054-Lu-ulu-un-Manthuwrun: Maiti Anafuatiliwa Na Matatu: Ahli Zake, Mali Na Amali, Zinabaki Amali

 

Lu-ulu-un-Manthuwrun

(Mkusanyiko Wa Hadiyth Mbali Mbali Na Mafunzo Yake)

Hadiyth Ya 54

Maiti Anafuatiliwa Na Matatu: Ahli Zake, Mali Na ‘Amali Zinabaki Naye Amali Zake

 

Alhidaaya.com

 

 

 

عَنْ أَنَسِ (رضي الله عنه) قَال: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم: ((يَتْبَعُ الْمَيِّتَ ثَلاَثَةٌ: أَهْلُهُ وَمَالُهُ وَعَمَلُهُ. فَيَرْجِعُ اثْنَانِ وَيَبْقَى واحِدٌ: يَرِجِعُ أَهْلُهُ وَمَالُهُ وَيَبْقَى عَمَلُهُ)) متفق عليه

 

 Imepokelewa kutoka kwa Anas (رضي الله عنه) amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Maiti hufuatwa na mambo matatu: ahli zake, mali yake, na ‘amali zake. Hurejea mawili na likabakia moja. Ahli zake na mali yake hurejea, na zikabakia ‘amali zake)). [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

Mafunzo Na Mwongozo:

 

 

1. ‘Amali njema anazozitanguliza mtu ni kheri yake kuliko anayoyaacha nyuma, na ‘amali hizi ndizo zitakazodumu. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 

 مَا عِندَكُمْ يَنفَدُ ۖ وَمَا عِندَ اللَّـهِ بَاقٍ ۗ وَلَنَجْزِيَنَّ الَّذِينَ صَبَرُوا أَجْرَهُم بِأَحْسَنِ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ﴿٩٦﴾

Mlivyo navyo nyinyi vinatoweka, na vilioko kwa Allaah ni vya kubakia. Na kwa yakini Tutawalipa wale waliosubiri ujira wao kwa mazuri zaidi ya yale waliyokuwa wakitenda. [An-Nahl 16: 96)]

 

 

2. Kila mmoja ataingia kaburini peke yake, ataacha kila kitu nyuma yake ila ‘amali zake ndizo zitakazomfaa zikiwa ni njema. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

وَلَقَدْ جِئْتُمُونَا فُرَادَىٰ كَمَا خَلَقْنَاكُمْ أَوَّلَ مَرَّةٍ وَتَرَكْتُم مَّا خَوَّلْنَاكُمْ وَرَاءَ ظُهُورِكُمْ ۖ  

  Na kwa yakini mmetujia mmoja mmoja kama Tulivyokuumbeni mara ya kwanza; na mmeyaacha nyuma yenu yote Tuliyokuruzukuni.  [Al-An’aam (6: 94]

 

 

Rejea pia: Maryam (19: 95).

 

Na Rejea: Hadiyth namba (1).

 

 

3. Muumin anapasa akimbilie kutenda ‘amali njema nyingi zimfae Aakhirah. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

وَأَن لَّيْسَ لِلْإِنسَانِ إِلَّا مَا سَعَىٰ ﴿٣٩﴾

Na kwamba insani hatopata (jazaa) isipokuwa yale aliyoyafanyia juhudi.

 

وَأَنَّ سَعْيَهُ سَوْفَ يُرَىٰ ﴿٤٠﴾

Na kwamba juhudi yake itakuja kuonekana

 

ثُمَّ يُجْزَاهُ الْجَزَاءَ الْأَوْفَىٰ ﴿٤١﴾

Kisha atalipwa jazaa kamilifu. [An-Najm (53: 39-41)]

 

 

Rejea pia: Aal-‘Imraan (3: 133), Al-Hadiyd (57: 21), Al-Hashr 59: 18), Al-Baqarah (2: 110), Al-Muddath-thir (74: 74).

 

 

4. Wanaobaki nyuma ya maiti iwe ni funzo kwao watambue kwamba nao bila shaka siku moja watapelekwa kaburini.

 

 

5. Rejea Hadiyth namba (8) (63) (72), (78). 

 

 

 

Share