Kuorodhesha Aayah Ambazo Hukmu Yake Imefutwa

 

Kuorodhesha Aayah Ambazo Hukmu Yake Imefutwa

 www.alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

Asalaam alaykum.

Naomba kuorodhoshewa Ayah  zilizofutwa katika Quran (hazifanyi kazi kwa kushuka aya nyingine). Kwa upande wangu hili limekuwa tatizo kubwa sana hasa kutokana na nchi nnayoishi ni ngumu kupata watu wenye ilmu hii. Najua kuwa ni kazi kubwa kuorodhesha Aayah zote hizo lakini nakuombeni hata mungeandika makala inayohusiana na hilo.

Jazaka-A llahu khair.

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

 

Kama ulivyotaja hapo juu kuwa hiyo ni kazi ngumu, kwani inataka makini na wasaa wa kuweza kufanya hivyo. Tutajaribu kutekeleza hilo ombi lako. Hata hivyo, tutaorodhesha zile ambazo zinakuja haraka haraka katika akili. Nazo ni kama zifuatazo:

 

 

1.     Kubatilishwa hukmu ya Aayah zifuatazo Suwratul Baqarah [2]: 219 na Suwratun Nisaa’ [4]: 43 kwa ile Aayah ya Suwratul Maa’idah [5]: 90 – 91.

 

 

2.     Kubatilishwa hukmu ya Aayah zifuatazo Suwratur Ruwm [30]: 39, Suwratun Nisaa’ [4]: 161 kwa zile Aayah za Suwratul Baqarah [2]: 275 – 280.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share