030 - Ar-Ruwm
الرُّوم
Ar-Ruwm: 030
(Imeteremka Makkah)
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
الم ﴿١﴾
1. Alif Laam Miym.
غُلِبَتِ الرُّومُ ﴿٢﴾
2. Warumi wameshindwa.
فِي أَدْنَى الْأَرْضِ وَهُم مِّن بَعْدِ غَلَبِهِمْ سَيَغْلِبُونَ ﴿٣﴾
3. Katika nchi iliyo karibu, nao baada ya kushindwa kwao, watashinda hivi karibuni.
فِي بِضْعِ سِنِينَ ۗ لِلَّـهِ الْأَمْرُ مِن قَبْلُ وَمِن بَعْدُ ۚ وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ ﴿٤﴾
4. Katika miaka baina ya mitatu na tisa. Amri ni ya Allaah Pekee kabla na baada. Na Siku hiyo watafurahi Waumini.
بِنَصْرِ اللَّـهِ ۚ يَنصُرُ مَن يَشَاءُ ۖ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ ﴿٥﴾
5. Kwa Nusura ya Allaah. Anamnusuru Amtakaye, Naye Ndiye Mwenye Enzi na Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Kurehemu.
وَعْدَ اللَّـهِ ۖ لَا يُخْلِفُ اللَّـهُ وَعْدَهُ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٦﴾
6. Ni Ahadi ya Allaah. Allaah Hakhalifu Ahadi Yake, lakini watu wengi hawajui.
يَعْلَمُونَ ظَاهِرًا مِّنَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَهُمْ عَنِ الْآخِرَةِ هُمْ غَافِلُونَ ﴿٧﴾
7. Wanajua yaliyo dhahiri ya uhai wa dunia, lakini wao wameghafilika na Aakhirah.
أَوَلَمْ يَتَفَكَّرُوا فِي أَنفُسِهِم ۗ مَّا خَلَقَ اللَّـهُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا إِلَّا بِالْحَقِّ وَأَجَلٍ مُّسَمًّى ۗ وَإِنَّ كَثِيرًا مِّنَ النَّاسِ بِلِقَاءِ رَبِّهِمْ لَكَافِرُونَ ﴿٨﴾
8. Je, hawatafakari katika nafsi zao? Allaah Hakuumba mbingu na ardhi na vilivyo baina yake isipokuwa kwa haki na muda maalumu uliokadiriwa. Na hakika wengi miongoni mwa watu bila shaka ni wenye kukanusha kukutana na Rabb wao.
أَوَلَمْ يَسِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَيَنظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۚ كَانُوا أَشَدَّ مِنْهُمْ قُوَّةً وَأَثَارُوا الْأَرْضَ وَعَمَرُوهَا أَكْثَرَ مِمَّا عَمَرُوهَا وَجَاءَتْهُمْ رُسُلُهُم بِالْبَيِّنَاتِ ۖ فَمَا كَانَ اللَّـهُ لِيَظْلِمَهُمْ وَلَـٰكِن كَانُوا أَنفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ ﴿٩﴾
9. Je, hawatembei katika ardhi wakatazama jinsi ilivyokuwa hatima ya wale walio kabla yao? Walikuwa ni wenye nguvu zaidi kuliko wao, na walichimbua ardhi, na wakaistawisha zaidi kuliko walivyoistawisha (makafiri), na wakawajia Rusuli wao kwa hoja bayana, na Allaah Hakuwa Akiwadhulumu, lakini walikuwa wakijidhulumu nafsi zao.
ثُمَّ كَانَ عَاقِبَةَ الَّذِينَ أَسَاءُوا السُّوأَىٰ أَن كَذَّبُوا بِآيَاتِ اللَّـهِ وَكَانُوا بِهَا يَسْتَهْزِئُونَ ﴿١٠﴾
10. Kisha uovu ukawa hatima ya wale waliofanya uovu kwa vile walikadhibisha Aayaat za Allaah na walikuwa ni wenye kuzifanyia istihzai.
