Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Kuoa Zaidi Ya Wake Wanne Nini Hikma Yake?

SWALI:

 

Kwa nini Mtume alioa zaidi ya wake wanne? na hali ya kuwa amri wa kuoa wake wanne ilishatoka? Nitashukuru nikijibiwa

 

 


JIBU: 

Tanbihi: Siku zote unapojiwa na masuala tata kama haya, usihukumu jambo kwa kuitumia dalili moja pekee bali unalazimika kukusanya dalili zaidi ya moja katika suala husika, ili uweze kupata jawabu mnasaba.

 

Jibu:

Kwanza kabisa suala la Mtume (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuoa mke zaidi ya mmoja ni katika jumla ya mambo makhususi aliyoruhusiwa yeye binafsi na Allaah pasi na ruhusa hiyo kuwahusu Waumini wengine.

Allaah Anasema:

"Ee Mtume! Tumekuhalalishia wake zako uliowapa mahari yao, na (wanawake) uliyowamiliki kwa mkono wako wa kuume katika wale uliyopewa na Mwenyezi Mungu na Tumekuhalalishia mabinti wa 'ami zako, na mabinti wa mashangazi zako, na mabinti wa wajomba zako, na mabinti wa dada za mama zako, waliohama pamoja nawe; na (tumekuhalalishia kila) mwanamke Muislam akijitoa mwenyewe bure kwa Mtume, kama mwenyewe Mtume akitaka kumuoa: ni halali kwako wewe tu (kumuoa mwanamke bure bila ya mahari) si kwa Waislam wengine. Bila shaka Tumekwishabainisha tuliyowafaridhia wao katika wake zao na wanawake waliyowamiliki kwa mikono yao ya kuume (Tumekufanyia hivi peke yako wewe Mtume tu) ili isiwe dhiki kwako (ukitaka kumuoa mwanamke mwengine kwa ajili ya kutangaza dini) na Allaah ni mwingi wa kusamehe (na mwingi wa kurehemu). [Al-Ahzaab :50-52]

 

Pili: Kuna hekima na sababu nyingi za Mtume (Swalla Allahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuoa wake wengi, kwa amri ya Mola wake miongoni mwazo ni:

 

1. Kutoa mafunzo na kuandaa wakufunzi

 

2. Kutangaza Dini

 

3. Sababu za kishari'ah

 

4. Masuala ya kijamii

 

5. Sababu za kisiasa, n.k.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share