Mume Taabaan Katika Tendo La Ndoa, Na ‘Ibaadah Zake Dhaifu

SWALI:

 

Assalama Alaikum,

nimeishi na mume muda miaka 29, lakini miezi 6 sasa anamatatizo katika tendo la ndoa, anakua na hamu na mimi, lakini akianza kukutana na mimi anakua hawezi, nimesikia katika vyombo vya habari vya dini ya kiislamu, kuwa inawezekana pengine sote tunasibiwa na shetani, na mimi naziona ishara ambazo zinasababisha kusibiwa na shetani na pia imeelezwa kuwa inalazimika kufanya rukia au kuzidisha ibada, mimi najitahidi kwa kuzidisha ibada, lakini la kushangaza mume yeye nikimwambia ajishughulikie hataki kujitibu, pia kuswali kwake kwa tabu anasali anavyoona yeye, yaani mfano hasali msikitini au vipindi havitimii au atasali nyumbani, na jitihada imefanyika kumhimiza na kumuombea dua ili mume wangu afanye ibada lakini bado hajakubali, na mimi sina raha juu ya matatizo aliyonayo mume wangu. Je niongeze juhudi gani ili ndoa yetu iwe na furaha kama inavyotakiwa?


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Shukrani zetu kwa swali lako kuhusu mume kuwa taabani katika tendo la ndoa.

Hakika ukosefu au kupungua kwa nguvu za kiume unasababishwa na sababu nyingi. Miongoni mwazo ni:

 

1.     Ugonjwa

2.     Uzee

3.     Kusibiwa na Shaytwaan

 

Ama kusibiwa na Shaytwaan inatakiwa umpeleke mumeo kwa Shaykh aliye mzoefu katika kusoma Ruqyah ili amsomee na Insha’Allaah atapata nafuu. Ikiwa udhaifu umetokana na uzee au ugonjwa itabidi umtafutue daktari wa kuweza kumtazama na kumpatia dawa muafaka.

 

Hata hivyo, huo unaweza kuwa ni mtihani kutoka kwa Allaah Aliyetukuka kwako na kwake kutizamwa kama mtabaki vipi katika Dini yenu na kama mtaweza kushukuru na kuvumilia badala ya kwenda kwa waganga na wachawi.

Inabidi usichoke kuzungumza naye kuhusu yeye kufanya ‘Ibaadah na pia kutumia watu walio karibu naye kufanya kazi hiyo. Na hivyo hivyo muombe sana Allaah Aliyetukuka kila saa na wakati ili Amuafu na Amuondolee tatizo hilo la kutofanya ‘Ibaadah mumeo.

 

Na bila shaka Allaah Aliyetukuka husikia Du’aa za waja Wake.

 

Kwa maelezo na manufaa zaidi bonyeza viungo vifuatavyo:

 

 

 

Ikiwa Hawaridhiani Katika Kitendo Cha Ndoa Wafanye Nini?

 

Anafaa Kuachika Ikiwa Mume Hawezi Tendo La Ndoa?

 

Mume Kahama Chumba Kwa Miezi 3 Hafanyi Tendo La Ndoa, Akiulizwa Anasema Anachoka Kazini

 

Anampenda Sana Mume Wake Lakini Hawana Raha Katika Tendo La Ndoa, Wafanyeje?

 

Mke Analalamika Mume Ana Mashetani Yanamfanya Asiweze Kukamilisha Tendo La Ndoa

 

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share