Makaroni Ya Zuchini Na Sosi Ya Nyama Ng’ombe

Makaroni Ya Zuchini Na Sosi Ya Nyama Ng’ombe

Makaroni

Vipimo na Namna ya Kuatayarisha

Makaroni  - 500 gms

Kitunguu maji Katakata (chop) - 1

Nyanya/tungule Katakata vipande vidogodogo (dice) - 3

Kitunguu saumu (thomu) Saga au katakata (chop) - 1 kijiko cha supu

Zuchini  - kata slesi za round - 2

Pilipili boga (capsicum) katakakata  - 1

Chumvi Kisia

Pilipili manga - 1 kijiko cha chai

Mafuta  - 2 vijiko vya supu

Namna Ya Kupika:

  1. Chemsha makaroni yaive, chuja maji. Tia siagi kidogo yasigandane.
  2. Katika sufuria, weka mafuta, kaanga vitunguu hadi vilainike na kugeuka rangi kidogo.
  3. Tia kitunguu thomu kaanga.
  4. Tia nyanya, pilipili manga, chumvi changanya vizuri.
  5. Tia slesi za zuchini, na pilipili boga funika kidogo viive kidogo.
  6. Tia makaroni, changanya vizuri yakiwa tayari kuliwa na sosi ya nyama.

Sosi Ya Nyama:

Vipimo na Namna ya Kutayarisha

Nyama ng’ombe Katakata vipande vidogo kiasi - ½ kilo

Tangawizi mbichi saga - 1 kijiko cha chai

Kitunguu saumu (thomu) saga - 1 kijiko cha chai

Kitunguu Katakata (chop) - 1

Nyanya kopo (paste) - 3 vijiko vya supu

Kotmiri - Katakata (chop) - ½ kikombe cha chai

Oregano (bizari ya pasta) - 1 kijiko cha chai 

Namna Ya Kupika

  1. Weka nyama katika sufuria, tia tangawizi mbichi, kitunguu thomu, chumvi changanya vizuri.
  2. Funika uchemshe nyama hadi iwive na kukaribia kukauka.
  3. Tia mafuta, vitunguu, nyanya, nyanya kopo, oregano, changanya vizuri uendelee kupika.
  4. Ikiwiva tia kotmiri, zima moto ikiwa tayari kuliwa na makaroni.

 

 

 

 

 

Share