Kukaa Faragha Na Mwanamke Unayetaka Kumuoa Inajuzu?

SWALI:

Kama kuna mwanamke ninatarajia kumuoa na kwao washanijua lakini nikasema baada ya kumaliza elimu yangu ya chuo nitamuoa jee naweza kukaa nae peke yake tukawa tunaongea maswala yoyote tukiwa wawili tuu au hairuhusiwi hadi nitapomuoa, na nini hukmu ya wanaoishi na wanawake kwa kutaraji kuwaoa na wakafanya nao mapenzi?


JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kukaa faragha na mwanamke unayetaka kumuoa.

Kigezo kuwa wazazi wao wanakujua wewe si ruhusa au kibali cha nyinyi kukaa peke yenu faragha au kuzungumza. Inatakiwa kwanza uende ukampose kwa wazazi wake hao rasmi na kufanya hivyo utakuwa umeweka dhamana asiposwe na mwengine kwani hakuna posa juu ya posa katika Uislamu.

Ukishamposa utakuwa na ruhusa ya kuweza kukutana naye lakini si faragha bali ni nyumbani kwao ukiwa wewe, yeye na Mahram ya huyo msichana uliyemposa.

Kukaa faragha haifai kwani Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

Hakai mwanamme na mwanamke peke yao (faragha) ila watatu wao ni Shaytwaan”. At-Tirmidhiy

Na akasema tena: “Shaytwaan hutembea kwenye mwili wa binaadamu kama damu (inavyotembea)”.

Kwa hiyo, haifai mwanamke na mwanamme kukaa faragha kwa hali yoyote ile.

Soma zaidi makala  pamoja na maswali na majibu katika viungo vifuatavyo:

Ikhtilaatw (Kuchanganyika Wanaume Na Wanawake)

Mawasiliano Na Mchumba Baada Kuposa Na Kabla Ya Ndoa

Mchumba Bado Hana Uwezo Kunioa, Je, Kuwasiliana Kabla Ya Ndoa Kunakubalika?

Anataka Kuishi Na Mchumba Wake Chumba Kimoja Kabla Ya Kuoana

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share