Shaykh Fawzaan: Kasumba Haiwi Isipokuwa Kwa Ujahili

 

Kasumba Haiwi Isipokuwa Kwa Ujahili

 

Shaykh Swaalih bin Fawzaan Al-Fawzaan (Hafidhwahu Allaah)

 

Alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

Wanapatikana katika zama hizi, wenye kasumba na watu (Wanachuoni fulani) pamoja na kwamba Haki iko kinyume nao, tunaomba maelekezo ya namna ya kuwanasihi vijana hao, jazaaka Allaahu khayraa.

 

 

 

JIBU:

Tunawanasihi watafute elimu kwanza, kwani wao hawafanyi ta'aswub kwa mtu isipokuwa ni kwa ujahili (kutokuwa na elimu).

Basi ni juu yao kutafuta elimu yenye manufaa na wajifunze shariy'ah ya Dini ya Allaah, na itawabainikia wao Haki in Shaa Allaah.

Ama ikiwa watabaki ni Majaahil au wenye kujifanya ni wenye elimu, basi hili haliwazidishii isipokuwa ikhtilaaf na haiwazidishii isipokuwa mivutano baina yao."

 

 

[Al-Ijaabaat Al-Faaswilah 'Alaa Ash-Shubuhaat Al-Haaswilah, mj. 2, uk. 12]

 

Share