Inafaa Kushirikiana Na Makafiri Kuwachangisha Pesa Waislamu Wenzao Kuzitumia Kwa Siri?

 

SWALI:

Asalam Aleikum, Natarajia U mzima na Allah s.a.w, Apate kukuhifadhi na kukupa afya. Sheke nilikuwa na swali au ombezi moja na natarajia utanifafanulia au kunijibu hili hoja ambalo linalo ni kera sana

 kuna watu ambao wanaowahubiria wasio kuwa waislamu (wakristo) kupitia kitabu chao, na kupata kuwasilimisha wengi sana, kwangu mimi nimefurahia jambo hili. Lakini kitu kinacho ni kera ni kuwa kuna baadhi yao wanaoshirikiana na wasiokuwa waislamu kuandaa mikutano hayo halafu kuchangisha na kugawanana nao hela.  je uislamu unaruhusu jambo hili la baadhi ya wahubiri kushirikia na makafiri yaani kupanga kama game hivi halafu kula pesa za wailsamu kwa siri je yafaa ?  naomba kama unaweza kunisaidia na aya au hadithi au kauli ya mwanachuoni yeyote yule abainishaye uchafu huu kupitia kitabu na sunnah. natarajia kama unaweza uniandikie kama nakala hivi

wasalam aleikum


JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukrani zetu kwa swali lako kuhusu kushirikiana kwa Waislamu na Wakristo katika ukusanyaji wa pesa katika mihadhara.

Uislamu umeweka misingi ya ukweli na uaminifu na mlinganiaji Muislamu anatakiwa awe aifanye kazi ya ulinganiaji kwa kufuata maadili bora katika ulinganizi kama yalivyofundishwa na Uislamu. Muislamu haifai kumdanganya hata asiyekuwa Muislamu kwa njia yoyote ile.

Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alitutahadharisha kwa kutuambia: “Mwenye kutudanganya si katika sisi” (Muslim).

Na haifai kwa Muislamu kushirikiana na hata Muislamu mwenziwe licha ya Mkristo katika kuwalaghai na kuwatapeli wanaadamu pesa au kitu chochote kingine. Hivyo, jambo hilo ambalo linafanywa halifai na pesa hizo zinakuwa ni za haramu kwao kutumia.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share