اللَّـهُ يَبْدَأُ الْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُ ثُمَّ إِلَيْهِ تُرْجَعُونَ ﴿١١﴾
11. Allaah Anaanzisha uumbaji, kisha Anaurudisha, kisha Kwake mtarejeshwa.
وَيَوْمَ تَقُومُ السَّاعَةُ يُبْلِسُ الْمُجْرِمُونَ ﴿١٢﴾
12. Na Siku itakaposimama Saa, wahalifu watakata tamaa.
وَلَمْ يَكُن لَّهُم مِّن شُرَكَائِهِمْ شُفَعَاءُ وَكَانُوا بِشُرَكَائِهِمْ كَافِرِينَ ﴿١٣﴾
13. Na wala hawatokuwa na waombezi miongoni mwa waliokuwa wakiwashirikisha (na Allaah), na wao wenyewe watakuwa ni wenye kuwakanusha washirikishwa wao.
وَيَوْمَ تَقُومُ السَّاعَةُ يَوْمَئِذٍ يَتَفَرَّقُونَ ﴿١٤﴾
14. Na siku itakaposimama Saa, Siku hiyo watafarikiana.
فَأَمَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ فَهُمْ فِي رَوْضَةٍ يُحْبَرُونَ ﴿١٥﴾
15. Ama wale walioamini na wakatenda mema, basi wao watakuwa katika mabustani mazuri wakifurahishwa.
وَأَمَّا الَّذِينَ كَفَرُوا وَكَذَّبُوا بِآيَاتِنَا وَلِقَاءِ الْآخِرَةِ فَأُولَـٰئِكَ فِي الْعَذَابِ مُحْضَرُونَ ﴿١٦﴾
16. Na wale waliokufuru na wakakadhibisha Aayaat Zetu na makutano ya Aakhirah, basi hao katika adhabu watahudhurishwa.
فَسُبْحَانَ اللَّـهِ حِينَ تُمْسُونَ وَحِينَ تُصْبِحُونَ ﴿١٧﴾
17. Basi msabihini Allaah mnapoingia jioni na mnapoingia asubuhi.
وَلَهُ الْحَمْدُ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَعَشِيًّا وَحِينَ تُظْهِرُونَ ﴿١٨﴾
18. Na Ana Himidi katika mbingu na ardhi, na (msabihini pia) mwanzo wa usiku na wakati wa Adhuhuri.
يُخْرِجُ الْحَيَّ مِنَ الْمَيِّتِ وَيُخْرِجُ الْمَيِّتَ مِنَ الْحَيِّ وَيُحْيِي الْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا ۚ وَكَذَٰلِكَ تُخْرَجُونَ ﴿١٩﴾
19. Anatoa kilichohai kutokana na kilichokufa, na Anatoa kilichokufa kutokana na kilichohai, na Anaihuisha ardhi baada ya kufa kwake, na hivyo ndivyo mtakavyotolewa (kufufuliwa).
وَمِنْ آيَاتِهِ أَنْ خَلَقَكُم مِّن تُرَابٍ ثُمَّ إِذَا أَنتُم بَشَرٌ تَنتَشِرُونَ ﴿٢٠﴾
20. Na katika Ishara Zake ni kwamba Amekuumbeni kutokana na udongo, tahamaki mmekuwa watu mnaotawanyika.
وَمِنْ آيَاتِهِ أَنْ خَلَقَ لَكُم مِّنْ أَنفُسِكُمْ أَزْوَاجًا لِّتَسْكُنُوا إِلَيْهَا وَجَعَلَ بَيْنَكُم مَّوَدَّةً وَرَحْمَةً ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ ﴿٢١﴾
21. Na katika Ishara Zake ni kwamba Amekuumbieni katika jinsi yenu wake ili mpate utulivu kwao, na Amekujaalieni baina yenu mapenzi na rahmah. Hakika katika hayo, bila shaka kuna mazingatio kwa watu wanaotafakari.
