041 - Fusw-Swilat
فُصِّلَت
Fusswilat: 041
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
حم﴿١﴾
1. Haa Miym.
تَنزِيلٌ مِّنَ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ﴿٢﴾
2. Ni uteremsho kutoka kwa Ar-Rahmaan (Mwingi wa Rahmah), Mwenye Kurehemu.
كِتَابٌ فُصِّلَتْ آيَاتُهُ قُرْآنًا عَرَبِيًّا لِّقَوْمٍ يَعْلَمُونَ﴿٣﴾
3. Kitabu kilichofasiliwa waziwazi Aayaat zake, kikisomeka kwa Kiarabu kwa watu wanaojua.
بَشِيرًا وَنَذِيرًا فَأَعْرَضَ أَكْثَرُهُمْ فَهُمْ لَا يَسْمَعُونَ﴿٤﴾
4. Kinachobashiria mazuri na kinachoonya. Lakini wamekengeuka wengi wao, basi wao hawasikii.
وَقَالُوا قُلُوبُنَا فِي أَكِنَّةٍ مِّمَّا تَدْعُونَا إِلَيْهِ وَفِي آذَانِنَا وَقْرٌ وَمِن بَيْنِنَا وَبَيْنِكَ حِجَابٌ فَاعْمَلْ إِنَّنَا عَامِلُونَ﴿٥﴾
5. Na wakasema: Nyoyo zetu zimo katika vifuniko kwa yale unayotuitia, na masikioni mwetu mna uziwi, na baina yetu na baina yako kuna kizuizi, basi tenda nasi tunatenda.
قُلْ إِنَّمَا أَنَا بَشَرٌ مِّثْلُكُمْ يُوحَىٰ إِلَيَّ أَنَّمَا إِلَـٰهُكُمْ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ فَاسْتَقِيمُوا إِلَيْهِ وَاسْتَغْفِرُوهُ ۗ وَوَيْلٌ لِّلْمُشْرِكِينَ﴿٦﴾
6. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Hakika mimi ni mtu kama nyinyi; hufunuliwa Wahy kwamba: Muabudiwa wenu wa haki ni Ilaah Mmoja, basi thibitini imara Kwake, na mwombeni Maghfirah. Na ole kwa washirikina.
الَّذِينَ لَا يُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَهُم بِالْآخِرَةِ هُمْ كَافِرُونَ﴿٧﴾
7. Ambao hawatoi Zakaah, nao ni wenye kuikanusha Aakhirah.
إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَهُمْ أَجْرٌ غَيْرُ مَمْنُونٍ﴿٨﴾
8. Hakika wale walioamini na wakatenda mema watapata ujira usiokatika.
قُلْ أَئِنَّكُمْ لَتَكْفُرُونَ بِالَّذِي خَلَقَ الْأَرْضَ فِي يَوْمَيْنِ وَتَجْعَلُونَ لَهُ أَندَادًا ۚ ذَٰلِكَ رَبُّ الْعَالَمِينَ﴿٩﴾
9. Sema: Je, hivi nyinyi mnamkufuru Yule Aliyeumba ardhi kwa siku mbili, na mnamfanyia waliolingana Naye? Huyo Ndiye Rabb wa walimwengu.
وَجَعَلَ فِيهَا رَوَاسِيَ مِن فَوْقِهَا وَبَارَكَ فِيهَا وَقَدَّرَ فِيهَا أَقْوَاتَهَا فِي أَرْبَعَةِ أَيَّامٍ سَوَاءً لِّلسَّائِلِينَ﴿١٠﴾
10. Na Akaweka humo milima iliyosimama thabiti juu yake, na Akabariki humo kwa kheri zisizokatika, na Akakadiria humo chakula chake katika siku nne. Ni idadi madhubuti kabisa kwa wanaouliza.
ثُمَّ اسْتَوَىٰ إِلَى السَّمَاءِ وَهِيَ دُخَانٌ فَقَالَ لَهَا وَلِلْأَرْضِ ائْتِيَا طَوْعًا أَوْ كَرْهًا قَالَتَا أَتَيْنَا طَائِعِينَ﴿١١﴾
11. Kisha Akazikusudia mbingu (Kuziumba), nazo ni moshi, Akaziambia pamoja na ardhi: Njooni kwa khiari au kwa lazima. Zikasema: Tumekuja hali ya kuwa tumetii.
