005 - Swali La 5: Wakati Gani 'Amali (Matendo) Inakuwa 'Ibaadah?

Swali La 5:

متى يكون العمل عبادة؟

 

Wakati gani ‘amali (matendo) inakuwa ‘Ibaadah?

 

Jibu:

إذا كمل فيه شيئان وهما كمال الحب مع كمال الذل قال الله تعالى

 

Matendo yanakuwa Ibaadah yanapotimia ndani yake mambo mawili nayo ni: Ukamilifu wa upendo pamoja na ukamilifu wa unyenyekevu.

 

Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema:

وَالَّذِينَ آمَنُوا أَشَدُّ حُبًّا لِّلَّـهِ ۗ

 

Na wale ambao wameamini wana mapenzi zaidi kwa Allaah.[1]

 

Anasema tena:

 

إِنَّ الَّذِينَ هُم مِّنْ خَشْيَةِ رَبِّهِم مُّشْفِقُونَ ﴿٥٧﴾

Hakika wale ambao kwa kumuogopa Mola wao ni wenye kukhofu  (huku wakinyenyekea)[2]

 

Na mambo hayo Allaah (سبحانه وتعالى) Ameyakusanya katika Aayah kwa kusema:

 

إِنَّهُمْ كَانُوا يُسَارِعُونَ فِي الْخَيْرَاتِ وَيَدْعُونَنَا رَغَبًا وَرَهَبًا ۖ وَكَانُوا لَنَا خَاشِعِينَ ﴿٩٠﴾

Hakika wao walikuwa wakikimbilia katika mambo ya kheri, na (walikuwa) wakituomba kwa matumaini na khofu, na walikuwa Kwetu wenye kunyenyekea[3]

 

 [1] Al-Baqarah (2: 165).

[2] Al-Muuminuwn (23: 57).

[3] Al-Anbiyaa (21: 90).

 

Share