Kununua Nyumba kwa Njia ya Ribaa

SWALI: 

Kuhusu mambo yanahusika riba nimenunuwa nyumba yakuish mimi nawanangu. Munifid wasalam


 

JIBU: 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho. 

Shukrani kwa swali lako kuhusu ununuzi wako wa nyumba kwa njia ya Ribaa.

Hakika Uislamu ni Dini ambayo imepiga vita sana utoaji na uchukuaji wa Ribaa ya aina yoyote ile. Kufanya hivyo ni laana na Muislamu huwa anatangaza vita na Allaah Aliyetukuka na Mtume wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Hilo ni miongoni mwa madhambi saba yenye kuangamiza. 

Inatakiwa ikiwa ulikuwa hujui basi kama inawezekana jitoe na udai haki yako. Na uweke Niyah ya kutorudia tena na uombe msamaha kwa wingi sana.

Soma zaidi suala hilo katika viungo hapa chini ambapo kuna maelezo kwa kirefu kuhusiana na swali lako: 

Mkopo Wa Nyumba Wa Benki (Mortgage) Ni Halali? 

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share