وَمِنْ آيَاتِهِ خَلْقُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَاخْتِلَافُ أَلْسِنَتِكُمْ وَأَلْوَانِكُمْ ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّلْعَالِمِينَ ﴿٢٢﴾
22. Na katika Ishara Zake ni uumbaji wa mbingu na ardhi, na kukhitilafiana lugha zenu na rangi zenu. Hakika katika hayo, bila shaka kuna mazingatio kwa wenye ujuzi.
وَمِنْ آيَاتِهِ مَنَامُكُم بِاللَّيْلِ وَالنَّهَارِ وَابْتِغَاؤُكُم مِّن فَضْلِهِ ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَسْمَعُونَ ﴿٢٣﴾
23. Na katika Ishara Zake ni kulala kwenu usiku na mchana na kutafuta kwenu Fadhila Zake. Hakika katika hayo, bila shaka kuna mazingatio kwa watu wanaosikia.
وَمِنْ آيَاتِهِ يُرِيكُمُ الْبَرْقَ خَوْفًا وَطَمَعًا وَيُنَزِّلُ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَيُحْيِي بِهِ الْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَعْقِلُونَ ﴿٢٤﴾
24. Na katika Ishara Zake Anakuonyesheni umeme kwa kukutieni khofu na matumaini, na Anateremsha kutoka mbinguni maji, Akahuisha kwayo ardhi baada ya kufa kwake. Hakika katika hayo, bila shaka kuna mazingatio kwa watu wenye akili.
وَمِنْ آيَاتِهِ أَن تَقُومَ السَّمَاءُ وَالْأَرْضُ بِأَمْرِهِ ۚ ثُمَّ إِذَا دَعَاكُمْ دَعْوَةً مِّنَ الْأَرْضِ إِذَا أَنتُمْ تَخْرُجُونَ ﴿٢٥﴾
25. Na katika Ishara Zake, ni kwamba mbingu na ardhi zimesimama kwa Amri Yake, kisha Atakapokuiteni wito mmoja mara mtatoka ardhini.
وَلَهُ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ كُلٌّ لَّهُ قَانِتُونَ ﴿٢٦﴾
26. Na ni Wake Pekee wote waliomo katika mbingu na ardhi, na wote Kwake wanatii.
وَهُوَ الَّذِي يَبْدَأُ الْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُ وَهُوَ أَهْوَنُ عَلَيْهِ ۚ وَلَهُ الْمَثَلُ الْأَعْلَىٰ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿٢٧﴾
27. Naye Ndiye Anayeanzisha uumbaji, kisha Anaurudisha, nayo ni sahali mno Kwake. Naye Ana Sifa za juu kabisa katika mbingu na ardhi. Naye Ndiye Mwenye Enzi na Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.
ضَرَبَ لَكُم مَّثَلًا مِّنْ أَنفُسِكُمْ ۖ هَل لَّكُم مِّن مَّا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُم مِّن شُرَكَاءَ فِي مَا رَزَقْنَاكُمْ فَأَنتُمْ فِيهِ سَوَاءٌ تَخَافُونَهُمْ كَخِيفَتِكُمْ أَنفُسَكُمْ ۚ كَذَٰلِكَ نُفَصِّلُ الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَعْقِلُونَ ﴿٢٨﴾
28. (Allaah) Amekupigieni mfano kwa hali ya nafsi zenu. Je, katika hao iliyowamiliki mikono yenu ya kuume mnao washirika wowote katika vile Tulivyokuruzukuni? Kisha mkawa nyinyi katika hivyo sawasawa, mnawaogopa kama mnavyoogopeana wenyewe kwa wenyewe? Hivyo ndivyo Tunavyofasili waziwazi Aayaat kwa watu wenye akili.
بَلِ اتَّبَعَ الَّذِينَ ظَلَمُوا أَهْوَاءَهُم بِغَيْرِ عِلْمٍ ۖ فَمَن يَهْدِي مَنْ أَضَلَّ اللَّـهُ ۖ وَمَا لَهُم مِّن نَّاصِرِينَ ﴿٢٩﴾
29. Bali wale waliodhulumu wamefuata hawaa zao bila ya ilimu. Basi nani atamhidi ambaye Allaah Amempotowa? Na hawatokuwa na wowote wa kuwanusuru.
