Imaam Ash-Shaatwibiy - Wanaume (Wanachuoni) Ndio Ufunguo Wa Elimu

Wanaume (Wanachuoni) Ndio Ufunguo Wa Elimu
 
 
Imaam Ash-Shaatwibiy (Rahimahu Allaah) amesema:
 
 
"Na hakika wamesema: 'Hakika elimu ilikuwa katika vifua vya wanaume, kisha ikahamia kwenye vitabu, na funguo zake zikawa katika mikono ya wanaume.'
Haya maneno yanakusudia kwamba hakuna budi kuipata (hiyo elimu) kutoka kwa wanaume, kwani hakuna njia zaidi ya hizo hatua mbili.
Ushahidi wa hili upo kwenye (Hadiyth) Swahiyh (Al-Bukhaariy na Muslim):
'Hakika Allaah Haichukui elimu kwa kuing'oa kutoka kwa watu, lakini Huichukua kwa kuwachukua (roho zao) Wanachuoni..."
Ikiwa hali ndio hivyo, basi hakuna shaka kuwa wanaume (Wanachuoni) ndio wenye kukamata funguo zake (elimu)."
 
 
 
[Al-Muwaafaqaat, mj. 1, uk. 140]
 
Share