Viumbe Gani Wameishi Duniani Bila Kukaa Matumboni Mwa Mama Zao?

SWALI:

 

Assalam aleikum Warmatullah Wabarakatu me ningependa kufahamu ni viumbe gani wameishi duniani bila ya kukaa matumboni mwa mama zao? WABILLAH TAWFIQ

 


 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Shukrani zetu kwa swali lako kuhusu viumbe walioishi duniani bila kukaa kwenye matumbo ya mama zao.  Miongoni mwao ni:

 

 

  1. Nabii Aadam (‘Alayhis Salaam).

 

  1. Hawwaa, mke wa Nabii Aadam (‘Alayhis salaam).

 

  1. Ngamia wa Nabii Shu’ayb (‘Alayhis Salaam).

 

  1. Ndege waliokuja kumpiga Abraha na jeshi lakewaliokuwa wamekuja Makkah kuvunja al-Ka’bah.

 

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share