Tashahhud Ya Kwanza Ni Fupi Au Ni Kamilifu Kama Tashahhud Ya Pili Pamoja Na Swalaatul-Ibraahimiyyah?

SWALI:

 

Bismillahi Rahamni rahiym, Assalam aleykum warahmatullahi.

 

Natangulizi kwa kutoa shukrani zangu za dhati kwanza kwa Alha SubhanahuWataala na pili kwenu nyie kwa kutuelimisha kupitia mtandao, inshaAllah jaza zenu mtaipata kwa Allaw. Sawli langu ni kuhusu tahiyatu ya kwanza mimi ninavyofahamu katika kikao cha kwanza husoma hadi pale "assalam aleyka ayyuha nabbiyu warahmatullahi wabarakatuhu, assalam aleyna wa alaa ibadi llahi swaalihiyn" kisha ukatoa shahada halafu ukainuka kisha katika kikao cha pili ndio huamlizia kwa kumswalia Mtume swallahau alayhi wassalam. ila nimepata maoni mangine kuwa katika kikao cha kwanza pia yafaa kumswalia Mtume. Sasa nawaomba ndugu zangu katika imani munijuze zaidi.Shukran tena.


 

JIBU: 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho. 

Shukrani kwa swali lako kuhusu kusoma kisomo cha Tahiyyatu katika kitako cha kwanza na cha pili.  

Ni kweli suala hilo lina tofauti baina ya Maulamaa. Kuna wanaoona ni vizuri kusoma Tashahhud na kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam katika kikao cha kwanza cha Tashahhud. Na kuna wengine wanaona kuwa inatosha tu kusoma Tashahhud hadi utakapofika Ash-hadu an Laa ilaaha illa Allaah, na katika kikao cha pili cha Tashahhud ndio inaongezwa na kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na pia du’aa za kuepushwa na adhabu nne, na zingine mbalimbali anazotaka kuomba mtu. 

Msimamo wa kwanza ni wa Imaam Ash-Shaafi’iy, Ibn Hazm, Al-Albaaniy, Ibn Baaz na Maulamaa wengine. 

Na msimamo wa pili ni wa Jamhuur; wanachuoni wengi.

Na misimamo yote miwili ina dalili zake. 

Tunaona msimamo wa kwanza ni bora zaidi kwani una ukamilifu na ujira zaidi kwa mwenye kujumuisha yote mawili. Na misimamo yote miwili ina dalili zake.

 Tafadhali bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo zaidi:

 

043 - Tahiyyaatu (Tashahhud) Ya Kwanza

045 - Wajibu Wa Tashahhud Ya Kwanza Na Hukmu Ya Du'aa Ndani Yake Pamoja Na Matamshi Yake

46 - Kumswalia Mtume Pahala Pake Na Matamshi Yake Mbali Mbali

47 - Nukta Muhimu Kuhusu Kumswalia Mtume Wa Ummah ‘Swalaatu 'Alan-Nabbiyy’ (Nukta Ya Kwanza Na Ya Pili)

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share