فَقَضَاهُنَّ سَبْعَ سَمَاوَاتٍ فِي يَوْمَيْنِ وَأَوْحَىٰ فِي كُلِّ سَمَاءٍ أَمْرَهَا ۚ وَزَيَّنَّا السَّمَاءَ الدُّنْيَا بِمَصَابِيحَ وَحِفْظًا ۚ ذَٰلِكَ تَقْدِيرُ الْعَزِيزِ الْعَلِيمِ﴿١٢﴾
12. Akamaliza kuziumba mbingu saba katika siku mbili, na Akaifunulia kila mbingu jambo lake. Na Tukaipamba mbingu ya dunia kwa taa na hifadhi. Hayo ni Takdiri ya Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mjuzi wa yote.
فَإِنْ أَعْرَضُوا فَقُلْ أَنذَرْتُكُمْ صَاعِقَةً مِّثْلَ صَاعِقَةِ عَادٍ وَثَمُودَ﴿١٣﴾
13. Wakikengeuka, basi sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Nakuhadharisheni radi na umeme angamizi mfano wa radi na umeme angamizi wa kina ‘Aad na Thamuwd.
إِذْ جَاءَتْهُمُ الرُّسُلُ مِن بَيْنِ أَيْدِيهِمْ وَمِنْ خَلْفِهِمْ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا اللَّـهَ ۖ قَالُوا لَوْ شَاءَ رَبُّنَا لَأَنزَلَ مَلَائِكَةً فَإِنَّا بِمَا أُرْسِلْتُم بِهِ كَافِرُونَ﴿١٤﴾
14. Walipowajia Rusuli mbele yao na nyuma yao wakiwaambia: Msimuabudu isipokuwa Allaah, wakasema Angelitaka Rabb wetu, bila shaka Angeliteremsha Malaika. Na hakika sisi tunayakataa mliyotumwa nayo.
فَأَمَّا عَادٌ فَاسْتَكْبَرُوا فِي الْأَرْضِ بِغَيْرِ الْحَقِّ وَقَالُوا مَنْ أَشَدُّ مِنَّا قُوَّةً ۖ أَوَلَمْ يَرَوْا أَنَّ اللَّـهَ الَّذِي خَلَقَهُمْ هُوَ أَشَدُّ مِنْهُمْ قُوَّةً ۖ وَكَانُوا بِآيَاتِنَا يَجْحَدُونَ﴿١٥﴾
15. Ama kina ‘Aad, wao walitakabari katika ardhi bila ya haki, na wakasema: Nani mwenye nguvu zaidi kuliko sisi? Je, hawakuona kwamba Allaah Ambaye Amewaumba Ndiye Mwenye nguvu zaidi kuliko wao? Nao walikuwa wanazikanusha Ishara Zetu.
فَأَرْسَلْنَا عَلَيْهِمْ رِيحًا صَرْصَرًا فِي أَيَّامٍ نَّحِسَاتٍ لِّنُذِيقَهُمْ عَذَابَ الْخِزْيِ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۖ وَلَعَذَابُ الْآخِرَةِ أَخْزَىٰ ۖ وَهُمْ لَا يُنصَرُونَ﴿١٦﴾
16. Basi Tukawapelekea upepo wa dhoruba wenye mngurumo katika siku za mikosi ili Tuwaonjeshe adhabu ya hizaya katika uhai wa dunia. Na bila shaka adhabu ya Aakhirah ni ya hizaya zaidi, nao hawatonusuriwa.
وَأَمَّا ثَمُودُ فَهَدَيْنَاهُمْ فَاسْتَحَبُّوا الْعَمَىٰ عَلَى الْهُدَىٰ فَأَخَذَتْهُمْ صَاعِقَةُ الْعَذَابِ الْهُونِ بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ﴿١٧﴾
17. Na ama kina Thamuwd, wao Tuliwaongoza, lakini walistahabu upofu kuliko hidaaya. Basi ikawachukuwa radi na umeme angamizi wa adhabu idhalilishayo kwa sababu ya waliyokuwa wakiyachuma.