فَأَقِمْ وَجْهَكَ لِلدِّينِ حَنِيفًا ۚ فِطْرَتَ اللَّـهِ الَّتِي فَطَرَ النَّاسَ عَلَيْهَا ۚ لَا تَبْدِيلَ لِخَلْقِ اللَّـهِ ۚ ذَٰلِكَ الدِّينُ الْقَيِّمُ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٣٠﴾
30. Basi elekeza uso wako kwenye Dini ukijiengua na upotofu na kuelemea haki. (Shikamana na) umbile la asili la kumpwekesha Allaah Alilowaumbia watu. Hakuna kubadilisha Uumbaji wa Allaah. Hiyo ndio Dini iliyonyooka sawasawa, lakini watu wengi hawajui.
مُنِيبِينَ إِلَيْهِ وَاتَّقُوهُ وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَلَا تَكُونُوا مِنَ الْمُشْرِكِينَ ﴿٣١﴾
31. Mkiwa ni wenye kutubu mara kwa mara kwa ikhlasi Kwake (Allaah), na mcheni Yeye, na simamisheni Swalaah, na wala msiwe miongoni mwa washirikina.
مِنَ الَّذِينَ فَرَّقُوا دِينَهُمْ وَكَانُوا شِيَعًا ۖ كُلُّ حِزْبٍ بِمَا لَدَيْهِمْ فَرِحُونَ ﴿٣٢﴾
32. (Wala msiwe) miongoni mwa wale walioifarakisha dini yaowakawa makundi makundi. Kila kundi wanafurahia waliyonayo.
وَإِذَا مَسَّ النَّاسَ ضُرٌّ دَعَوْا رَبَّهُم مُّنِيبِينَ إِلَيْهِ ثُمَّ إِذَا أَذَاقَهُم مِّنْهُ رَحْمَةً إِذَا فَرِيقٌ مِّنْهُم بِرَبِّهِمْ يُشْرِكُونَ ﴿٣٣﴾
33. Na inapowagusa watu dhara, humwomba Rabb wao huku wakielekea Kwake kwa tawbah na ikhlasi, kisha Anapowaonjesha Rahmah kutoka Kwake, tahamaki kundi miongoni mwao humshirikisha Rabb wao.
لِيَكْفُرُوا بِمَا آتَيْنَاهُمْ ۚ فَتَمَتَّعُوا فَسَوْفَ تَعْلَمُونَ ﴿٣٤﴾
34. Ili wayakanushe Tuliyowapa. Basi stareheni, karibuni mtakuja kujua.
أَمْ أَنزَلْنَا عَلَيْهِمْ سُلْطَانًا فَهُوَ يَتَكَلَّمُ بِمَا كَانُوا بِهِ يُشْرِكُونَ ﴿٣٥﴾
35. Au Tumewateremshia hoja ya wazi ambayo inazungumzia usahihi wa yale waliyokuwa wakimshirikisha Naye?
وَإِذَا أَذَقْنَا النَّاسَ رَحْمَةً فَرِحُوا بِهَا ۖ وَإِن تُصِبْهُمْ سَيِّئَةٌ بِمَا قَدَّمَتْ أَيْدِيهِمْ إِذَا هُمْ يَقْنَطُونَ ﴿٣٦﴾
36. Na Tunapowaonjesha watu Rahmah huzifurahia, na unapowasibu uovu kutokana na iliyotanguliza mikono yao, mara wao wanakata tamaa.
أَوَلَمْ يَرَوْا أَنَّ اللَّـهَ يَبْسُطُ الرِّزْقَ لِمَن يَشَاءُ وَيَقْدِرُ ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ ﴿٣٧﴾
37. Je, hawaoni kwamba Allaah Anamkunjulia riziki Amtakaye, na Anadhikisha (kwa Amtakaye). Hakika katika hayo bila shaka mna ishara kwa watu wanaoamini.
