi kuanguka wakati huo , kisha akasema atakapo fuata mtu msimamo huo tulio utaja wa kwamba nusu ya khumsi ni fungu la imamu kisha akaifanya nusu nyingine ni kwa ajili ya familia ya Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) wasafiri wao masikini wao kama ilivyo kuja katika Qur-an.

Amesema atakaye fanya hivi hayupo mbali na kuipata haki katika hilo, bali atakua amepatia, lakini wamekhitilafiana watu wetu katika mlango huu angalia kitabu (Al-MUQNIA: 46)

Na amesema Al sheikh Al Tuusiy aliyefariki (460H) ambae ni muasisi  wa chuo cha kishia

cha Al Najaf na ndiye kiongozi wake wa kwanza baada ya kutaja hukumu za khumus akasema: hii itakuwa katika muda atakao kuja imamu, kisha akasema: ama katika  hali ya kutokuwepo wamewaruhusu  mashia wao kufanya katika haki zao  ndoa, biashara na makazi... ama isiyo kuwa hayo  haifai mtu kujifanyia atakavyo kwa hali yoyote ama kile wanacho stahiki katika khumusi zilizo hifadhiwa wakati wa ghaiba, wamekhitalifiana watu wetu kwa hilo na hakuna hoja maalum isipokuwa kila mmoja  kati yao mafaqihi wa shia amesema usemi wa kuondowa shaka .

 

Kisha Al Tuusiy akazidhibiti hoja hizi katika sehemu nne:

 1. Baadhi yao wamesema hakika jambo hili linaenda  katika hali ya ghaiba mwenendo wa yale  tuliyo ruhusiwa kuanzia wanawake  na biashara- kwa maana ya kwamba katika muda wa ghaiba na kujificha imamu kila kitu ni halali- na hii ndio kauli iliyo sahihi zaidi kwa sababu inakubaliana na maelezo ya kisheria yaliyopokewa kutoka kwa maimamu, na ndiyo kauli ya wanazuoni wengi, (wa kishia)

  .

 2. Wanasema watu inapasa kuhifadhi au kuhifadhiwa khumusi madamu mtu yuko hai yatakapomkaribia mauti basi amuusie mtu anayemuamini katika ndugu zake ili aikabidhi kwa kiongozi atakapofika, au na ausie kama alivyousiwa mpaka aifikishe kwa kiongozi.

 3. Na watu wengine wanasema: inapasa kugawanywa khumusi mafungu sita, matatu ya kiongozi  yatazikwa au yatawekwa kwa mtu muaminifu, na kauli hii ndiyo aliyoichaguwa Al-Tuusiy.

 

Na mafungu matatu mengine yatagawanywa kwa wanao stahiki miongoni mwa mayatima wa familia ya Mohammad na masikini wao  na wakatikiwa na njia wao, na haya  ni miongoni mwa yanayotakiwa kufanyiwa kazi, na kauli hii inalingana na fat’wa  ya mufidu katika kuifananisha khumusi na zaka.

Kisha anasema (na lau wangekuwa watu ni mwenye kutumia njia ya kutoa wasiwasi kwa kuifanyia kazi njia mojawapo kati ya hizi zilizotajwa asinge pata madhambi).

Sheikh Al-Tuusiy ameyadhibiti matumizi ya khumusi katika kauli nne hizi zilizotangulia, na yeye mwenyewe amechaguwa kauli ya nne , lakini akaweka wazi kuwa mtu akichagua kauli yoyote kati ya hizi hana madhambi.

Nasi tunaziona kauli hizi nne, ingawa zimekhitalifiana  katika baadhi ya maelezo lakini tunaziona zimekubaliana katika kitu kimoja, ambacho ndicho tunachokielezea , nacho ni kwamba mali za khumusi ambazo ni mali ya imamu aliyejificha au mtu mwengine hazitolewi kupewa mabwana wakubwa wala wanazuoni.

Na pamoja nakuwa kauli nne hizi zilizotangulia zimekhitalafiana katika namna ya ugawaji wa mali ya khumus isipokua hakuna ndani yake ishara wala maelezo ya wazi yanayoonyesha wajibu au uhalali tu wa kuitowa khumsi au sehemu katika yake kwa mabwana wakubwa na wana zuoni.

Hakika kauli ya nne ambayo ndiyo aliyo ichagua Al shaikh al tuusiy  ndiyo waliyokuwa nayo mashia wote , na Al Tuusiy. Kama inavyofahamika  ndiye muasisi wa chuo cha kishia cha Annajaf  nae ndie sheikh wa kikundi, je hivi unadhani sheikh huyu na mashia wote wa zama zake na wa nyuma yake walikuwa wanakosea .

Basi hii ndiyo fatwa ya kiongozi wa kwanza wa chuo cha Annajaf.

 

Basi sasa tuone fatwa nyingine ya kiongozi mwingine wa chuo hicho  maulana al imamu aliyeaga dunia Abil-  Qasim Al khuuiy  ili itupambanukie tofauti iliyopo kati ya fatwa ya kiongozi wa kwanza wa chuo hiki na fat’wa ya kiongozi mwengine wa chuo hicho hicho.  

Amesema al imamu al khuuiy katika kubainisha anayestahiki kupewa khumus.

 

Khumus katika zama zetu hugawanywa katika sehemu mbili: nusu ni kwajili ya imamu wa zama hizi Al Hujatu Al  Muntadhir mwenyezimungu azifanye fidia roho zetu kwake . Na nusu ni kwa ajili ya banii Hashimu Mayatima wa na masikini wao na walio katikiwa na njia… mpaka aliposema: nusu ambayo inatolewa kwa  imamu (Alayhis Salaam) inarejea katika zama za kujificha kwa naibu wake nae ni Al faqihi mwanazuoni mwenye kuaminika anae jua matumizi yake,ima kwa kumpa au kumuomba ruhusa… Angalia kitabu (Dhiyau Al Salihina Mas’ala 1259, Uk: 347) hakika fatwa ya imamu Al khuuiy ina khitalifiana na fatwa ya Al sheikh Al Tuusiy, sheikh Atuusiy hakusema khumus apewe mwanazuoni, na wamefuata maelezo  ya fatwa yake mashia wote wa zama zake,ili hali tunaona fatwa ya maulana aliyefariki Al imamu Al khuuiy inatoa hoja ya kuitoa khumus au sehemu yake kupewa faqih na mujatahidin (wanazuoni)

.

 

Share