Uzinduzi Mwingine
Kutokana na hayo yaliyo tangulia tumekwisha fahamu ya kuwa khumsi haitolewi kwa mashehe wala wanazuoni ,na limekuwa wazi jambo hili kwetu kufuatia maelezo ya maudhui hii tuliyo yatowa kwa pande zake zote ,na ni vizuri kwetu kuzindua kua mafakihi na marejeo ya kidini(wanazuoni) wanadai kuwa wao ni katika Ahlu Bait, utamuona moja wao akikuonesha mtiririko wa nasaba yake mpaka kwa kadhim (a.s), jua kwamba ni jambo lisilo wezekana kwa idadi kubwa hii yote ya wanazuoni wa Iraqi Irani sirya Lebanon nchi za ghuba na Pakistan na nyenginezo kua ni katika Ahlul-baiti , na kuhesabu wanazuoni wa Iraqi tu ataona kua ni jambo lisilo wezekana kuwa idadi yote hiyo ya wanazuoni wa Iraqi ni katika Ahlul-baiti , vipi itawezekana tukichanganya na wanazuoni wa miji mingine?bila shaka idadi yao ni kubwa sanasana je itawezekana vipi wote hawa wawe ni katika Ahlul-baiti ???
Na zaidi ya hayo mti wa nasabu ya mtume unauzwa na kununuliwa hapa chuoni , anaetaka kuupata utukufu wa nasabu ya Ahlul Bait ni juu yake kuja na dada yake au mke wake kwa sharti awe mzuri kwa mtukufu mmoja wapo ili astarehe nae,au aje na kiwango cha mali na atapata utukufu kwa moja kati ya njia mbili hizi:- na hili ni jambo maarufu hapa chuoni kwetu (CHUO CHA KISHIA CH ANNAJAF).
kwa ajili hiyo ninasema yasiwahadae yale ambayo wanayafanya baadhi ya watukufu,na waandishi wakati anapoweka mmoja wao mti wa nasaba yake katika ukurasa wa mbele wa kitabu chake ni kwa ajili ya kuwahadaa watu wepesiwepesi matajiri na masikini ,ili wampelekee khumsi za mali zao.
Na mwisho wa utafiti wa khumus sitosahau kuitaja kauli ya rafiki yangu mpenzi mshairi hodari Ahmad Al Safy Al Najafiy(r.a) ambae nilifahamiana nae baada yakupata shahada ya Ijtihadi tukawa marafiki wapenzi achilia mbali tofauti ya umri ilopo kati yetu , kwani alikuwa akinizidi kwa miaka takriban thelathini au zaidi ,nakumbuka alipo niambia mwanangu usiichafuwe nafsi yako kwa mali ya khumsi kwani ni mali ya haramu , na akanidadisi kuhusu khumsi mpaka akanikinaisha kua ni haramu , kisha akanitajia beti za shairi alilokuwa amelitunga kwa ajili hii, ambazo nilizihifadhi kwenye mfuko wangu wa kumbukumbu , na hapa ninazinukuu kwa kwa faida ya wasomaji watukufu kama zilivyo, anasema (r.a),
“Nina washangaa watu, kuomba omba kwa kutumia dini
Basi ikiwa kupata elimu ndio sababu ya kuomba omba basi itakuwa ujinga ni bora kuliko elimu, na je katika zama za Mtume(s.a.w) kulikuwa na watu wanaoishi kutegemea mali za watu kwa jina hilo? Na hata kama Mwenyezi Mungu ameifaradhisha zaka basi hakuna kuchukuliwa kwa udhalilishaji basi kwa malengo, wametuletea watoto wa sasa ni kazi,na haikua kwa watoto ni geni
- Login or register to post comments
- Email this page


