Ameoa Wamepata Mtoto Lakini Kamwacha Kwa Ajili ya Wazazi Wake

SWALI:

 

ssalam Aleikum. Shekhe ipi hukmu ya mtoto wa kiume ambaye aliowa akazaa na kuwachana na mkewe juu ya wazazi wake?


 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani kwa swali lako kuhusu hukmu ya mwanamme aliyeoa na kuacha kwa sababu ya wazazi.

Hakika ni kuwa hili swali linaning’inia kwani hakuna maelezo yoyote kuhusu hilo lililotokea. Je, ni kwa nini wazazi wakamuamuru mtoto wao amuache mkewe?

 

Majibu kwa swali hilo linaweza kutupatia sisi mwangaza na kuweza kukunasihi inavyotakiwa. Zinatakikana sababu za msingi kwa jambo kama hilo kukubalika. Ikiwa kuna kosa lolote upande wa mke inatakiwa zifuatwe njia muafaka za kutatua tatizo hilo ili wanandoa hao waishi kwa wema na uzuri. Endapo njiz zote zimetumika na mke hakuweza kujirekebisha ndio mume atoe talaka.

 

Na ikiwa mke atakuwa hana makosa yoyote yale wazazi na mume watakuwa na makosa ya kuchukua uamuzi huo na hiyo itakuwa ni dhulma kwa wote hao dhidi ya mwanamke. Na ni nasaha kwa mwanamke aliyeachwa kwa njia hiyo afanye subira kwani subira huleta faraja na hakuna mwenye kusubiri kwa ajili ya Allaah Aliyetukuka ila hupata ujira mara mbili. Na kwa uchaji wako wa Allaah Aliyetukuka, Allaah Atamfungulia mwanamke huyo njia ambayo hajaitarajia kabisa. Nasaha ni kuwa amsamehe mwanamme huyo aliyemuacha kwa kosa hilo na pia wazazi wa mwanamme na Allaah Aliyetukuka Atamlipa kwa hayo inshaAllaah.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share