014 - Ni Ipi Dalili Inayojulisha Kujumuisha Mojawapo Ya Mafungu Hayo Kuwa Ndio Dini Yote?

Swali La 14:

 

Ni ipi dalili inayojulisha kujumuisha mojawapo ya mafungu hayo kuwa ndio Dini yote?

 

Jibu:

 

Allaah (سبحانه وتعالى) Anasema:

 

إِنَّ الدِّينَ عِندَ اللَّـهِ الْإِسْلَامُ ۗ

Hakika Dini mbele ya Allaah ni Uislamu.[1]

 

Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema:

 

 ((بَدَأَ الإِسْلامُ غَرِيبًا ، وَسَيَعُودُ كَمَا بَدَأَ غَرِيبًا...))

 

((Uislamu ulianza ukiwa mgeni na utaondoka ukiwa ni mgeni kama ulivyoanza)).[2]

 

Na akasema tena:

 

((أفضل الإسلام إيمان بالله))

 

((Uislamu bora kwa mtu ni kumuamini Allaah)).[3][1] Aal-‘Imraan (3: 19)

[2] Muslim, Kitaabul Iymaan Juz 145.

[3] Ahmad 4/114, Atw-Twabaraniy katika Al-Kabiyr kutoka katika Hadiyth ya ‘Amru bin ‘Absa, al-Haythamiy katika kitabu chake ‘Al-Mujma’ (1/63) kuwa watu waliopokea ni thiqah (waaminifu).

 

Share