Kuna Aayah Zinazotaja Kuwa Wanawake Wengi Wataingia Motoni?

SWALI:

 

Assalam aleikum warahmatullahi wabarakat,bismillahi rrahmani rrahim,i wanted to ask kuhusu wanawake ndio watakao ingia wengi motoni..kuna hadith sahih bukhari 4.464 narrated imran bin hussain r.a..also bukhari 7:124,7:125,the prophet s.a.w said'i lookd at paradise and found poor people forming its majority of its inhabitants and i looked hell and saw the majority of its inhabitants were women' and another hadith narrated by abu said al khudri that the prophet said 'o people! Give alms, then he went towards women and said 'o women! give alms for i have seen that the majority of the dwellers of hell fire were you (women) they asked why and the prophet replied because they curse frequently and are ungrateful to their husbands' i told my fellow students at my university and thus they wanted an ayyah from the quran, plz inform me about the ayyah in the quran that many women will enter hell. shukran and jaza yenu iko kwa ALLAH.

 


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Shukrani kwa swali lako kuhusu Aayah inayoelezea kuwa wanawake wengi kuwa watakuwa motoni.

 

Hakika ni kuwa hakuna Aayah yenye kutuelezea hayo. Ama Hadiyth zipo na nyengine ni kama ulivyonukuu hapo juu.

 

Hatuelewi ni kwa nini hao wanafunzi wenzako wawe wanataka Aayah baada ya kupewa Hadiyth ambazo ni sahihi? Je, wanataka tu kujua kama zipo Aayah au hawaamini Hadiyth?

 

Isijekuwa hao wanafunzi ni miongoni mwa wale watu wasioamini Hadiyth za Mtume ambao wanajulikana kama Qur-aniyuun ‘The Qur’anites’ au ‘The Submitters’?

 

Jaribu kulifanyia utafiti hilo na kama ni wale wapingao Hadiyth basi soma makala hii ifuatayo yenye kueleza habari zao kwa urefu:

 

Qur-aniyuun – Wanaopinga Hadiyth Za Mtume (Swallah Allaahu ‘Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam)

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share