وَنَجَّيْنَا الَّذِينَ آمَنُوا وَكَانُوا يَتَّقُونَ﴿١٨﴾
18. Na Tukawaokoa wale walioamini, na walikuwa wenye taqwa.
وَيَوْمَ يُحْشَرُ أَعْدَاءُ اللَّـهِ إِلَى النَّارِ فَهُمْ يُوزَعُونَ﴿١٩﴾
19. Na Siku watakayokusanywa maadui wa Allaah kupelekwa motoni, nao watapangwa safusafu wa mwanzo wao hadi mwisho wao.
حَتَّىٰ إِذَا مَا جَاءُوهَا شَهِدَ عَلَيْهِمْ سَمْعُهُمْ وَأَبْصَارُهُمْ وَجُلُودُهُم بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ﴿٢٠﴾
20. Mpaka watakapoufikia, yatashuhudia dhidi yao masikio yao, na macho yao, na ngozi zao kwa yale waliyokuwa wakiyatenda.
وَقَالُوا لِجُلُودِهِمْ لِمَ شَهِدتُّمْ عَلَيْنَا ۖ قَالُوا أَنطَقَنَا اللَّـهُ الَّذِي أَنطَقَ كُلَّ شَيْءٍ وَهُوَ خَلَقَكُمْ أَوَّلَ مَرَّةٍ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ﴿٢١﴾
21. Na wataziambia ngozi zao: Mbona mnashuhudia dhidi yetu? Zitasema: Ametutamkisha Allaah Ambaye Ametamkisha kila kitu, Naye Ndiye Aliyekuumbeni mara ya kwanza, na Kwake mtarejeshwa.
وَمَا كُنتُمْ تَسْتَتِرُونَ أَن يَشْهَدَ عَلَيْكُمْ سَمْعُكُمْ وَلَا أَبْصَارُكُمْ وَلَا جُلُودُكُمْ وَلَـٰكِن ظَنَنتُمْ أَنَّ اللَّـهَ لَا يَعْلَمُ كَثِيرًا مِّمَّا تَعْمَلُونَ﴿٢٢﴾
22. Na hamkuwa mkijisitiri hata yasishuhudie masikio yenu, wala macho yenu, wala ngozi zenu, lakini mlidhania kwamba Allaah Hajui mengi katika yale mnayoyatenda.
وَذَٰلِكُمْ ظَنُّكُمُ الَّذِي ظَنَنتُم بِرَبِّكُمْ أَرْدَاكُمْ فَأَصْبَحْتُم مِّنَ الْخَاسِرِينَ﴿٢٣﴾
23. Na hiyo dhana yenu mliyokuwa mkimdhania Rabb wenu, ndiyo imekuangamizeni, na mmekuwa miongoni mwa waliokhasirika.
فَإِن يَصْبِرُوا فَالنَّارُ مَثْوًى لَّهُمْ ۖ وَإِن يَسْتَعْتِبُوا فَمَا هُم مِّنَ الْمُعْتَبِينَ﴿٢٤﴾
24. Basi wakivuta subira, lakini moto ndio makazi yao tu. Na wakiomba wapewe nafasi tena ya kufanya utiifu wa kumridhisha Allaah, basi wao si wenye kuridhishwa na kupewa.
وَقَيَّضْنَا لَهُمْ قُرَنَاءَ فَزَيَّنُوا لَهُم مَّا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ وَحَقَّ عَلَيْهِمُ الْقَوْلُ فِي أُمَمٍ قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِهِم مِّنَ الْجِنِّ وَالْإِنسِ ۖ إِنَّهُمْ كَانُوا خَاسِرِينَ﴿٢٥﴾
25. Na Tuliwawekea marafiki wa karibu, wakawapambia yaliyo mbele yao na ya nyuma yao, na ikawathibitikia kauli wawe pamoja na nyumati zilizopita miongoni mwa majini na wanaadamu. Hakika wao wamekuwa ni wenye kukhasirika.
وَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا لَا تَسْمَعُوا لِهَـٰذَا الْقُرْآنِ وَالْغَوْا فِيهِ لَعَلَّكُمْ تَغْلِبُونَ﴿٢٦﴾
26. Na wale waliokufuru wakasema: Msiisikilize hii Qur-aan na ifanyieni rabsha huenda mkashinda.
فَلَنُذِيقَنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا عَذَابًا شَدِيدًا وَلَنَجْزِيَنَّهُمْ أَسْوَأَ الَّذِي كَانُوا يَعْمَلُونَ﴿٢٧﴾
27. Bila shaka Tutawaonjesha wale waliokufuru adhabu kali, na bila shaka Tutawalipa uovu zaidi wa yale waliokuwa wakiyatenda.
ذَٰلِكَ جَزَاءُ أَعْدَاءِ اللَّـهِ النَّارُ ۖ لَهُمْ فِيهَا دَارُ الْخُلْدِ ۖ جَزَاءً بِمَا كَانُوا بِآيَاتِنَا يَجْحَدُونَ﴿٢٨﴾
28. Hiyo ndio jazaa ya maadui wa Allaah, moto! Watapata humo makazi yenye kudumu. Ndio jazaa kwa sababu walikuwa wakizikanusha Aayaat na Ishara Zetu.
وَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا رَبَّنَا أَرِنَا اللَّذَيْنِ أَضَلَّانَا مِنَ الْجِنِّ وَالْإِنسِ نَجْعَلْهُمَا تَحْتَ أَقْدَامِنَا لِيَكُونَا مِنَ الْأَسْفَلِينَ﴿٢٩﴾
29. Na watasema wale waliokufuru: Rabb wetu! Tuonyeshe wale waliotupotoa miongoni mwa majini na wanaadamu tuwaweke chini ya miguu yetu ili wawe miongoni mwa wa chini kabisa.
إِنَّ الَّذِينَ قَالُوا رَبُّنَا اللَّـهُ ثُمَّ اسْتَقَامُوا تَتَنَزَّلُ عَلَيْهِمُ الْمَلَائِكَةُ أَلَّا تَخَافُوا وَلَا تَحْزَنُوا وَأَبْشِرُوا بِالْجَنَّةِ الَّتِي كُنتُمْ تُوعَدُونَ﴿٣٠﴾
30. Hakika wale waliosema: Rabb wetu ni Allaah, kisha wakathibiti imara, Malaika huwateremkia (kuwaambia): Msikhofu, wala msihuzunike, na pokeeni bishara njema ya Jannah ambayo mlikuwa mkiahidiwa.
نَحْنُ أَوْلِيَاؤُكُمْ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَفِي الْآخِرَةِ ۖ وَلَكُمْ فِيهَا مَا تَشْتَهِي أَنفُسُكُمْ وَلَكُمْ فِيهَا مَا تَدَّعُونَ﴿٣١﴾
31. Sisi ni rafiki zenu walinzi katika uhai wa dunia na katika Aakhirah. Na mtapata humo yale yanayotamani nafsi zenu, na mtapata humo yale mtakayoyahitajia.
نُزُلًا مِّنْ غَفُورٍ رَّحِيمٍ﴿٣٢﴾
32. Ni mapokezi ya takrima kutoka kwa Mwenye Kughufuria, Mwenye Kurehemu.
وَمَنْ أَحْسَنُ قَوْلًا مِّمَّن دَعَا إِلَى اللَّـهِ وَعَمِلَ صَالِحًا وَقَالَ إِنَّنِي مِنَ الْمُسْلِمِينَ﴿٣٣﴾
33. Na nani mwenye kauli nzuri zaidi kuliko yule anayelingania kwa Allaah na akatenda mema na akasema: Hakika mimi ni miongoni mwa Waislamu!
وَلَا تَسْتَوِي الْحَسَنَةُ وَلَا السَّيِّئَةُ ۚ ادْفَعْ بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ فَإِذَا الَّذِي بَيْنَكَ وَبَيْنَهُ عَدَاوَةٌ كَأَنَّهُ وَلِيٌّ حَمِيمٌ﴿٣٤﴾
34. Na wala haulingani sawa wema na uovu. Zuia (uovu) kwa ambalo ni zuri zaidi. Hapo utamkuta yule ambaye baina yako na baina yake kuna uadui, kama ni rafiki mwandani.
