Kumrejea Mke Baada Majosho Tatu


 

SWALI:

Ikwa nimempatia mke talaka moja na akapitiwa mke huyo na majosho matatu je nafa kumrejelea tena au mpaka nimuoe kwa mara ya pili.


 

 JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola  wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukran kwa swali lako zuri na mas-ala haya yanakuwa ni matatizo makubwa kwa jamii zetu. Hakika ni kuwa kumrudia mtalaka wako ni kabla ya kumalizika eda yake baada ya hayo majosho matatu au tohara tatu. Eda yake ikimalizika ikiwa bado unaona unamtaka kuishi naye ni lazima upeleke posa upya kwa wazazi wake, naye huyo mwanamke akubali kurudiwa au kuolewa na wewe. Utahitajika kulipa mahari upya kwa kiwango mutakacho kubaliana na kisha ifungwe nikaah mpya.

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share