Imaam Ibn Rajab: Ipi Elimu Yenye Manufaa?

 

Ni Ipi Elimu Yenye Manufaa?

 

Imaam Ibn Rajab (Rahimahu-Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

Imaam Ibn Rajab (Rahimahu Allaah) amesema:

 

 

"Hii elimu yenye manufaa (Diyn) inapelekea katika mambo mawili:

Jambo la kwanza, ni kumjua Allaah na Anayostahiki Yeye kuhusiana na Majina Mazuri na Sifa za juu na Matendo adhimu; nayo inalazimu kumtukuza Yeye, kumuadhimisha, kumkhofu, kumheshimu, kumpenda, kumtegemea, kuridhika na Qadhwaa Yake na kusubiri mitihani Yake.

 

Jambo la pili, ni elimu ya yale Anayoyapenda Yeye (Allaah) na Anayoyaridhia na Anayoyachukia na yale yanayomfanya Yeye kughadhibika miongoni mwa Itikadi na matendo na maneno yaliyo ya dhahiri na yaliyofichika.

Kwa hivyo, inampasa yule mwenye elimu, aharakishe kwa yale Anayoyapenda Allaah na Kuyaridhia, na ajiepusha na yale yenye kumchukiza Allaah na kumghadhibisha.

Kwa hali hiyo, ikiwa elimu italeta tija kwa yule mwenye kuimiliki hiyo elimu, basi hiyo ndio elimu yenye manufaa."

 

[Fadhwl 'Ilm As-Salaf 'Alaa 'Ilm Al-Khalaf Li Ibn Rajab, uk. 7]

 

Share