117-Lu-ulu-un-Manthuwrun: Kusema Analolijua Mtu Au Kukiri Kutokuwa Na Ujuzi Wa Jambo Na Kujikalifisha Nalo

Lu-ulu-un-Manthuwrun

 

(Mkusanyiko Wa Hadiyth Mbali Mbali Na Mafunzo Yake)

 

Hadiyth Ya 117  

 

Kusema Analolijua Mtu Au Kukiri Kutokuwa Na Ujuzi Wa Jambo Na Kujikalifisha Nalo

 

 

 

 

عَنْ مَسْرُوقٍ (رضي الله عنه) قَالَ: دَخَلْنَا عَلَى عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مَسْعُودٍ فَقَالَ: يَا أَيُّهَا النَّاسُ، مَنْ عَلِمَ شَيْئًا فَلْيَقُلْ بِهِ، وَمَنْ لَمْ يَعْلَمْ فَلْيَقُلْ اللَّهُ أَعْلَمُ فَإِنَّ مِنْ الْعِلْمِ أَنْ يَقُولَ لِمَا لاَ يَعْلَمُ: اللَّهُ أَعْلَمُ. قَالَ اللَّهُ تَعَالى لِنَبِيِّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((قُلْ مَا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ مِنْ أَجْرٍ وَمَا أَنَا مِنْ الْمُتَكَلِّفِينَ)) البخاري

Imepokelewa kutoka kwa Masruwq(رضي الله عنه)  amesema: “Tulikwenda kwa ‘Abdullaah bin Mas’uwd (siku moja) akatuambia: “Enyi watu! Anayejua kitu aseme, na asiyejua aseme: “Allaah Anajua.” Hakika miongoni mwa elimu ni kusema katika usilolijua: “Allaah Anajua.” Allaah Alimwambia Rasuli Wake   (صلى الله عليه وآله وسلم): ((Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Sikuombeni ujira wowote juu ya hili, na wala mimi si miongoni mwa wenye kujidai kuzusha chochote kisichohusu. [Swaad (38: 86)])).  [Al-Bukhaariy]

 

 

Mafunzo Na Mwongozo:

 

 

1. Makatazo ya kujikalifisha katika mas-alah ya elimu ya Dini. 

 

 

2. Kutokusema jambo la Dini bila ya kuwa na elimu sahihi yenye dalili wala kutoa Fatwa isipokuwa kwa mwenye elimu ya kutosha. Rejea: Yuwsuf (12: 108).

 

 

3. Allaah (سبحانه وتعالى) Ameonya kujiamulia mtu hukmu bila ya dalili, kwani hivyo ni kumzulia Yeye uongo. Anasema (سبحانه وتعالى):

 

 وَلَا تَقُولُوا لِمَا تَصِفُ أَلْسِنَتُكُمُ الْكَذِبَ هَـٰذَا حَلَالٌ وَهَـٰذَا حَرَامٌ لِّتَفْتَرُوا عَلَى اللَّـهِ الْكَذِبَ ۚ إِنَّ الَّذِينَ يَفْتَرُونَ عَلَى اللَّـهِ الْكَذِبَ لَا يُفْلِحُونَ﴿١١٦﴾

Na wala msiseme zinayotetea ndimi zenu uongo; hii halaal na hii haraam ili mumtungie Allaah uongo. Hakika wale wanaomtungia Allaah uongo hawafaulu. [An-Nahl (16: 116)]

 

 

4. Elimu ya Mwanachuoni (‘Aalim) haipunguki kwa kutokujua jambo na kulikiri.

 

 

5. Funzo kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na himizo la kufuata kigezo chake.

 

 

6. Inapokuwa halijui jambo analoulizwa mtu la elimu ni vyema aseme: “Allaah Anajua”: na anapolijua aseme: “Na Allaah Anajua zaidi.”

 

 

7. Kukiri kutokujua jambo la elimu ni dalili ya unyenyekevu wa mtu na kinyume chake ni kujionyesha sifa ya upeo wa elimu asiyokuwa nayo hakika mtu, kwani kila mmoja ana upeo wa kiasi fulani tu cha elimu. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَفَوْقَ كُلِّ ذِي عِلْمٍ عَلِيمٌ ﴿٧٦﴾

Na juu ya kila mwenye elimu yuko mwenye elimu zaidi. [Yuwsuf (12: 76)].

 

Share