02-Tawbah Hukmu Na Fadhila Zake: Vipi Kuomba Maghfirah Na Tawbah?

Tawbah Hukmu Na Fadhila Zake

 

02-Vipi Kuomba Maghfirah Na Tawbah?

         

 

 

1-Kuomba Maghfirah Na Tawbah Mara Sabiini Au Mara Mia Kwa Siku:

 

Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  alibashiriwa kufutiwa madhambi yake yaliyotangulia na yaliyo mbele yake. Juu hivyo alikuwa akiomba kila siku maghfirah na tawbah mara sabiini au mara mia.  Kwa hiyo inatupasa sisi tuombe zaidi yake, au angalau mara mia kwa siku.  Hadiyth ya Abuu Hurayrah ifuatayo:

 

 عن أبي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه : سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ : ((وَاللَّهِ إِنِّي لاَسْتَغْفِرُ اللَّهَ وَأَتُوبُ إِلَيْهِ فِي الْيَوْمِ أَكْثَرَ مِنْ سَبْعِينَ مَرَّةً)) رواه البخاري (6307)  

 

Imetoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah  (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)   akisema: ((Wa-Allaahi mimi naomba maghfirah kwa Allaah na kutubia Kwake zaidi ya mara sabiini kwa siku)) [Al-Bukhaariy]

 

 

Na Rasuli wa Allaah  (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akaamrisha watu kuomba maghfirah na kutubia kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) mara mia kwa siku aliposema:

 

 

 ((يَا أَيُّهَا النَّاسُ تُوبُوا إِلَى اللَّهِ وَاسْتَغْفِرُوهُ، فَإِنِّي أَتُوبُ إِلَى اللَّهِ، وَأَسْتَغْفِرُهُ فِي كُلِّ يَوْمٍ مِائَةَ مَرَّةٍ)))   مسلم

 

((Enyi Watu tubieni kwa Allaah na muombe maghfirah kwani mimi natubia kwa Allaah na namuomba maghfirah mara mia kwa siku)) [Muslim]

 

 

 2-Kuomba Maghfirah Na Tawbah Kwa Kuswali Rakaa Mbili:

 

 

Akaamrisha pia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuswali rakaa mbili kwa ajili ya kuomba maghfirah na kutubia kwa Allaah ('Azza wa Jalla):

 

عن أبي بكر الصديق رضي الله عنه قال:  سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: ((ما من رجل يُذْنِبُ ذَنباً، ثمَّ يَقومُ فَيتَطَهَّرُ ويصلي، ثُمَّ يَستَغْفِر اللهَ إِلا غُفِرَ لهُ)) ثم قرأ:   ((وَالَّذِينَ إِذَا فَعَلُوا فَاحِشَةً أَوْ ظَلَمُوا أَنْفُسَهُمْ ذَكَرُوا اللَّهَ فَاسْتَغْفَرُوا لِذُنُوبِهِمْ وَمَنْ يَغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلَّا اللَّهُ وَلَمْ يُصِرُّوا عَلَى مَا فَعَلُوا وَهُمْ يَعْلَمُونَ)) رواه ابو داود و الترمذى والنسائي - وصححه الألباني في صحيح الترميذي وصحيح الترغيب  

Kutoka kwa Abuu Bakr Asw-Swiddiyq (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Yeyote atakayefanya dhambi kisha akachukua wudhuu, kisha akaswali, kisha akaomba maghfirah basi ataghufuriwa)) Kisha akasoma: ((Na wale ambao wanapofanya machafu au wakajidhulumu nafsi zao (kwa maasi), humdhukuru Allaah wakaomba maghfirah kwa madhambi yao. Na nani anayeghufuria madhambi isipokuwa Allaah. Na hawaendelei katika waliyoyafanya na wao wanajua)) [Aal-‘Imraan:  135 – Ameipokea Abuu Daawuwd, At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, na Imesahihishwa na Shaykh Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Tirmidhiy (406) na Swahiyh At-Targhiyb (680)]

 

 

 

3-Kuomba Maghfirah Na Tawbah Kwa Sayyid Al-Istighfaar (Du’aa Adhimu Kabisa Ya Kuomba Maghfirah)

 

 

 

 وعن شداد بن أوس رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم أنه قال: ((سيد الاستغفار أن يقول العبد: اللّهـمَّ أَنْتَ رَبِّـي لا إلهَ إلاّ أَنْتَ، خَلَقْتَنـي وَأَنا عَبْـدُك، وَأَنا عَلـى عَهْـدِكَ وَوَعْـدِكَ ما اسْتَـطَعْـت، أَعـوذُبِكَ مِنْ شَـرِّ ما صَنَـعْت، أَبـوءُ لَـكَ بِنِعْـمَتِـكَ عَلَـيَّ وَأَبـوءُ بِذَنْـبي فَاغْفـِرْ لي فَإِنَّـهُ لا يَغْـفِرُ الذُّنـوبَ إِلاّ أَنْتَ))  رواه البخاري في صحيحه

Imetoka kwa Shaddaad Bin 'Aws  (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)   kasema: ((Du’aa adhimu kabisa ya kuomba maghfirah  ni kusema:    

 

