015 - Ni Ipi Dalili Ya Taarifa Ya Nguzo Za Kiislamu Kwa Upana?

Swali La:  15

 

Ni ipi dalili ya taarifa ya nguzo za Kiislamu kwa upana?

 

Jibu:

 

Ni kauli ya Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) wakati Jibriyl alipomuuliza kuhusiana na Dini.

 

((Uislamu ni kukiri kuwa hakuna mungu isipokuwa Allaah na Muhammad ni Mjumbe Wake, kusimamisha Swalaah, kutoa Zakaah, kufunga Ramadhwaan na kutekeleza Hijjah kwa mwenye uwezo)).[1]

 

Na kauli yake Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم):

 

((بُنِيَ الإِسْلاَمُ عَلَى خَمْسٍ))

 

((Uislamu umejengwa kwa nguzo tano)).[2]

 

Katika Hadiyth hii Mtume (صلى الله عليه وآله وسلم) ametanguliza kutaja Hijjah juu ya Swawm ya Ramadhwaan, na zote Hadiyth hizo mbili ni Swahiyh kwa Imaam al-Bukhaariy na Imaam Muslim.[1] Al-Bukhaariy: 1/114 na 8/513 na Muslim (8).

[2] Imepokewa na Al-Bukhaariy na Muslim.

 

Share