فَآتِ ذَا الْقُرْبَىٰ حَقَّهُ وَالْمِسْكِينَ وَابْنَ السَّبِيلِ ۚ ذَٰلِكَ خَيْرٌ لِّلَّذِينَ يُرِيدُونَ وَجْهَ اللَّـهِ ۖ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ ﴿٣٨﴾
38. Basi mpe jamaa wa karibu haki yake, na masikini na msafiri (aliyeharibikiwa). Hilo ni bora kwa wale wanaotaka Wajihi wa Allaah, na hao ndio wenye kufaulu.
وَمَا آتَيْتُم مِّن رِّبًا لِّيَرْبُوَ فِي أَمْوَالِ النَّاسِ فَلَا يَرْبُو عِندَ اللَّـهِ ۖ وَمَا آتَيْتُم مِّن زَكَاةٍ تُرِيدُونَ وَجْهَ اللَّـهِ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُضْعِفُونَ ﴿٣٩﴾
39. Na mlichotoa katika riba ili kizidi katika mali za watu, basi hakizidi kwa Allaah. Na mlichotoa katika Zakaah mkitafuta Wajihi wa Allaah, basi hao ndio watakaokuwa na ongezeko la maradufu.
اللَّـهُ الَّذِي خَلَقَكُمْ ثُمَّ رَزَقَكُمْ ثُمَّ يُمِيتُكُمْ ثُمَّ يُحْيِيكُمْ ۖ هَلْ مِن شُرَكَائِكُم مَّن يَفْعَلُ مِن ذَٰلِكُم مِّن شَيْءٍ ۚ سُبْحَانَهُ وَتَعَالَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ ﴿٤٠﴾
40. Allaah, Ndiye Amekuumbeni, kisha Akakuruzukuni, kisha Anakufisheni, kisha Atakuhuisheni. Je, kati ya washirika wenu yuko yeyote yule awezaye kufanya lolote katika hayo? Utakasifu ni wa Allaah na Ametukuka kwa ‘Uluwa kutokana na yale wanayomshirikisha.
ظَهَرَ الْفَسَادُ فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ بِمَا كَسَبَتْ أَيْدِي النَّاسِ لِيُذِيقَهُم بَعْضَ الَّذِي عَمِلُوا لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ ﴿٤١﴾
41. Ufisadi umedhihiri katika nchi kavu na baharini kwa sababu ya yale yaliyochumwa na mikono ya watu ili (Allaah) Awaonjeshe baadhi ya waliyoyatenda ili wapate kurejea.
قُلْ سِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَانظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الَّذِينَ مِن قَبْلُ ۚ كَانَ أَكْثَرُهُم مُّشْرِكِينَ ﴿٤٢﴾
42. Sema: Nendeni katika ardhi, mkatazame vipi ilikuwa hatima ya wale waliotangulia. Wengi wao walikuwa ni washirikina.
فَأَقِمْ وَجْهَكَ لِلدِّينِ الْقَيِّمِ مِن قَبْلِ أَن يَأْتِيَ يَوْمٌ لَّا مَرَدَّ لَهُ مِنَ اللَّـهِ ۖ يَوْمَئِذٍ يَصَّدَّعُونَ ﴿٤٣﴾
43. Basi elekeza uso wako kwenye Dini iliyonyooka kabla haijafika Siku isiyo na marudio inayotoka kwa Allaah. Siku hiyo watatengana.
مَن كَفَرَ فَعَلَيْهِ كُفْرُهُ ۖ وَمَنْ عَمِلَ صَالِحًا فَلِأَنفُسِهِمْ يَمْهَدُونَ ﴿٤٤﴾
44. Anayekufuru, basi kufuru yake ni madhara juu yake, na anayetenda mema, basi wanajiandalia mahali pa kupumzika kwa ajili ya nafsi zao.