Allaahumma Anta Rabbiy laa ilaaha illaa Anta Khalaqtaniy wa ana ‘abduka wa anaa ‘alaa ‘ah-dika wawa’-dika mastatwa’-tu, a’uwdhu bika min sharri maa swana’-tu, abuw-u Laka bini’-matika ‘alayya wa abuw-u bidhanbiy, faghfir-liy fainnahu laa yaghfirudh dhunuwba illaa Anta

 

((Ee Allaah, Wewe ni Rabb wangu, hapana muabudiwa wa haki ila Wewe, umeniumba mimi na mimi ni mja Wako, nami niko juu ya  ahadi Yako, na agano Lako, kiasi cha uwezo wangu, najikinga Kwako kutokana na shari ya nilichokifanya, nakiri  Kwako kwa kunineemesha, na nakiri kwa madhambi yangu, basi nakuomba unighufurie  kwani hakuna wa kughufuria  madhambi ila Wewe.)) [Al-Bukhaariy]

 

 

 

4-Kuomba Maghfirah Na Tawbah kwa Du’aa Ya Nabiy Yuwnus (‘Alayhis-salaam) alipokuwa tumboni mwa samaki:

 

 

لَّا إِلَـٰهَ إِلَّا أَنتَ سُبْحَانَكَ إِنِّي كُنتُ مِنَ الظَّالِمِينَ ﴿٨٧﴾

“Hapana Muabudiwa wa haki isipokuwa Wewe, Subhaanak! (Utakasifu ni Wako), hakika mimi nilikuwa miongoni mwa madhalimu.” [Al-Anbiyaa: 87]

 

 

5-Kuomba Maghfirah Na Tawbah Kwa Kumsabbih Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):   

 

  قَالَ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((مَنْ قَالَ: سُبْحَانَ اللهِ وَبِحَمْدِهِ فِي يَوْمٍ مائَةَ مَرَّةٍ، حُطَّتْ خَطَاياهُ وَلَوْ كانَتْ مِثْلَ زَبَدِ الْبَحْرِ))

Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ’alayhi wa aalihi wa sallaam amesema: ((Mwenye kusema:Subhaana-Allaahi wa Bihamdihi (Utakasifu ni wa Allaah na Himdi ni Zake) mara mia kwa siku, atafutiwa madhambi yake hata kama yalikuwa mfano wa povu la bahari)) [Hadiyth ya Abu Huraryah (Radhwiya Allaah ‘anhu) - Al-Bukhaariy (7/168) [6405], Muslim (4/2071)]

 

 

6-Kuomba Maghfirah Na Tawbah Kila Baada Ya Swalaah Za Fardhi:

 

 

قال النبي صلى الله عليه وسلم: ((من سبَّحَ اللَّهَ في دُبُرِ كلِّ صلاةٍ ثلاثًا وثلاثينَ وحمدَ اللَّهَ ثلاثًا وثلاثينَ وكبَّرَ اللَّهَ ثلاثًا وثلاثينَ فتلكَ تسعةٌ وتسعونَ وقالَ تمامَ المائةِ لا إلهَ إلَّا اللَّهُ وحدَهُ لا شريكَ لهُ لهُ الملكُ ولهُ الحمدُ وهوَ على كلِّ شيءٍ قديرٌ غُفِرت خطاياهُ وإن كانت مثلَ زَبَدِ البحرِ)) مسلم

 

Amesema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  ((Atakaye sabbih (Subnaaha Allaah) kila baada ya Swalaah mara thelathini na tatu, akaleta takbiyrah (Allaahu Akbar) mara thelathini na tatu, akaleta tahmiyd (AlhamduliLlaah) mara thelathini na tatu akamalizia kwa “Laa ilaaha illa-Allaahu Wahdahu laa shariyka Lah, Lahul-Mulku wa Lahul-Hamdu wa-Huwa ’alaa kulli shay-in Qadiyr - ataghufuriwa makosa yake japokuwa ni mfano wa povu la bahari))  [Hadiyth ya Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) katika Muslim (1/418) [597]

 

 

 

7-Kuomba Maghfirah Na Tawbah Kwa Kutaja Majina Matukufu Kabisa Ya Allaah (‘Azza wa Jalla):

 

 

قَالَ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((مَنْ قَالَ أَسْتَغْفِرُ اللَّهَ الَّذِى لاَ إِلَهَ إِلاَّ هُوَ الْحَىُّ الْقَيُّومُ وَأَتُوبُ إِلَيْهِ؛ غُفِرَ لَهُ وَإِنْ كَانَ فَرَّ مِنَ الزَّحْفِ))

Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)  amesema: ((Atakayesema: Astaghfiru-Allaahal-‘Adhwiyma Alladhiy laa ilaaha illaa Huwal-Hayyul-Qayyuwmu wa atuwbu Ilayhi

Namuomba maghfira kwa Allaah Mtukufu Ambaye Hapana muabudiwa wa haki ila Yeye, Aliyehai daima, Msimamizi wa kila kitu, na ninarejea kutubuia Kwake, Allaah Atamghufuria kama ana makosa hata kama ya kukimbia vitani)) [Hadiyth ya ibn Mas-‘uwd (Radhwiya Allaahu ‘anhu) - Abu Daawuwd (2/85) [1517], At-Tirmidhiy (5/569) [3577], ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh At-Tirmidhiy (3/182)]

 

 

 

 

Share