Alama Za Mapenzi Unaweza Kuswali Nazo

 SWALI:

Asalam alaikum, nashukuru alhamdulillah kwa kuwepo chomba hichi ambacho tunaweza kuuliza maswali ambayo yanatutatiza na inshallah mtanijibu kamaa inavyotakiwa kwa uwezo wake allah (s.w). Suala langu hili eti kufanya tendo la ndoa na mumeo au mkeo na kuwa na kwenye mwili wako ukawa mna love bite ni vibaya na eti huwezi kusali sala yako haikubaliwi? Samahanini sana kuweka neno hili kwani sijui nielezee vipi lkn nategemea inshallah mtakuwa mmelifaham. nategemea jibu lenu
 JIBU:

Shukrani zote anastahiki Allah, Muumba wa kila kitu Swalah na salamu zimfikie kipenzi chetu, Mtume Muhammad (s.a.w.), ali zake na Masahaba zake na wanaowafuata kwa wema mpaka siku ya Kiyama.

Katika mas-ala ya kidini hapana haya kwani wanawake wa Kiansari walikuwa wanauliza zaidi ya hayo na bila kuuliza jambo ambalo una shaka nalo basi hakutapatikana ufumbuzi.

Hakika ni kuwa love bites (alama za kimapenzi) si moja katika mambo yenye kuvunja Swalah, kwa hivyo unaweza kuswali nazo na Swalah yako ipo sawa sawa.

Na Allah Anajua zaidi.

 

 

Share