Anajua Kuwa Ribaa Ni Haraam Lakini Anaweka Makusudi Pesa Banki Ili Aipate Hiyo Ribaa Kisha Aitolee Sadaka

SWALI:

asalam alaykum warahmatullah wabarakatuh kwa fadhila za allah (subuhanah wataala) na mtume wetu muhammad (swalallah alayh wassalam) aiwezeshe alihidaya kutuadhi nasi inshaallah tuisome ili tuzidi kufadika. amin.

suala langu kwa mujibu wa majibu mbalimbali yanayohusiana na riba hususan jibu la endapo utakua kuna riba imeingia katika akaunti yako uitolee kama sadakaa kwa wanawositahiki jee ikiwa najua dhati kuwa riba inayopatikana ni haramu lakini ikawa nimewekeza pesa nyingi katika bank isiyokuwa ya kiislamu kama mtaji kwa lengo la kuipata hiyo riba na baadae ikawa ninaitumia kwa malengo ya kuitasaduk kwa wale wahitaji tu na sivinginevyo, jee naruhusika kwa makusudi kuekeza katika namana hii?


 

JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukrani zetu kwa swali lako kuhusu kuweka pesa kwa makusudi benki ili zipate ribaa.

Ni dhambi Muislamu kuweka pesa benki kwa kusudio la kupata ribaa na Muislamu anatakiwa atafute mbinu zote za kujiondoa katika ribaa ambayo ni dhambi kubwa katika shari’ah.

Kisha tufahamu kuwa sadaka inayokubaliwa na shari’ah ni ile inayotolewa kutoka katika mali yake iliyo safi kabisa. Ribaa si malisafi bali ni chafu hivyo huwezi kutolea sadaka.

Baadhi ya Wanachuoni wanaonelea kuwa ribaa anayopata Muislamu inahitajiwa kutolewa na mwenye kutoa asitarajie malipo kwani si sadaka. Kwa hiyo, tunatakiwa tuwe mbali na ribaa kwa hali zote.

Tafadhali bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo zaidi:

Akipewa Riba Benki Achukue Kisha Awape Maskini Au Aache

Aiwache Ribaa Kwa Manaswara Au Ampe Muislamu Asiyejiweza?

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share