لِيَجْزِيَ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ مِن فَضْلِهِ ۚ إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الْكَافِرِينَ ﴿٤٥﴾
45. Ili (Allaah) Awalipe wale walioamini na wakatenda mema katika Fadhila Zake. Hakika Yeye Hapendi makafiri.
وَمِنْ آيَاتِهِ أَن يُرْسِلَ الرِّيَاحَ مُبَشِّرَاتٍ وَلِيُذِيقَكُم مِّن رَّحْمَتِهِ وَلِتَجْرِيَ الْفُلْكُ بِأَمْرِهِ وَلِتَبْتَغُوا مِن فَضْلِهِ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ ﴿٤٦﴾
46. Na katika Ishara Zake ni kwamba Anapeleka pepo zenye bishara za kheri, na ili Akuonjesheni katika Rahmah Zake, na ili merikebu ziende kwa Amri Yake, na ili mtafute katika Fadhila Zake, na ili mpate kushukuru.
وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ رُسُلًا إِلَىٰ قَوْمِهِمْ فَجَاءُوهُم بِالْبَيِّنَاتِ فَانتَقَمْنَا مِنَ الَّذِينَ أَجْرَمُوا ۖ وَكَانَ حَقًّا عَلَيْنَا نَصْرُ الْمُؤْمِنِينَ ﴿٤٧﴾
47. Na kwa yakini Tuliwatuma kabla yako Rusuli kwa watu wao, wakawajia kwa hoja bayana, Tukawalipiza wale ambao wamefanya uhalifu. Na ni haki daima Kwetu kuwanusuru Waumini.
اللَّـهُ الَّذِي يُرْسِلُ الرِّيَاحَ فَتُثِيرُ سَحَابًا فَيَبْسُطُهُ فِي السَّمَاءِ كَيْفَ يَشَاءُ وَيَجْعَلُهُ كِسَفًا فَتَرَى الْوَدْقَ يَخْرُجُ مِنْ خِلَالِهِ ۖ فَإِذَا أَصَابَ بِهِ مَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ إِذَا هُمْ يَسْتَبْشِرُونَ ﴿٤٨﴾
48. Allaah Ndiye Ambaye Anatuma pepo za Rahmah kisha zikatimua mawingu, kisha Akayatandaza mbinguni Atakavyo, na Huyafanya mapande mapande. Basi utaona matone ya mvua yanatoka baina yake. Na Anapowafikishia Awatakao kati ya Waja Wake, mara hao wanafurahia.
وَإِن كَانُوا مِن قَبْلِ أَن يُنَزَّلَ عَلَيْهِم مِّن قَبْلِهِ لَمُبْلِسِينَ ﴿٤٩﴾
49. Na kwa hakika walikuwa kabla ya kuteremshiwa (mvua) ni wenye kukata tamaa.
فَانظُرْ إِلَىٰ آثَارِ رَحْمَتِ اللَّـهِ كَيْفَ يُحْيِي الْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا ۚ إِنَّ ذَٰلِكَ لَمُحْيِي الْمَوْتَىٰ ۖ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿٥٠﴾
50. Basi tazama athari za Rahmah ya Allaah! Vipi Anaihuisha ardhi baada ya kufa kwake! Hakika (Afanyayo) hayo, Ndiye bila shaka Mwenye Kuhuisha wafu, Naye juu ya kila kitu ni Muweza.
وَلَئِنْ أَرْسَلْنَا رِيحًا فَرَأَوْهُ مُصْفَرًّا لَّظَلُّوا مِن بَعْدِهِ يَكْفُرُونَ ﴿٥١﴾
51. Na Tungelituma upepo wa madhara na wakaiona (mimea yao) imekuwa manjano, wangeendelea baada ya hayo kukufuru.
فَإِنَّكَ لَا تُسْمِعُ الْمَوْتَىٰ وَلَا تُسْمِعُ الصُّمَّ الدُّعَاءَ إِذَا وَلَّوْا مُدْبِرِينَ ﴿٥٢﴾
52. Basi hakika wewe huwezi kusikilizisha wafu, na wala huwezi kusikilizisha viziwi wito wanapokengeuka wakigeuza migongo yao.
