Amfuate Imaam Anaporukuu Japokuwa Yeye Maamuma Hakumaliza Suwratul-Faatihah?

 

Amfuate Imaam Anaporukuu Japokuwa Yeye Maamuma Hakumaliza Suwratul Faatihah?

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

Asalam alaikum!

Kama mimi nipo nyuma ya imam na imam ameenda kurukuu kabla mimi sijamaliza surat alfatha je mimi nimfuate au nimalize ndio nimfuate?

 

 

JIBU: 

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametupatia muongozo barabara pale aliposema:

 

“Imaam amewekwa kufuatwa, akirunukuu nanyi rukuuni …” 

 

Kwa ajili hiyo, Imaam akirukuu kabla ya wewe kumaliza Suwratul-Faatihah inabidi uache pale ulipokomea ili kumfuata Imaam wako. Na kufanya hivyo ndio ukamilifu wa Swalaah yenyewe.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share