Alama Ya Mwezi Katika Misikiti

 

SWALI:

Nimefurahi sana kuona namna website hii nzuri kwa waislamu inavyotoa nafasi ya kuuliza maswali.
 
Swali: KWA NINI MISIKITI MINGI IMEWEKEWA ALAMA YA MWEZI? KAMA ALAMA HII NDO INATUMIKA KUASHIRIA MSIKITI,VP ISITUMIKE ALAMA NYINGINE KM JUA, MBINGU, MILIMA N.K. KWA SABABU VYOTE HIVI NI VIUMBE VYA M MUNGU NA NI ISHARA YA KUWEPO KWA ALLAH. SWALI HILI LINANICHANGANYA
SANA WAISLAM WENZANGU. NAOMBA MSAADA NA NI JUZI TU MNASWARA ALINIULIZA NIKAMWAMBIA KUWA SIJUI NA TUKAELEWANA NAE KUWA NIFUATILIE

  

JIBU:

 Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola  wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Kwa hakika alama na ishara hizo hazina umuhimu wala maana yoyote katika kuwekwa katika Misikiti au sehemu nyingine zozote. Kwani wakati wa Mtume (Swalla-Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Maswahaba zake (Radhiya-Allaahu 'anhum) alama kama hizo zilikuwa hazipo.

Baada ya hapo huenda Waislamu wakaamua kuwa wawe na ishara kama vile Mayahudi na Manaswara, kwani Mayahudi wana ile ishara ya nyota ya Daudi ambayo ina pembe sita na Manaswara wana ishara ya kuwa na msalaba. Kwa kuwa sisi huwa tarehe zetu za siku na miezi yetu hufuata mwezi, basi baadhi ya Waislam wakaona kuwa waweke hiyo alama ya mwezi kama nembo, lakini kiuhakika haina maana yoyote ya kisheria.

Na Allah Anajua zaidi.

 

Share