Vyuo Gani Vya Kwenda Kusoma Dini Nje?

Vyuo Gani Vya Kwenda Kusoma Dini Nje

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Assalamu Aleikum,

I will be coming for a holiday in Mombasa Kenya on the ....... for two months. Is there any place that you reccommend I could go and learn more about Islam for two these two months that i will be in Mombasa. I can read the Quran fluently but i need to learn the tajweed, Arabic language and other courses of Islam. My brother wants to go to Darul Mustafa in Tarim, Yemen for his Islamic Studies with Sh. Habib Ali Al Jifri, would you reccomend such a place or is there an alternative e.g. in Madina or Makkah.

Assalamu Aleikum

 


 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Kwenda kwako Kenya na kutaka kusoma 'ilmu tofauti ikiwemo mada ya lugha ya Kiarabu ni jambo zuri lakini muda wenyewe ni mfupi.

 

Kenya kuna ndugu wengi wanaofuata Manhaj Sahihi ambao unaweza kuulizia na ukaelekezwa kwao; cha msingi ni kuulizia nani wanaofuata na kulingania hii Dini kwa kufuata Manhaj ya Salafus Swaalih (Mwenendo wa Wema Waliotangulia kuanzia Maswahaba, Matabi'iyna na Waote waliowafuata wao kwa wema).

 

Nasaha zetu ni kuwa usiende kusoma huko kwenye huo ulichoeleza cha huyo mtu huko Tarim, kwani hao uliowataja ni Masufi wakubwa tena Wanachuoni wakubwa wameshatahadharisha kuwa ni watu wa bid’ah na matamanio na hata mafundisho yao yana aina za ushirikina na ghuluw (uvukaji mpaka wa Dini).

 

Hivyo, tunakunasihi ujihadhari na kaa mbali na vyuo kama ulivyovitaja na watu wake ambao wanamzulia Mtume na kueneza mafunzo ya upotofu.

 

Sehemu bora ya kusoma ni kwenye vyuo vya Kisalafi popote vilivyopo duniani, na sehemu zingine za kusoma ni Makkah na Madiynah, katika miji hiyo miwili mitukufu mtu atapata fadhila zaidi ya kufanya ‘Ibaadah katika Misikiti Mitukufu ambamo thawabu zake ni maradufu na pia kupata darsa za Mashaykh wakubwa humo ndani ya Misikiti hiyo mitakatifu mbali na masomo ya kawaida.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share