وَمَا أَنتَ بِهَادِ الْعُمْيِ عَن ضَلَالَتِهِمْ ۖ إِن تُسْمِعُ إِلَّا مَن يُؤْمِنُ بِآيَاتِنَا فَهُم مُّسْلِمُونَ ﴿٥٣﴾
53. Na wala wewe huwezi kuwahidi vipofu kutoka upotofu wao. Humsikilizishi isipokuwa yule anayeamini Aayaat Zetu, nao ndio wenye kusilimu (kwa Allaah).
اللَّـهُ الَّذِي خَلَقَكُم مِّن ضَعْفٍ ثُمَّ جَعَلَ مِن بَعْدِ ضَعْفٍ قُوَّةً ثُمَّ جَعَلَ مِن بَعْدِ قُوَّةٍ ضَعْفًا وَشَيْبَةً ۚ يَخْلُقُ مَا يَشَاءُ ۖ وَهُوَ الْعَلِيمُ الْقَدِيرُ ﴿٥٤﴾
54. Allaah Ndiye Ambaye Amekuumbeni kutokana na udhaifu, kisha Akajaalia baada ya udhaifu nguvu, kisha Akajaalia baada ya nguvu udhaifu na ukongwe. Anaumba Atakacho. Naye Ndiye Mjuzi wa yote, Mweza wa yote.
وَيَوْمَ تَقُومُ السَّاعَةُ يُقْسِمُ الْمُجْرِمُونَ مَا لَبِثُوا غَيْرَ سَاعَةٍ ۚ كَذَٰلِكَ كَانُوا يُؤْفَكُونَ ﴿٥٥﴾
55. Na Siku itakayosimama Saa wataapa wahalifu kwamba hawakubakia (duniani) ila saa moja tu. Hivyo ndivyo walivyokuwa wakighilibiwa.
وَقَالَ الَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ وَالْإِيمَانَ لَقَدْ لَبِثْتُمْ فِي كِتَابِ اللَّـهِ إِلَىٰ يَوْمِ الْبَعْثِ ۖ فَهَـٰذَا يَوْمُ الْبَعْثِ وَلَـٰكِنَّكُمْ كُنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ ﴿٥٦﴾
56. Na wale waliopewa ilimu na Iymaan watasema: Kwa yakini mmekaa kwa Majaaliwa na Hukmu ya Allaah mpaka Siku ya kufufuliwa. Basi hii ni Siku ya kufufuliwa, lakini nyinyi mlikuwa hamjui.
فَيَوْمَئِذٍ لَّا يَنفَعُ الَّذِينَ ظَلَمُوا مَعْذِرَتُهُمْ وَلَا هُمْ يُسْتَعْتَبُونَ ﴿٥٧﴾
57. Siku hiyo hautowafaa wale waliodhulumu udhuru wao, na wala hawatapewa nafasi ya kujitetea.
وَلَقَدْ ضَرَبْنَا لِلنَّاسِ فِي هَـٰذَا الْقُرْآنِ مِن كُلِّ مَثَلٍ ۚ وَلَئِن جِئْتَهُم بِآيَةٍ لَّيَقُولَنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا إِنْ أَنتُمْ إِلَّا مُبْطِلُونَ ﴿٥٨﴾
58. Kwa yakini Tumewapigia watu mifano ya kila namna katika hii Qur-aan. Na kama utawaletea (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) dalili yoyote, bila shaka wale waliokufuru watasema: Nyinyi (Waumini) si chochote ila wabatilifu.
كَذَٰلِكَ يَطْبَعُ اللَّـهُ عَلَىٰ قُلُوبِ الَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٥٩﴾
59. Hivyo ndivyo Allaah Anavyopiga chapa juu ya nyoyo za wale wasiojua.
فَاصْبِرْ إِنَّ وَعْدَ اللَّـهِ حَقٌّ ۖ وَلَا يَسْتَخِفَّنَّكَ الَّذِينَ لَا يُوقِنُونَ ﴿٦٠﴾
60. Basi subiri, hakika Ahadi ya Allaah ni haki. Na wala wasikuvunje moyo wale ambao hawana yakini ukataradadi (kubalighisha Risala).