وَمَا يُلَقَّاهَا إِلَّا الَّذِينَ صَبَرُوا وَمَا يُلَقَّاهَا إِلَّا ذُو حَظٍّ عَظِيمٍ﴿٣٥﴾
35. Na hapewi hayo isipokuwa wale waliovuta subira, na hapewi hayo isipokuwa mwenye fungu adhimu.
وَإِمَّا يَنزَغَنَّكَ مِنَ الشَّيْطَانِ نَزْغٌ فَاسْتَعِذْ بِاللَّـهِ ۖ إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ﴿٣٦﴾
36. Na utakapokuchochea uchochezi kutoka kwa shaytwaan, basi omba kinga kwa Allaah. Hakika Yeye Ndiye Mwenye Kusikia yote, Mjuzi wa yote.
وَمِنْ آيَاتِهِ اللَّيْلُ وَالنَّهَارُ وَالشَّمْسُ وَالْقَمَرُ ۚ لَا تَسْجُدُوا لِلشَّمْسِ وَلَا لِلْقَمَرِ وَاسْجُدُوا لِلَّـهِ الَّذِي خَلَقَهُنَّ إِن كُنتُمْ إِيَّاهُ تَعْبُدُونَ﴿٣٧﴾
37. Na katika Ishara Zake, ni usiku na mchana, na jua na mwezi. Msisujudie jua wala mwezi, bali msujudieni Allaah Aliyeviumba ikiwa Yeye Pekee mnamwabudu.
فَإِنِ اسْتَكْبَرُوا فَالَّذِينَ عِندَ رَبِّكَ يُسَبِّحُونَ لَهُ بِاللَّيْلِ وَالنَّهَارِ وَهُمْ لَا يَسْأَمُونَ ۩﴿٣٨﴾
38. Lakini wakitakabari, basi wale (Malaika) walio kwa Rabb wako wanamsabbih usiku na mchana, nao hawachoki.
وَمِنْ آيَاتِهِ أَنَّكَ تَرَى الْأَرْضَ خَاشِعَةً فَإِذَا أَنزَلْنَا عَلَيْهَا الْمَاءَ اهْتَزَّتْ وَرَبَتْ ۚ إِنَّ الَّذِي أَحْيَاهَا لَمُحْيِي الْمَوْتَىٰ ۚ إِنَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ﴿٣٩﴾
39. Na katika Ishara Zake, ni kwamba unaiona ardhi imetulia kame, kisha Tunapoiteremshia maji inataharaki na kunyanyuka. Hakika Yule Aliyeihuisha, bila shaka Ndiye Mwenye Kuhuisha wafu. Hakika Yeye juu ya kila kitu Ni Muweza.
إِنَّ الَّذِينَ يُلْحِدُونَ فِي آيَاتِنَا لَا يَخْفَوْنَ عَلَيْنَا ۗ أَفَمَن يُلْقَىٰ فِي النَّارِ خَيْرٌ أَم مَّن يَأْتِي آمِنًا يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۚ اعْمَلُوا مَا شِئْتُمْ ۖ إِنَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ﴿٤٠﴾
40. Hakika wale wanaozipotosha Aayaat Zetu hawawezi kujificha Tusiwaone. Je, basi yule atakayetupwa katika moto ni bora au yule atakayekuja akiwa katika amani Siku ya Qiyaamah? Tendeni mpendavyo, hakika Yeye Ni Mwenye Kuona yote myatendayo.
إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا بِالذِّكْرِ لَمَّا جَاءَهُمْ ۖ وَإِنَّهُ لَكِتَابٌ عَزِيزٌ﴿٤١﴾
41. Hakika wale waliokanusha Ukumbusho ulipowajia (wataangamia). Na hakika Hiki ni Kitabu chenye utukufu na udhibiti.
لَّا يَأْتِيهِ الْبَاطِلُ مِن بَيْنِ يَدَيْهِ وَلَا مِنْ خَلْفِهِ ۖ تَنزِيلٌ مِّنْ حَكِيمٍ حَمِيدٍ﴿٤٢﴾
42. Hakitokifikia ubatili mbele yake wala nyuma yake. Ni Uteremsho kutoka kwa Mwenye Hikmah wa yote, Mwenye Kustahiki Kuhimidiwa kwa yote.
