Biashara Ya Manukato Ya Wanawake Ni Haramu?

SWALI:

 

KUTOKANA NA MIPAKA YA MATUMIZI YA MANUKATO KWA WANAWAKE. JE KUFANYA BIASHARA YA MANUKATO NI HARAMU?

 


 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Shukrani kwa swali lako kuhusu biashara ya manukato.

Manukato ni halali kupakwa kishari’ah na wanaume na wanawake.

Wanaume kwao ni Sunnah kupaka wakati wowote ule, wakiwa nyumbani na nje ya nyumba.

Ama wanawake wanafaa wapake wakiwa ndani ya nyumba tu.

 

Kwa ule uhalali uliopo wa biashara hiyo, wewe muuzaji huna makosa yoyote ikiwa mwanamke atanunua kisha ajipake akiwa anatoka nyumbani. bali Makosa yatakuwa kwa ima wazazi wake au mume kwani wao wanafaa wamjulishe na kumnasihi kuhusu hilo.

 

Kwa muhtasari ni kuwa unaweza kuuza bila ya tatizo lolote lile.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share