مَّا يُقَالُ لَكَ إِلَّا مَا قَدْ قِيلَ لِلرُّسُلِ مِن قَبْلِكَ ۚ إِنَّ رَبَّكَ لَذُو مَغْفِرَةٍ وَذُو عِقَابٍ أَلِيمٍ﴿٤٣﴾
43. Huambiwi (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) isipokuwa yale yale waliyokwisha ambiwa Rusuli kabla yako. Hakika Rabb wako Ni Mwenye Maghfirah na Mwenye ikabu iumizayo.
وَلَوْ جَعَلْنَاهُ قُرْآنًا أَعْجَمِيًّا لَّقَالُوا لَوْلَا فُصِّلَتْ آيَاتُهُ ۖ أَأَعْجَمِيٌّ وَعَرَبِيٌّ ۗ قُلْ هُوَ لِلَّذِينَ آمَنُوا هُدًى وَشِفَاءٌ ۖ وَالَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ فِي آذَانِهِمْ وَقْرٌ وَهُوَ عَلَيْهِمْ عَمًى ۚ أُولَـٰئِكَ يُنَادَوْنَ مِن مَّكَانٍ بَعِيدٍ﴿٤٤﴾
44. Na lau Tungekifanya kisomeke kwa lugha isiyokuwa ya Kiarabu wangelisema: Mbona hazikufasiliwa waziwazi Aayaat zake? Ah! Cha lugha ya kigeni na hali (Nabiy) ni Mwarabu!? Sema: Hii (Qur-aan) kwa walioamini ni mwongozo na shifaa. Na wale wasioamini, wana uziwi masikioni mwao nayo ni upofu kwao. Hao wanaitwa kutoka mahali mbali.
وَلَقَدْ آتَيْنَا مُوسَى الْكِتَابَ فَاخْتُلِفَ فِيهِ ۗ وَلَوْلَا كَلِمَةٌ سَبَقَتْ مِن رَّبِّكَ لَقُضِيَ بَيْنَهُمْ ۚ وَإِنَّهُمْ لَفِي شَكٍّ مِّنْهُ مُرِيبٍ﴿٤٥﴾
45. Na kwa yakini Tulimpa Muwsaa Kitabu kisha kikahitilafiwa. Na lau si neno lilotangulia kutoka kwa Rabb wako, ingelihukumiwa baina yao. Na hakika wao bila shaka wamo katika shaka nayo (Qur-aan) yenye kuwatia wasiwasi.
مَّنْ عَمِلَ صَالِحًا فَلِنَفْسِهِ ۖ وَمَنْ أَسَاءَ فَعَلَيْهَا ۗ وَمَا رَبُّكَ بِظَلَّامٍ لِّلْعَبِيدِ﴿٤٦﴾
46. Yeyote yule atakayetenda mema basi ni kwa ajili ya nafsi yake, na yeyote yule atakayefanya uovu, basi ni kwa hasara yake mwenyewe, na Rabb wako Si Mwenye Kudhulumu kamwe waja.
إِلَيْهِ يُرَدُّ عِلْمُ السَّاعَةِ ۚ وَمَا تَخْرُجُ مِن ثَمَرَاتٍ مِّنْ أَكْمَامِهَا وَمَا تَحْمِلُ مِنْ أُنثَىٰ وَلَا تَضَعُ إِلَّا بِعِلْمِهِ ۚ وَيَوْمَ يُنَادِيهِمْ أَيْنَ شُرَكَائِي قَالُوا آذَنَّاكَ مَا مِنَّا مِن شَهِيدٍ﴿٤٧﴾
47. Kwake Pekee unarudishwa ujuzi wa Saa (Qiyaamah). Na hayatoki matunda yoyote kutoka mafumbani mwake, na habebi mimba mwanamke yeyote na wala hazai isipokuwa kwa Ujuzi Wake. Na Siku Atakayowaita (Aseme): Wako wapi (hao mnaodai) washirika Wangu? Watasema: Tunakiri Kwako hapana miongoni mwetu anayeshuhudia.
وَضَلَّ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَدْعُونَ مِن قَبْلُ ۖ وَظَنُّوا مَا لَهُم مِّن مَّحِيصٍ﴿٤٨﴾
48. Na yatawapotea yale waliyokuwa wakiyaomba kabla na watayakinisha kuwa hawana mahali pa kukimbilia.
لَّا يَسْأَمُ الْإِنسَانُ مِن دُعَاءِ الْخَيْرِ وَإِن مَّسَّهُ الشَّرُّ فَيَئُوسٌ قَنُوطٌ﴿٤٩﴾
49. Binaadamu hachoki kuomba Du’aa za kheri. Na inapomgusa shari, basi huwa mwenye kukosa tumainio lolote, mwenye kukata tamaa kabisa.
وَلَئِنْ أَذَقْنَاهُ رَحْمَةً مِّنَّا مِن بَعْدِ ضَرَّاءَ مَسَّتْهُ لَيَقُولَنَّ هَـٰذَا لِي وَمَا أَظُنُّ السَّاعَةَ قَائِمَةً وَلَئِن رُّجِعْتُ إِلَىٰ رَبِّي إِنَّ لِي عِندَهُ لَلْحُسْنَىٰ ۚ فَلَنُنَبِّئَنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا بِمَا عَمِلُوا وَلَنُذِيقَنَّهُم مِّنْ عَذَابٍ غَلِيظٍ﴿٥٠﴾
50. Na Tunapomuonjesha Rahmah kutoka Kwetu baada ya dhara iliyomgusa, bila shaka husema: Haya nayastahiki mimi na sidhani kama Saa itasimama. Na kama nitarejeshwa kwa Rabb wangu hakika nitapata mazuri zaidi Kwake. Basi bila shaka Tutawabainishia wale waliokufuru yale waliyoyatenda, na bila shaka Tutawaonjesha adhabu nzito.
وَإِذَا أَنْعَمْنَا عَلَى الْإِنسَانِ أَعْرَضَ وَنَأَىٰ بِجَانِبِهِ وَإِذَا مَسَّهُ الشَّرُّ فَذُو دُعَاءٍ عَرِيضٍ﴿٥١﴾
51. Na Tunapomneemesha binaadamu hukengeuka na kujitenga upande. Na inapomgusa shari, basi mara huwa mwenye Du’aa refu refu.
قُلْ أَرَأَيْتُمْ إِن كَانَ مِنْ عِندِ اللَّـهِ ثُمَّ كَفَرْتُم بِهِ مَنْ أَضَلُّ مِمَّنْ هُوَ فِي شِقَاقٍ بَعِيدٍ﴿٥٢﴾
52. Sema: Je, mnaonaje ikiwa (Qur-aan) ni kutoka kwa Allaah, kisha mkaikufuru, ni nani aliyepotoka zaidi kuliko yule aliye katika upinzani wa mbali?
سَنُرِيهِمْ آيَاتِنَا فِي الْآفَاقِ وَفِي أَنفُسِهِمْ حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَهُمْ أَنَّهُ الْحَقُّ ۗ أَوَلَمْ يَكْفِ بِرَبِّكَ أَنَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ شَهِيدٌ﴿٥٣﴾
53. Tutawaonyesha Ishara na Dalili Zetu katika peo za mbali na katika nafsi zao, mpaka iwabainikie kwamba hii (Qur-aan) ni haki! Je, haitoshelezi Rabb wako kuwa Yeye Ni Shahidi juu ya kila kitu?
أَلَا إِنَّهُمْ فِي مِرْيَةٍ مِّن لِّقَاءِ رَبِّهِمْ ۗ أَلَا إِنَّهُ بِكُلِّ شَيْءٍ مُّحِيطٌ﴿٥٤﴾
54. Tanabahi! Hakika wao wamo katika shaka ya kukutana na Rabb wao. Tanabahi! Hakika Yeye Amekizunguka kila kitu.
